ItsMi
Member
- Sep 13, 2021
- 66
- 31
Vijana hii ni fursa nyingine tena. Kwa kuwa Kipindi kirefu kilichopita wasnii waliokuwa wakifanya sanaa zao na kuziuza au pengine kuuziwa na madalali huku wakiambulia patupu pasipo kuipata haki yao ya msingi lakini hivi sasa taasisi inayohangaikia hakimiliki za wasanii (cosota) pamoja na basata ikiungwa mkono na sekta zingine za kiserikali wameweza kuanzisha mpango mkakati wa kuwalipa mirahaba wasanii wanaofanya kazi za sanaa nchini.
Hivi sasa wamekua vitani bega kwa bega na wasanii kuhakikisha haki za wasanii hao zinapatikana kwa kuwalipa kinachowastahili Ikiwa kama faida wanayoipata mara baada ya kazi zao kutumika na baadhi ya Vyombo vya habari na burudani lengo kubwa likiwa ni kumshika mkono msanii kumnufaisha na kile ambacho ni jasho lake ambalo hapo mwanzo lilimwagika pasina kumpatia manufaa aliyostahili zaidi ya hapo.
Hivyo nitoe pongezi kwa Cosota na basataa pamoja na serikali kwa ujumla wake ambao ndio wamekua wakilihangaikia swala hili kwa kulipa kipaombele swala hili na hatimae limefanikiwa na tayari wasanii wanaanza kunufaika.
Hivyo kwa wale wazazi waliodhani sanaa hailipi na kuwakataza vijana wao kujihusisha na sanaa niseme tu kwamba sasa ni wakati wa mabadiliko yaliyosubiriwa kwa miaka mingi kwenye nyanja ya sanaa na utamaduni.
Ni ombi langu kwamba waruhusu vijana wao pale inapobidi waweze kufanya vile vikubwa vilivyo ndani ya uwezo wao kwa kuwa ni vipaji mungu amewapa tuzidi kuwashika mikono na kamwe tusiwakatishe tamaa.
Asanteni