Hatimaye 'imevuja' rasmi Kujaa hadi 'Pomoni' vile kwa Mzee Mkapa 'Wapuuzi Day' kumbe ukikutwa nje unapewa Jezi ya 'Kubumba' na Kuingizwa bure!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,877
Nilishangaa sana na mno kwani Mashabiki wa Nyani Mbwa Sokwe FC ninaowafahamu Mimi Kwanza hawana Hela (nikimaanisha wengi wao ni Masikini na Choka Mbaya) kama Mimi GENTAMYCINE halafu pia ni 'Wabahili' kumzidi hata Kocha Arsene Wenger na Profesa Ibrahim Lipumba eti 'wamethibutu' kabisa 'Kuujaza' ule Uwanja katika Kilele chao cha 'Wapuuzi Day' Jumapili iliyopita.

Sasa mkiambiwa kuwa duniani hakuna 'Siri' tena taarifa kutoka kwa Watu wasiopenda kabisa Uwongo na Sifa za 'Kijinga' waliopo huko huko kwa waliokuwa na 'Wapuuzi Day' wamesema kuwa ili Kuwajibu Simba SC na 'Kutoaibika' kwa 'Dimba' la Hayati Temeke Stadium 'Kutokujaa' ilibidi zitengenezwe Jezi za 'Kubumba' kisha zigawiwe kwa Watu waliokuwa nje na Kuamriwa Kuingia bure.

Najua kama kawaida kuna ambao 'Mtabisha' hapa hivyo nawaombeni nendeni pale ilipo Baa ya Mianzini mumtafute Sele 'Kiguru' na wengine nendeni pale Baa ya kwa Chichi mtafuteni Mtu aitwae Kambarage ambao hawa wote huwa ni Waangalizi wa 'Magari' yenu mnayopaki pale ili wawapeni Ukweli huu wote na mengineyo ambayo hamkuyajua kama ya hadi 'Kuroga' Mechi ile tu ya Jana.

Taratibu sasa mnaanza Kuumbuka na Kuumbuana pia!
 
Tunawashukuru sana GSM na Eng. Hersi Said!
IMG-20200831-WA0099.jpg
 
Back
Top Bottom