Katika pilika pilika za maisha kama kuna jambo limetokea siku zote tunapaswa kuangalia ni CHANZO CHAKE na MATOKEO YAKE. Chanzo cha mahangaiko yote haya uliyoyapata na madhila uliyoyasababisha kwa Bajaji na abiria wake na hadi Boda Boda ni WEWE, UZEMBE WAKO wa kuendesha gari bila kuzingatia sheria umesababisha matatizo kwako na kwa wengine. Laiti kama ungeendesha chombo chako kwa kuzingatia sheria za barabarani yote yasingetokea. Unapotafakari umejifunza nini kwenye hili usijikite kwa jinsi ulivyoponyoka mikononi mwa Boda boda na polisi, (Matokeo) bali jikite jinsi gani UBADILIKE (Chanzo) ili siku nyingine usisababishe ajali, majehuri na vifo kwa wengine,
Pamoja na kwamba wengi wanawalaumu BodaBoda kwa uendesahji wao, lakini kuna kundi kubwa la vijana waendesha magari hasa madogo madogo kama IST, Vitz, Sieta, Olpa, Wish, Passo ambao nao hawana tofauti na Boda Boda kama mleta mada hapa, wanaendesha kwa fujo, kwa kasi isiyo lazima wakati hana sababu zozote za kwenda mwendo wa kasi kama huo.
Kumbuka CHANZO NI WEWE TANGU MWANZO HAYA MWENGINE NI MATOKEO TU. Hivyo usihangaike na matokeo bali hangaika na chanzo.