(Makala ifuatayo inapatikana pia kwenye tovuti ifuatayo ya : Uwekezaji Tanzania)
Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango,kufanya maamuzi ya kifedha na kutimiza taratibu kadhaa za kisheria. Wakati mwingine sio lazima kuzifanya hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu.
Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria.
Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi:
- Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan)
- Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara
Tumia fursa za bure za kujifunza zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini.
- Chagua enao sahihi la kuiweka biashara yako.
Tafuta ushauri wa namna ya kuchagua eneo ambalo ni rafiki kwa aina ya biashara unayotaka kufungua na pia ni rafiki kwa wateja watarajiwa. Pia fanya utafiti ili kuweza kuchagua eneo sahihi la biashara yako.
- Tafuta mtaji kwa ajili ya biashara yako
Tafuta mikopo yenye riba nafuu na yenye masharti ambayo utayamudu huku ukizingatia hali yako ya kiuchumi (Usijiingize kwenye mkopo wowote ambao hujui namna ambavyo utaweza kuulipa). Njia mbadala ya kupata mtaji ni kujiunga na kuchangia nguvu na wajasiriamali wenzako au kujiunga na mtu au taasisi yenye fedha ambazo ipo na utayari wa kuziwekeza kwenye biashara/mradi (venture capital).
- Amua mfumo wa kisheria wa umiliki ambao utakaifaa biashara yako
Amua aina ya umiliki ambao ni mwafaka zaidi kwa ajili ya biashara yako: Umiliki binafsi(sole proprietorship), biashara ya ushirikiano(partnership), kampuni(corporation) au chama cha ushirika(cooperative).
- Sajili jina la biashara yako.
Sajili jina la biashara yako katika mamlaka ya usajili wa biashara katika nchi yako ( kwa Tanzania mamlaka husika ni BRELA). Kitendo cha kusajili jina la biashara yako kitaipa biashara mtazamo chanya ( credibility) kwenye macho ya jamii na wateja watarajiwa.
- Jisajili kwenye mamlaka za kodi na pia jisajili kwenye mamlaka za za mji au jiji ili kupata vibali vya kufanya biashara katika eneo husika.
- Jifunze haki na wajibu wa mwajiri na mwajiriwa.
Katika uhai wa biashara yako utahitaji kuajiri wasaidizi na ili kukwepa kufikishwa katika vyombo vya sheria ni vyema ukajifunza haki zako(mwajiri) na haki za mwajiri kwa mujibu wa sheria za nchi mapema ili wakati utakapo fika uweze kuzitimiza kikamilifu.
Mfululizo wa makala zinazochambua kila hatua kwa kina zitafuata hivi karibuni.
WITO
- Kama umependezwa na makala hii tafadhali washirikishe wenzako kwenye mitandao ya jamii.
- Tembelea tovuti yetu kwa ajili ya makala nyingine kama hii: ( Bofya hapa)