Hatimae Dstv Wamenipigia Simu

Marumeso

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
1,410
1,322
Wakuu katika hali isiyo ya kawaida nimepigiwa simu na dstv wakidai eti wananikumbusha tarehe ya malipo imefika.

Baada ya sim hii nimejiuliza maswali mengi sana hasa ikizingatiwa hawa jamaa walikuwa wana huduma mbovu sana kwa wateja unaweza kuwa na tatizo ukawapigia wasipokee na au wakakupa majibu ya bora liende. Nikajiuliza kuna nini kimewasibu kiasi siku hizi wanafikia hatua ya kuwapigia simu wateja na kuongea kwa upole?

Ni kwamba wameingiwa na malaika kiasi wamebadilika hadi wanasaka wateja kiasi hicho au nao wanaogopa kutumbuliwa?
 
Sababu bila ya kumumunya maneno ni AZAM TV......bigup Tido. Ya taifa wanajuta.

Tunajuwa kuna jipu huko ya taifa lakini wanangoja tusahau mambo ya LIVE halafu walitumbue. Mlamuwa tu tonge kabla hawajatutumbua.
 
Walizidi bei za vifurushi vyao imekua ni mzigo usiobebeka
Mambo ya kulipa kwa dolari halafu kila siku wanapandisha bila Taarifa acha waisome namba
Ni mwendo wa Azam Tv tu..!
 
Hawa Dstv wangefanya kama kampuni za simu...yaani tuweze kununua kifurushi kwa week au siku ...85000 kwa mwezi ni nyingi saana.Wafanye utafiti na waendane na hali halisi ya mtanzania.
 
mbona kawaida tu...wanakawaida ya kuwapigia wateja wao kila mwezi...kama malipo yanakaribia au yameisha haujalipia lazima wakupigie....kusema kweli huduma zao kwa wateja ni bora kuliko azam..Azam kuwapata ni issue na ukiwapata sometimes unaweza usitatuliwe tatizo mpaka uwapigie zaidi ya mara tatu...
 
Back
Top Bottom