Hatimaye TFF waipa Simba barua ya hukumu na kuwataka waende FIFA

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,288
15,238
Hatimaye TFF waipa Simba SC barua ya hukumu na kuwataka waende FIFA hata leo kama wakiona wameonewa.

Kipengele muhimu ktk barua ya TFF kinasema :

" Mohamedi Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano ...."

Sasa wale wajumbe wa kamati ya masaa 72 waliosema mchezaji ana kadi tatu waliziona wapi ?

4b4f5c40591650a61a008342a1f88482.jpg
 
Hawa nao waongo. Mbona kwenye press conference walisema simba wamepokwa point kwa vile hawakulipia rufaa yao?

Kwa hiyo maamuzi yao yametokana na kagera kwaambia kirahisi tu kuwa mchezaji wao hakuwa na kadi tatu? Kama haya ndiyo maamuzi ya kamati ya katiba na sheria. Na kama refa wa kati ripoti ya yake ilionyesha Faki alikuwa na kadi ya njano siku ya mchezo na Lyon basi kwa mujibu wa kanuni za FIFA, maamuzi ya refa kwa kati ni ya mwisho. Hivyo simba watashinda kirahisi hii rufaa FIFA. Ikumbukwe FIFA wanatambua maamuzi ya refa wa kati tu na si yale maelezo ya kagera sugar.
 
Mbona mnageuka sasa?

Si mlitaka TFF iwaambie kama Fakhi alikuwa na kadi au la?

Sasa taarifa hiyo hapo, Fakhi hakuwa na kadi 3.
 
Malinzi kaharibu soka la TZ kama alivyoboronga kule Yanga. Kila siku migogoro na maamuzi ya hovyo. Muda umefika akae pembeni
 
Mbona mnageuka sasa?

Si mlitaka TFF iwaambie kama Fakhi alikuwa na kadi au la?

Sasa taarifa hiyo hapo, Fakhi hakuwa na kadi 3.

shida siyo point 3 mkuu. Ni hivi mara baada ya kamati iliyotengua hizo point 3 alizopewa simba sababu yao kubwa ilikuwa simba walikata rufaa nje ya muda unaoruhusiwa na vilevile hawakulipia rufaa yao. Wakaenda mbali zaidi na kututhibitishia kuwa faki alikuwa na kadi tatu na hataruhusiwa kucheza mchezo unaofuata. Sasa mbona wamegeuka kile walichokisema? Huwezi kuhoji eti watu mbalimbali wakati ripoti ya mwamuzi na kamisaa vipo.
 
TFF malinzi au ipi? malinzi = mainzi
a. raisi wa kagera
b. raisi wa tff
c. katibu Mkuu yanga
d. yote juu Sawa

jibu ni .....
 
Pale TFF hakuna uongozi wa mpira ila ni uongozi wa Yanga tu pale. Hata aibu hana timu yetu ya taifa kuburuza mkia? Nafikiri hata wewe mtoa mada unapaswa ujiite MKIA maana haiwezekani TFF inatufanya wote tuitwe mikia kwa uendeshaji wa ovyo wa soka letu.
 
Kaburu nae kawa yanga wakati ni makamu mwenyekiti wa simba!
 
Rufaa imekatwa TFF majibu yanatolewa na bodi ya ligi tujuzeni wanaojua sheria za tff ni sahihi
 
Hawa nao waongo. Mbona kwenye press conference walisema simba wamepokwa point kwa vile hawakulipia rufaa yao?

Kwa hiyo maamuzi yao yametokana na kagera kwaambia kirahisi tu kuwa mchezaji wao hakuwa na kadi tatu? Kama haya ndiyo maamuzi ya kamati ya katiba na sheria. Na kama refa wa kati ripoti ya yake ilionyesha Faki alikuwa na kadi ya njano siku ya mchezo na Lyon basi kwa mujibu wa kanuni za FIFA, maamuzi ya refa kwa kati ni ya mwisho. Hivyo simba watashinda kirahisi hii rufaa FIFA. Ikumbukwe FIFA wanatambua maamuzi ya refa wa kati tu na si yale maelezo ya kagera sugar.
sasa MEZANI FC wakalipe dollar 15,000/= ili wacheze KARATA TATU
 
Pale TFF hakuna uongozi wa mpira ila ni uongozi wa Yanga tu pale. Hata aibu hana timu yetu ya taifa kuburuza mkia? Nafikiri hata wewe mtoa mada unapaswa ujiite MKIA maana haiwezekani TFF inatufanya wote tuitwe mikia kwa uendeshaji wa ovyo wa soka letu.
Ni kama vile Kamati ya masaa 72 ni simba tupu
 
Mikia ni wote tu hata yanga ni mikia maana kila wakicheza kimataifa wanashika mkia. Taifa stars ya Malinzi nayo ni mkia ndani ya E.A. Habari ya kuitana mikia mkome kabisa, maana soka la bongo ni kichwa cha mwandawazimu. Tuombe serengeti boys wafute hili tatizo la mkia.
 
Back
Top Bottom