Chishango
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 875
- 363
Baada ya kutokea sintofahamu katika uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga uliokuwa ufanyike leo asubuhi uchaguzi huo umehairishwa mpaka utakapotangazwa tena. Chanzo cha uhairishaji huo ni kutokana na katibu wa CCM wilaya ya mbinga kwa ushawishi wa mwenyekiti wa CCM mkoa Ndg Oddo Mwisho ambaye ana mahusiano nae ya kimapenzi hali iliyopelekea katibu huyo kupeleka mapendekezo feki kwenye kamati ya siasa ya mkoa tofauti na yale yaliyopitishwa na kamati ya siasa ya wilaya ambayo yalisababisha mgombea anayekubalika kukosa sifa na kuondolewa. kitendo hicho kiliwaudhi madiwani wengine ambao walitishia kukihama chama hicho na kuhamia CHADEMA kama jina la mgombea huyo lisiporudishwa Kimsingi mwenyekiti wa CCM wa mkoa ndiye alikuwa mwnyekiti wa halmashauri ya MBINGA kabla haijagawanywa na sasa anagombea kwa upande wa Nyasa. hali ilikuwa mbaya asubuhi ya leo baada ya kundi la vijana kuzingira ofisi za CCM na madumu ya petrol kwa lengo la kuwachoma moto madiwani watakaoshiriki uchaguzi huo kabla hawajatawanywa na polisi
Nawasilisha wadau
Nawasilisha wadau