Unajua Africa tukikaa hivi kwa chuki na utengano mwisho wa siku tutabaki kua kama slaves tu kwa hawa jamaa wa western countries, nipo nje kuna stores flani zinaitwa 7/11 kwa walioishi nje watakua wanazijua zipo nyingi sana, ukiingia kuna bango flani hivi la sigara wameonyesha Africa afu sokwe ndio kashika mic anatangaza habari, afu wameandika "This is Africa" yani a direct hit nje tunadharaulika.. Tufikirie kuungana hasa kwa mazuri, kichwani iwepo kunyanyua uchumi kama nchi moja vile ila sio kufikiria kila mtu kufaidika kivyake, at the end kama ilivokua vision ya Ghadhafi Africa ingekua moja tungekua na nguvu sana, we have everything we need na kama huamini hata scientist wapo vichwa vya kutosha tu, hapa nlipo nafahamu lecturers wanne wanafundisha vyuo vikubwa sana duniani ni watanzania, je wa nchi nyingine? We can do everything ourselves ila muungano tusiupuuzie, why hate Kenyans or Ugandans?? i have Kenyan friends, Ugandan friends mbona ni watu wazuri tu, alichokufanyia mkenya moja sio wakenya wote, kwani mtanzania mwenzako hajawahi kufanyia ubaya? si uchukie watanzania wote sasa kama ni hivo. Think of realizing your dreams n not hatred, that way utakua angalau umepunguza shida moja kwenye taifa lako..