Hatima ya ukombozi wa Tanzania itaamuliwa na mfumo

Hatima ya ukombozi wa Tanzania itaamuliwa na mfumo

Eliso

New Member
Joined
Apr 23, 2025
Posts
1
Reaction score
0
Ugonjwa mkubwa wa Tanzania upo katika mfumo wa uendeshaji wa hili taifa,ukiiponya mifumo
umeliponya taifa.

Tanzania haimuitaji Tundu Lissu,haimuitaji Zitto Wala Lungwe,haiwaitaji CHADEMA,CHAUMMA au CCM Ili iwe na maendeleo ya kijamii au kiuchumi bali inahitaji mifumo Bora ya uendeshaji wa Taifa ambayo inatakiwa ianze na mabadiriko ya Katiba iliyopo Sasa hivi.

Ninasisitiza mabadiriko wa mfumo kama njia mbadala ya kulikuza taifa letu na kuwa bora kwa sababu, watu wema wanaweza wakawepo katika serikali inayoundwa na chama chochote kile lakini mfumo uliopo ukawafanya nao wawe wabaya na wasioneshe wema wao,hivo hivo watu wabaya watakuwepo katika mfumo mbaya na watautumia watakavo bila kujali chama kilichopo madarakani kinaongozwa na mtu mwema.

Maana yangu ni kwamba CCM Ina watu wema ila mifumo haiwaruhusu wao kuwa wema,CHADEMA, ACT, CHAUMMA,NCCR nao wanaweza kuwa wanahubiri yaliyomo mema lakini siku wakipewa hii nchi nao wana watu wabaya ndani Yao watakaotumia huu mfumo mbovu kujiridhisha wao na familia zao.

Mwisho kabisa watanzania tunatakiwa tutambue kwamba hakuna mwanasiasa atabadirisha mfumo kuwa bora bali sisi wananchi ndo tunajukumu la kupaza sauti zetu na kufanya kila tuwezalo kuhakikisha tunapata mfumo ulio bora wa uendeshaji wa hii nchi.
 
Back
Top Bottom