Hatima mabilioni ya Dowans kujulikana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatima mabilioni ya Dowans kujulikana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by joseeY, Sep 28, 2011.

 1. joseeY

  joseeY Senior Member

  #1
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  KITENDAWILI cha iwapo Kampuni ya kufua umeme ya Dowans inastahili kulipwa tuzo ya Sh94 bilioni na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) au la kinatarajiwa kuteguliwa wakati Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itakapotoa uamuzi wake wa kisheria.

  Dowans iliwasilisha maombi katika mahakama hiyo ikiomba tuzo ya kiasi hicho cha fedha dhidi ya Tanesco, baada ya kuamriwa na jopo la majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) ya Paris, Ufaransa Novemba mwaka jana.

  Jopo hilo liliketi chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen akisaidiwa na wasuluhishi Swithin Munyantwali na Jonathan Parke na kutoa uamuzi huo wa kuitaka Tanesco ilipe tuzo hiyo ya mabilioni.

  Vyanzo vya habari kutoka Mahakama Kuu, vilidokeza kwamba uamuzi wa maombi hayo ya usajili wa tuzo hiyo ya Dowans unatarajiwa kutolewa.

  Endapo Mahakama Kuu itakubaliana na maombi ya Dowans, basi tuzo hiyo itasajiliwa na kuipa nguvu ya kisheria kulipwa mabilioni hayo.Hata hivyo, Dowans kwa kujihami, imeshafungua maombi mengine ya utekelezaji wa hukumu hiyo ya ICC katika Mahakama Kuu Uingereza kupitia kwa mwanasheria maarufu nchini
   
 2. R

  Rugemeleza Verified User

  #2
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Habari nilizozipata ni kuwa Dowans wameshinda kesi yao na hivyo Mahakama Kuu imekaza tuzo. Ndivyo nchi yetu inavyoliwa.
   
 3. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hureeee CCM oyeeeeeeeeee! Igunga Oyeeeeeee Rostam Oyeeeeeeeeeeee!!!!!!!!
   
Loading...