ile kurupuka ya serikali ya awamu ya tano sasa imewatokea puani, wameamliwa na Bunge kuleta mpango wa mwaka mmoja kwa maana ya 2016/ 17 na ule wa muda mrefu wa miaka mitano kama ilivyokuwa imeombwa asubuhi na wabunge zitto kabwe na tundu lissu.
watumbua majipu ya uongo acheni kukurupuka, fuateni sheria na taratibu.
====================
watumbua majipu ya uongo acheni kukurupuka, fuateni sheria na taratibu.
====================
Serikali imeuwasilisha na kuuondoa mpango wa pili wa maendeleo ya taifa
Serikali imeuwasilisha na kuuondoa mpango wa pili wa maendeleo ya taifa kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kubainia kuwa kuna kanuni na tararibu ambazo zimekiukwa katika kuwasilisha mpango huo bungen.
Mpango huo ambao uliwasilishwa bungeni na waziri wa fedha na mipango Mh Dk Philip Mipango ulibainisha mapendekezo ya mwelekeo wa pili wa maendeleo kwa miaka mitano ijayo ya serikali kwa kipindi cha miaka.
Baada ya waziri wa fedha kuwasilishwa mpango huo Mh Zitto kabwe na Mh Tundu Lissu walioamba miongozo juu ya jambo hilo.
Hata hivyo mwenyekiti wa bunge Mh Andrew Chenge aliwaambia wabunge hao kuwa jambo hilo amelichukua anahitaji muda kulifanyia kazi nahivyo kuruhusu taratibu zingine kuendelea na ulipofika muda wa kambi ya upinzani kuwasilisha hotuba yao wakagoma.
Kisha Mh Chenge akalazimika kuahirisha bunge kablya ya muda.
Baada ya kuahiriswa kwa kikao hicho na bungeni kurejea jioni ndipo waziri mwenye dhamana alipoamua kuondoa mpango huo bungeni.
Kufuatia hatua hiyo baadhi wabunge hasa wa upinzani akiwemo Mh James Ole Milya amesema kitendo cha kuondolewa kwa hoja hiyo ni ishara nzuri kwa serikal i kuwa imeanza kuyafanyia kazi mawazo yao.
ITV ilimtafuta waziri wa katiba na sheria Mh Dk Harrison Mwakyembe ambaye amesema kilichotoke ni tatizo la kiufundi tuu na jumatatu litarekebishwa.
Awali waziri wa fedha Mh Dk Philip Mipango aliwasilisha mpango huo na kubainisha mambo mbalimbali na maendeleo kwa kipindi cha 2016/2017