Hatari...!

Hatari...!

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
HII HALI INASIKITISHA SANA
mob-justice.jpg
 
.....KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

Hili swala la kuchukulia sheria mkononi linatisha jamani, hata watu wanashauriwa wakimgonga mtu barabarani ni bora wakimbilie polisi, hata watu wenye nia njema tu hushindwa kusimama kwa kuhofia maisha yao na kuogopa mob justice.
Tabia ya kujichukulia sheria mkononi imekuwa ni tatizo kubwa nchini na ni kinyume na haki za binadamu. Hebu tazama picha hii wananchi wakijichukulia sheria mkononi kwa mtu anayedhaniwa kuwa ni mwizi, Je, mtu
akiamua kumpakazia mtu kumwita mwizi kwa sababu zake binafsi na watu wakachukua hatua kama hii kwa mtu asiyekuwa na hatia?

Je ni jinsi gani tunaweza kukomesha hii tabia?
 
Caught red handed. Ushahidi tosha unaoweza kumtia hatiani huyu jamaa mwenye jiwe na yule mwenzie anaekuja kuleeeeeee........
 
Wakati sijakutana na wizi wa hawa vibaka kwa kukata electric wire umeme ulikuwa umekata na generator lilikuwa limekaa muda bila kuwashwa hivyo battery ikawa imekufa. Waliingia kabla hata wale mifugo wangu wa usiku hawajafunguliwa fasta waliondoka na battery za gari kubwa, na vitu kadhaa walivyokutana navyo!!! Mifugo kuanza kuita fasta walishapanda ukuta na kukimbia!!!! Siku nyingine waliingia nyumba ya ndugu yangu alikuwa ndo anaanza maisha wakakomba kila kitu sebuleni, nahisi walimpulizia dawa akalala fofofo!!! Sasa basi hawa watu hawana huruma, wakati mwingine kama wakikuibia na ukawa huna alternative ya kupata mali zingine, basi utajikuta ukiinua jiwe na kuwamaliza maana wakienda polisi, baada ya masaa machache unawaona mtaani. Wananchi wamechoka.
 
Maamuzi ya namna hii yanakuja wakishauibia ndo utajua n wabaya kiasi gani, waliwahi nipiga lita 100 diesel, betr 2 kubwa na taa zote za trailer wakang'oa, kibaya zaidi sikuwa na wakumshitakia . Nilitamani Livonia shingo ya mtu aisee
 
halafu wale wa pembeni wanashangilia............

ni kama clip moja niliangalia ya yule mwizi wa boda boda
 
Hii ni DHAMBI, hata Mungu hapendi na amekataza tusiue. Hakuna chenye thamani zaidi ya uhai wa binadamu sasa iweje ufurahie kuutoa kwa sababu ya kosa la wizi au mengine? Hata wanaoshangilia hapo wameshiriki kuua damu ya huyo marehemu itakuwa mikononi mwao! Ndio maana kizazi cha leo tuna matatizo mengi na vitu vya ajabu sana, ni laana hii.
 
eeeee bwana eeeee hii noma aise binadamu wasikie tu usiombe yakukute
 
Wakati sijakutana na wizi wa hawa vibaka kwa kukata electric wire umeme ulikuwa umekata na generator lilikuwa limekaa muda bila kuwashwa hivyo battery ikawa imekufa. Waliingia kabla hata wale mifugo wangu wa usiku hawajafunguliwa fasta waliondoka na battery za gari kubwa, na vitu kadhaa walivyokutana navyo!!! Mifugo kuanza kuita fasta walishapanda ukuta na kukimbia!!!! Siku nyingine waliingia nyumba ya ndugu yangu alikuwa ndo anaanza maisha wakakomba kila kitu sebuleni, nahisi walimpulizia dawa akalala fofofo!!! Sasa basi hawa watu hawana huruma, wakati mwingine kama wakikuibia na ukawa huna alternative ya kupata mali zingine, basi utajikuta ukiinua jiwe na kuwamaliza maana wakienda polisi, baada ya masaa machache unawaona mtaani. Wananchi wamechoka.

walimpulizia dawa ipi?
 
Ndugu, Usiukumu ili nawe usije kuhukumiwa!
inawezekana anayehukumiwa naye alihukumu huku akiujua huo msemo na sasa yanamkuta!
Dalili iliyo wazi kuwa pamoja na hii picha kuonyesha nyaya za umeme kwenye background kielelezo cha ustaarabu wa eneo husika lakini bado wakazi husika wanafanya mambo kama miaka 5,000 iliyopita ...yaani wakati wa Moses na Torati! Inasikitisha kwana kwa mtenda na mtendewa.

hii hali inasikitisha sana
mob-justice.jpg

hii ni dhuluma!
Kama unamwamini mungu ; haya ni madhambi makubwa!
Huu ni unyama!
Huu si utu; ni kinyume cha haki za binabamu!
Haijalishi amefanya uovu gani ,tujiepushe na kumwaga damu.
 
Haya majitu mie siyaonii huruma kabisa kwa sababu ndiyo yanayokuwa ya kwanza kujichukulia "sheria" mkononi wakijiaminisha chochote cha mtu ni chao muda wowote! wamewahi kuniliza, ila mbaya zaidi waliwahi kunipiga kisu, bahati tu nilipona! Ni wauaji wakubwa kuliko watu wanavyowadhania! Anayewatetea ni bado tu hawajamtenda!:frusty:
Angalizo: washughulikiwe tu wale ambao tumejiridhisha kuwa ni vibaka na wezi!
 
kujichukulia sheria mkononi ni makosa sawa, lakin kama ushawahi kuibiwa mkuu hawa jamaa wanarudisha nyuma sana na hiyo ndo adhabu yao inayowastahili sana tu.
 
Miongoni mwa hao waliosimama hapo, kuna mwingine unakuta ni mpiga dili kama za huyo anayeondolewa uhai.
 
Sio siri bora wampige tuu. huyp jamaa ajikuwahi alfajili unaenda job lazima akupige panga au nondo. wacha afe wahed.i
 
Back
Top Bottom