Hatma ya pombe zenye vifungashio vya plastiki (Viroba)

Hatma ya pombe zenye vifungashio vya plastiki (Viroba)

wiser1

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
2,604
Reaction score
3,982
Habari wakuu,

Naimani wote mko salama na hata walioktk shida ngumu Mungu awajaalie yaliyomema na kufuta machozi yao.

Rejea somo tajwa, natambua miezi kadhaa imepita tangu pombe ya viroba kusitishwa rasmi nchini huku asilimia kubwa ya wafanyabihashara wakiachwa ktk madeni makubwa na wengine kulaani kitendo hiki!

Swali: Kitendo hiki serikali ilikurupuka ama ilimaanisha kuzuia?

Baadhi ya maeneo mengi wamekuwa wanauza pombe hii kisiri siri na wengine kufungua kabisa na kuuza zikiwa kwa glass!

Nini hatima ya wafanyabihashara ambao waliambiwa kusubiria maelekezo mengine?

Je wafanyabihashara hawa walifungua kesi popote kushtaki serikali?

Karibuni wadau tujadiliane ili km wapo waliofungua kesi pia tufahamu kesi zao zinaendeleaje.

Na pia wale wazazi ambao vijana wao walikuwa wanakunywa viroba kwa wingi wameacha? au hali ikoje kwa sasa?

Na huku mitaani tulipo kuzuiwa kwa viroba kumeleta faida na hasara zipi?

wiser1
 
Tulishajadili sana mambo ya viroba... Ila ngoja tuwasubiri waje
 
Hii issue imeleta usumbufu sana kwa watu, viroba hivyo vina nembo ya TBS, TFDA na TRA n.k
 
Wapige marufuku na sigara bila kujali kodi ya sigara ili tuone kama kweli ni wazalendo na wanawapenda wananchi, kwani ni hatari kwa afya za jamii,
Mkuu umesema kweli kabisa manake hata mimi nitaacha masigaret, manake nilikuwa mshabiki wa viroba sasa hivi hakuna nakunywa biere yaani nilikuwa siwezi kulala bila viroba , mh maja zuia masigareti unitoe kifungoni
 
Kwangu mm bora vimezuiliwa maana hata afya za waliokua wameathiriwa na matumizi ya viroba zimeimarika tangu kukatazwa kwake...
 
Juzi kuna sehemu nimekaa nikasikia jamaa anamwambia mihudumu nipe, Nipe dangote nikajiuliza pale kina hardware au? Kumbe ndo jina la viroba
 
Kwangu mm bora vimezuiliwa maana hata afya za waliokua wameathiriwa na matumizi ya viroba zimeimarika tangu kukatazwa kwake...
Naona uchaguzi mkuu unaokuja 2020 vijana watakuwa wanajitambua,uchaguzi uliopita vijana walipiga kura huku wakifyonza viroba wengine walikesha wanafyonza kura zikaharibika.
 
Walifanya jambo la msingi kuvizuia kwa maana baadhi ya vijana walikuwa wanaharibikiwa tu, kisa viroba
 
Juzi kuna sehemu nimekaa nikasikia jamaa anamwambia mihudumu nipe, Nipe dangote nikajiuliza pale kina hardware au? Kumbe ndo jina la viroba
aseee kumbe jina linabadilika kulingana na maeneo!
 
Back
Top Bottom