Hatarii

KESSY FRANCIS

Member
Nov 9, 2011
42
11
MASHEIKH TUSITUMIE VIBAYA NAFASI ZETU ZA UONGOZI NDANI *YA DINI KUPOTOSHA WAUMINI.
*
Ni ukweli usiopingika kuwa viongozi wa dini duniani kote wamekuwa watu wa kuaminika, kutumainiwa na kujizolea mamlaka ambazo kimsingi hawana, lkn kutokana na wao kujikita zaidi ktk maswala ya kiroho na kimwili. Nchi zingine chache Sana duniani SERIKALI IMEFUNGAMANA NA DINI, kwahiyo viongozi wa dini wanaweza kuwa ndiyo viongozi wa serikali kwa hiyo ni vigumu sana kutenganisha kauli zao sehemu yeyote na wanakuwa na mamlaka za kisheria. lkn TZ SERIKALI YETU AIFUNGAMANI NA DINI YEYOTE ila raia wake na viongozi wake ni waumini wa madhehebu mbalimbali, na swala hili la kutenganisha kati ya dini na serikali ni la kikatiba ( secularism ). Kwahiyo taasisi hizi mbili muhimu zinahitaji kueshimiana na kuwa wavumilivu wa kuvumiliana kwani watanzania ni waumini wa dini mbalimbali na wengine hawana dini kabisa.*

Swala la SENSA duniani kote kwa nchi zinazofungamana na dini na nchi zisizofungamana na dini swala la sensa ni muhimu na hufanywa kwa vipindi tofautitofauti kulingana na *wanavyojipangia nchi husika na inategemea kwa wakati huo ni TAARIFA GANI MUHIMU ZINAHITAJIKA, kwa maendeleo ya taifa hilo, taarifa hizo muhimu ndizo ambazo zitatumika kupanga SERA za nchi, mathalani dawa ziagizwe kwa idadi gani? Shule zijenge wapi na kwa idadi gani? Na kupanga mikakati mingine ya kiusalama, kiuchumi n.k. MWAKA HUU WA SENSA SERIKALI INASEMA HAWATAWEKA KIPENGELE CHA DINI na sababu wakatoa. Lakini ikumbukwe kuwa VITA YA DINI POPOTE PALE ULIMWENGUNI HAIJAWAHI KUISHA kwani serikali inahofia kujitokeza waumini wa dhehebu Fulani kujiona wao ni wengi na hivyo wanahaki kuliko wengine kwa hiyo kuondoa uwezekano wa Hilo kutokea na kuhatarisha amani na utulivu wetu. KAMA DINI ZINAONA WANAHITAJI KUJUA IDADI YA WAUMINI WAO WANA HAKI NA RUHUSA YA KUFANYA HIVYO PINDI WATAKAPO.*

SI LAZIMA KILA KINACHOFANYIKA KWINGINE DUNIANI NA SISI TUIGE.
*watanzania wenzangu natoa RAI kuwa tusijaribu kufanya kitu kwa gharama zetu wenyewe ambacho kinaweza kuhatarisha AMANI, UPENDO, MSHIKAMANO *wetu ambayo ni TUNU tulioachiwa na baba wa taifa hili. TUJITOKEZE KUSHIRIKI KIKAMILIFU KTK ZOEZI MUHIMU LA SENSA KWA KUPANGA MAENDELEO YETU.
 
Mahubiri yako mazuri kama ungekuwa unajua haki, ni bora amani itoweke watu wakajifunza kuwa ubaguzi wa aina yeyote haufai. Kama wakorintho wanaogopa kufa waislam kwetu ibada, wait and see.
 
Tatizo letu tunaongea sana na kuponda lakini suluhisho zero. Hakuna watanzania wenye ujasiri wa kutetea haki zao hadi kufa, wengi ni fuata mkumbo. Likiwaka tunasahau na dini zetu na kujificha katika shimo moja.
 
Back
Top Bottom