Hatujaelewa nini kuhusu bodi ya MCC?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Hawa Wazungu walileta waangalizi wa uchaguzi Zanzibar October 25, mwisho wa siku nao wakatoa kauli zao za mwisho kua uchaguzi ulikua huru na wa haki,haki itendeke! CCM peke yao dunia nzima wakakataa kata kata kua uchaguzi haukua huru na wa haki! Hawa hawa Wazungu ambao tunawapigia magoti kwa ajili ya misaada wakaonya kua demokrasia itumike kutatua mgororo huo na sio kurudia uchaguzi ila ccm masikio wakayaziba!




Kwanini tuwalaumu Wazungu ilihali hatutaki kutii na kuheshimu mawazo yao? Uwezo hatuna?kila tunachotumia zaidi ya 80% ni kutoka kwao! CCM mtasababisha Wananchi kukosa huduma za bara bara, maji na Umeme mkidhani bila Wazungu mtayaweza!hatufurahii kuikosa misaada hii na wala hatufurahii kua tegemezi lakini tukumbuke kua "hata mbuyu ulianza kama mchicha" tusiharakie kujidai kua tunayaweza huku maandalizi bado ni madogo.



Serikali inakusanya hadi kuvyanz 1.3 trillion kwa mwezi, misharaha tu ya wafanyakazi ni zaidi ya billion 500 kwa mwezi, bado Elimu bure,afya, Umeme,barabara matatizo megine lukuki ambayo ni mahitaji ya kila mwezi!

Hatuangalii kua bado hatujapangilia vyanzo vya kudumu vya mapato yanayiwezesha serikali kukidhi mahitaji yake bila kutegemea wahisani, Hebu tuone aibu kusema kua tutaweza kujitegemea kwa kuangalia mfano wa taifa kubwa tajiri hasa utajiri wa mafuta kama Nigeria lakini bado linategea wahisani kujiendesha, hili ni taifa tajiri Afrika lakini mpaka sasa bado ni tegemezi! Sisi Tunaotegemea makusanyo ya kodi ambazo zilikwepwa miaka iliyopita na bado hatujui wakishalipa wote huko mbeleni titakusanya kiasi gani! Napata wasi wasi tunaweza kurudi kwa mamantilie kule kule kudai kodi.




Kwahiyo wahisani sababu zao ni za msingi, tumekosea sana kwa sababu tu kuna watu hawataki kuona wenzao nao wanastahili kuongoza! Matumizi ya mitandao watumiaji wamekua wanyonge hawako huru kwa mujibu wa haki za binadamu.
Chukulia mfano Kule Marekani CIA wameshindwa kabisa kuingilia kampuni iliyotengeza simu iliyokua inamilikiwa na mtuhumiwa wa ugaidi ili kuifungua kuangalia mawasiliano yake,hii ni kwa sababu ya sheria zao nzuri za mitandao.
 
Back
Top Bottom