Wakati sijakutana na wizi wa hawa vibaka kwa kukata electric wire umeme ulikuwa umekata na generator lilikuwa limekaa muda bila kuwashwa hivyo battery ikawa imekufa. Waliingia kabla hata wale mifugo wangu wa usiku hawajafunguliwa fasta waliondoka na battery za gari kubwa, na vitu kadhaa walivyokutana navyo!!! Mifugo kuanza kuita fasta walishapanda ukuta na kukimbia!!!! Siku nyingine waliingia nyumba ya ndugu yangu alikuwa ndo anaanza maisha wakakomba kila kitu sebuleni, nahisi walimpulizia dawa akalala fofofo!!! Sasa basi hawa watu hawana huruma, wakati mwingine kama wakikuibia na ukawa huna alternative ya kupata mali zingine, basi utajikuta ukiinua jiwe na kuwamaliza maana wakienda polisi, baada ya masaa machache unawaona mtaani. Wananchi wamechoka.