Hatimaye kesho ligi ya uingereza inaisha. Yafuatayo ndo uchambuzi wangu wa kina

dume la kenge

Senior Member
Apr 12, 2017
177
232
1. Kuna timu inayofananishwa na mwanamume anayetumia nguvu nyingi kutafuta hela mchana, alafu ikifika usiku anazimwaga kiulaini kwa malaya. Hii timu ilitumia nguvu nyingi kuwafunga zile big 5 huku anajiachia kiulaini kwa timu mbovu. mwishowe akapoteza ubingwa. 2. Kuna timu inayofananishwa na bibi kizee aliyekutana na chatu, yaani hawezi akakimbia wala kupiga kelele kwa nguvu manake nguvu hazimo tena. Hii ndo timu pekee yenye huruma uingereza nzima. Hataki akufunge wala umfunge, na ikitokea akakifunga kipindi cha kwanza lazima akuachie mwishoni mwa mchezo. Yaani ni masikini jeuri, naye amepoteza ubingwa. 3. Kuna timu inayofananishwa na mnyama pori aina ya ngiri. Huyu mnyama anapokuwa anakimbizwa na simba anakimbia sana mpaka anamuacha simba umbali mrefu kabisa ila baadaye anajisahau kwamba alikua anakimbizwa, anaanza kuchunga kama kawaida mwishowe anakamatwa kiulauni.
Hii timu inaanza msimu kwa kasi katikati anajisahau mwishoni anakuwa moto wa kuotea mbali. Yeye pia akapoteza ubingwa. 4. Kuna timu inayofananishwa na binti mzuuuuri ,mrembo asiye na kosoro yoyote ile ,lakini ameshendikana kuolewa. Kwake kila mwaka ni moto wa kuotea mbali, lakini mwisho wa siku hapati hata kale ka kombe ka mbuzi. Good for nothing, sawa na mwanafunzi ambaye kila swali darasani analijua na analijibu kwa ufasaha lakini ikifika kwenye mtihani, wajanja wanampita kiulaiiini. 5.kuna timu inayofananishwa na mwanaridha mpumbavu, anayekwenda kwenye mashindano huku anajiamini 100% kwamba atashinda kisa tu anamiguu mirefu. Hawa walianza msimu kwa kujiamini kwamba kombe ni lao kisa tu wana kocha wa kimataifa , mwenye rekodi kibao. Ligi inaisha hawana hili wala lile. 6. Kuna timu inayofananishwa na mtoto wa masikini anayejitambua, aliyepelekwa shule akasoma ili aweze kukomboa familia kwa ujumla dhidi ya janga la umasikini. Hii timu ilianza kwa changamoto, baadaye wakaka kwa pamoja kocha mkuu ,wachezaji pamoja na viongozi wengine wakakubaliana kwamba njia peke ni kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano miongoni mwa wachezi pamoja na kocha. Hatimaye wakashinda ligi.
 
Namba 6 haileti maana, kusema timu inafananishwa na mtoto wa masikini?? Hujaitendea haki Chelsea maana hawa ni big spenders kuanzia manunuzi mpaka mishahara.
Atleast ungesema ni mtoto wa tajiri ambaye hakubweteka na utajiri wa nyumbani kwao, akakaza msuli akatoboa!!

Mtazamo tu.
 
Namba 6 haileti maana, kusema timu inafananishwa na mtoto wa masikini?? Hujaitendea haki Chelsea maana hawa ni big spenders kuanzia manunuzi mpaka mishahara.
Atleast ungesema ni mtoto wa tajiri ambaye hakubweteka na utajiri wa nyumbani kwao, akakaza msuli akatoboa!!

Mtazamo tu.
Nakubaliana na mawazo yako Mkuu ingawa sikumaanisha umasikini wa kifedha kwa Chelsea, najaribu tu kulinganisha kujituma kwake na anavojituma mtoto wa masikini.
 
Back
Top Bottom