Hatua zilizochukuliwa Ubungo ziwe endelevu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatua zilizochukuliwa Ubungo ziwe endelevu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 8, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Maoni ya katuni


  Jana katika safu hii tuliandika tahariri mbili, moja ilibeba kichwa cha habari kinachosema ‘Chonde chonde wachuuzi ondokeni Ubungo Tanesco’ tuliwalenga wachuuzi ambao wametanda katika eneo lote la Ubungo kuanzia njia panda ya barabara ya Maziwa na Morogoro, Ubungo Mataa, mbele ya makao makuu Tanesco, hadi mbele ya kituo cha umeme cha Watsilla.
  Kadhalika tuliwalenga wachuuzi waliotanda barabara ya Mandela kuanzia Ubungo Mataa hadi darajani.
  Tulifikia hatua hiyo kwa kutambua hatari ambayo miaka yote ipo katika eneo hilo; kwa bahati nzuri uongozi wa wilaya ya Kinondoni chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo, ulikuwa umewatangazia wachuuzi hao kuwa waondoke katika eneo hilo kwa kuwa ni hatari kwa usalama wao, lakini pia kwa mitambo ya umeme iliyotanda eneo lote hilo.

  Eneo hilo ndilo kitovu cha mitambo ya umeme jijini Dar es Salaam. Kuna mitambo ya Tanesco, Aggreko, Watsilla, Symbion na Songas. Unapozungumza kitovu cha kusambaza umeme katika gridi ya taifa hakika huwezi kuacha

  kuzungumza Tanesco Ubungo, pamoja na unyeti huu eneo hilo kwa muda mrefu sana limeachwa bila usalama wake kudhibitiwa kiasi ya kuvutia wachuuzi wengi kuendesha shughuli zao kwa kuwa ni eneo linalopitwa na watu wengi kwa sababu kituo kikuu cha mabasi ya mkoani pia kiko maeneo hayo.

  Tunakumbuka Tanesco wamekuwa wakiomba vyombo vya habari na umma kwa ujumla wasaidie kampeni yake ya kuwataka wachuuzi hao waondoke, lakini juhudi hizo hazijazaa matunda yotote ya maana, hali imekuwa mbaya kiasi cha hata watumishi wa Tanesco kushindwa kuingia ofisini kwao kutokana na kupangwa kwa bidhaa barabarani karibu kabisa na lango la makao makuu ya ofisi zao.

  Watumiaji wengine wa barabara ndiyo hali imekuwa mbaya zaidi, ni vigumu waenda kwa miguu kutumia barabara zilizojengwa kwa ajili yao, kuanzia darajani barabara ya Mandela, kwenda makutano ya Sam Nujoma na Morogoro, kuelekea makao makuu ya Tanesco, aghalab waenda kwa miguu wamekuwa wakipishana na magari barabarani kwa

  sababu eneo la watembea kwa miguu lilikwisha kutekwa na kugeuzwa soko la bidhaa za wachuuzi.
  Uchuuzi huu zamani ulikuwa unafanyika saa za jioni na usiku, lakini siku hizi ni kuanzia asubuhi. Ubungo iligeuzwa soko.
  Kwa kweli hakuna ubishi kwamba kila anayejishughulisha mjini anatafuta ruziki yake na wale wanaomtegemea, kwa

  maana hiyo ni dhahiri wachuuzi hawa wapo katika harakati za kujitafutia kipato, ni halali yao kushughulika kwa sababu hata maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile!

  Tunachosema sisi ni kwamba pamoja na juhudi za wachuuzi kujituma ili wapate mkate wao kwa njia halali, tunafikiri kujituma huko ni lazima pia kuzingatie sheria na kanuni za kufanya biashara; kwamba wajiulize je, eneo wanalopanga bidhaa zao limetengwa mahususi kwa ajili hiyo?

  Pia wajiulize kwa kufanya hivyo wanaleta madhara gani kwa watumiaji wengine wa eneo husika?
  Tunasema bila kuficha ukweli, kwamba kufanya biashara au uchuuzi wowote katika eneo tajwa ni hatari kwa usalama wa wachuuzi wenyewe, wateja wao na zaidi sana kwa taasisi zilizoko eneo hilo, hususan mitambo ya umeme.

  Tanesco hivi karibuni walitoa mfano wa kikosi cha zima moto na ukoaji kushindwa kuzima moto uliolipuka kwenye moja ya transfoma zake kituoni hapo kwa sababu ya kukosa sehemu ya kupita.

  Tunaamini kuwa wachuuzi wana maeneo mahususi ambayo yametengwa kwa ajili ya kuendesha shughuli zao, kama vile kwenye masoko yaliyojengwa kwa kazi hiyo, tunaamini kuendelea kuchuuza kwenye maeneo ya waenda kwa miguu, kwenye vituo vya daladala na kugeuza uzio wa kituo kikuu cha umeme cha Ubungo kuwa eneo la kuchuuza kila aina ya bidhaa, ni kuhatarisha usalama wao na wa wakazi wengine wa Jiji la Dar es Salaam, ni kwa jinsi hiyo tunaunga mkono juhudi za kuwahamisha eneo hilo.

  Tunaunga mkono juhudi za kuwataka wachuuzi hawa warejee kwenye maeneo yanayoruhusiwa kuendesha shughuli zao, ili wafanye kazi zao bila kubugudhiwa lakini pia bila kuleta bugudha kwa watu wengine.
  Sambamba na uungaji mkono huu tungependa kuzichagiza taasisi zilizoko eneo hilo, kwa maana ya Tanesco, Songas,

  Watsilla, Aggreko, Shirika la Viwango (TBS), Wizara ya Maji, waache utamaduni wa ovyo wa kuakaa na kushuhudia maeneo yao yakivamiwa na wachuuzi bila kuchukua hatua na mwishowe kujikuta wakigeuka kuwa walalamikaji bila kuchukua hatua zozote za kutatua tatizo husika.
  Tunajua kwa hakika kabisa katika eneo lote la jiji la Dar es Salaam hakuna hata mita moja ya mraba isiyokuwa na mwenyewe, kwa hiyo suala la kuvamiwa kwa maeneo halina nafasi kwa kuwa kila mwenye kumiliki eneo anawajibika kulilinda na kulitunza. Tunataka uwajibikaji sasa na si kelele ambazo hazina tija yoyote.

  SOURCE: NIPASHE
   
 2. THK DJAYZZ

  THK DJAYZZ JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Searching...100%
  Loading...100%
  Network Connected !
   
Loading...