Hatua saba muhimu za uponyaji wa CHADEMA!

LENGEJU BOB kama wapenda mabadiliko wote tungekuwa kama wewe basi mgogoro huu ungeonekana mdogo sana. Binafsi nimefurahishwa sana na makala hii. ni matumaini yangu kuwa wahusika watahusoma na kuhufanyia kazi.
 
Last edited by a moderator:
Asante ndugu mpenda mabadiliko.... Naamini hakuna lisilowezekana chini ya jua... ni suala la kuvua ubinafsi na kuvaa uzalendo tu! na Pengine hiki ni kipimo kwa wapenda nchi wote... Tukiamua kufuata msemo wa mwaga mbona namwaga ugali ni sawa! na matokeo yake tutayaona....na tukiamua kuweka mbele maslahi mapana, tunaweza kuokoa jaazi na kuipaisha demokrasia ya Tanzania!
 
Nimeienda hoja yako mwenye kuielewa ataielewa
 
Slaa katoa amri swala hili lisijadiliwe, lakini Godbless Lema na viongozi wengine wamepuuzia amri hiyo ya Slaa...
 
Umenigusa, umenitia Moyo...Asante

Lengeju, kakudanganya demokrasia yaendana na uchumi hivyo uchumi kwanza then demokrasia. Mi ni CCM nina biashara zangu ambzazo zinasahmiri na kumea kwa uwepo wa CCm nina influence kubwa kwa sababu baba yangu ni mjumbe mkuu CCM, halafu wewe unaleta usatwi wa demokrasi wapi bwana.
 
Watu wengine akili zao ziko kwenye kucha, Sasa wakishakata kucha ndo huibuka na nyuzi Kama hizi.
Yaani kurudisha wasaliti kwenye injini ya chama ndo kunusuru chama?
Tunasubiri kwanza, kucha zako ziote ili utupe ushauri wako.
 
Mtoa mada, wewe ni mwanasheria/unasomea sheria, bila shaka ungeweka input ya kisheria katika mada yako ungemake sense zaidi. TUELEZE BWANA LENGAJU, NI KWA VIPI NA NI KWA NAMNA GANI UNAWEZA KUMUWEKA HATIANI ZITTO KABWE KUHUSIKA NA ULE WARAKA?. KWA USHAHIDI UPI?.

Usiogope kusimamia haki ili kuappease kundi fulani, Unaweza vipi kuisifu kamati kuu kufanya maamuzi ya Kijinga, bila hata wewe kujiridhisha ni Ushahidi gani unamuweka katika makosa Zitto?.
 
Nawashukuru wote mlichangia...nawakaribisha wengine wenye mawazo. Suala la Demokrasia ni suala la ustawi wa nchi. Tushirikiane kujenga Nchi yetu! Nawapenda sana....Tuipende Nchi yetu!
 

 
Vita yoyote duniani huwa inakuwa na mshindi hata kama ni baada ya miongo kadhaa. Ila kwa dunia ya sasa wenye busara hujitahidi kuzuia vita isitokee au kukolea pale inapokuwa imeanza kutokea. Kuna msamiati unaitwa MEZA YA MAZUNGUMZO siku hizi ndio ambao ulimfanya Kikwete akatukanwa sana na Kagame.

Katika siasa pia vita za kisiasa ndani ya vyama na zenyewe washindi hupatika. NCCR walipatikana, UDP walipatikana, CUF walipatikana na hata CHADEMA watapatikana. Swali ni je vita hii itakiacha Chama na nguvu ile ile?

Katika nchi vita husababisha wakimbizi, uchumi kuporomoka, majengo kuharibiwa, vifo n.k. Historia inaonyesha palipotokea vita katika vyama Chama kilikufa na kupoteza nguvu na mvuto wake.

Naona Chama kikiwa hatarini hasa kipindi hiki tunapoendelea na uchaguzi wa ndani. Maana kunaweza kutokea kundi la wanaoshindwa kwenye uchaguzi na wanaoshinda.

NAAMINI KATIKA MAZUNGUMZO NA SIO MSHINDI WA VITA ATAKUWA NANI.
 
Mwenye kehima kuokoa maisha, lakini mbabe hujichimbia kaburi lake mwenyewe! Negotiation and compromise is a sign of strength, wisdom and vision.
 

Ndani ya CHADEMA hakuna vita isipokua maamuzi ya kinidhamu.Kama ni vita basi ni kati ya Kanuni,sheria na katiba Vs Watovu wa nidhamu na wahaini waliokiri kosa

Kwa hiyo CHADEMA kuna mchakato wa maamuzi ya kinidhamu na utekelezaji wa maazimio ya kamati kuu juu ya hatua za kinidhamu kuhakikisha chama kinakua kisafi na misingi yake inaheshimiwa tofauti na hivyo vyama vingine

Hakuna Mjadala na watovu wa nidhamu.Hata mimi binafsi nilishawahi kuadhibiwa na hakujawahi kuwa na majadiliano katika kulinda misingi ya uanzishwaji wa chama


Nampongeza Mwanasheria Mkuu wa Chama Tundu Lissu kwa kusimama kidete katika hili.Namuunga Mkono kwa 100%.Hakuna mjadala na wahaini wanaoharibu umoja na mshikamano zaidi ya kuchora mstari mwekundu wa moto
 
unamaanisha kwamba mtu mmoja au hata 50 kama inavyosemekana wako vitani na chama chao , au tuseme wanaipiga cdm ?
 

Bro u truely great great thnker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…