Hatari: Zanzibar ni zaidi ya inavyonenwa!

Kwa matokeo yalokwisha tangazwa na ZEC yakaonesha kuwa CUF walikuwa tayari wana majimbo tisa kutoka unguja, ni pathognomonic kuwa washindi, sema tu kuwa hata wakitangazwa kuwa washindi ccm Zanzibar itaanza ku behave kama CUF inavyo behave wakiwa nje ya dola
Potelea mbali , aliyeshinda atangazwe .
 
Hiyo makala ina kiwango cha hali ya juu sana ya uandishi na imezingatia zaidi facts na kujiepusha kuegemea upande mmojawapo kati ya pande 2 zinazohusika zaidi na mgogoro huu ambao ni CCM na CUF.
 
we jamaa ni typist mzuri sana, tumeona ubora wako.
siku nyingine fupisha, toa points tu na sio brabra nyingi

Haya ndio matatizo ya watanzania wengi,UVIVU wa kusoma,ndio maana hata mkiwekewa mikataba "fake",mnashindwa kuigundua.... :)
 
Pamoja na points zako nzuri mkuu, ulisahau jambo moja zuri; Nini kifanyike?? Tuwape points zetu tu, huenda zikawasaidia hao wenye uwezo. Kama wataisoma hii article, nakuhakikishia kuwa watajua kuwa sasa watu si mazuzu ka walivyoamini.
Si nabii ila, Mimi naona giza nene zaidi kwa Muungano huu. Kama umeshikiliwa kwa gundi ya unga wa ngano vile. Ukikauka, na naona ka tiyari ushakauka waweza katika ghafla.
Viongozi, wamekaa kimyaaaa. Hakuna aliyediriki kutoa tamko rasmi kuhusu uchaguzi. Mnavyozidi kukaa kimya ndo mnavyozidi kuchagiza mihemko. Mngejua mngetangaza pale pale kuwa hakuna mshindi. Sijui, ila nawaza tuu.
Atakaye tangazwa leo, baada ya mda mrefu hivi. Awe awaye au iwe iwavyo, si ni uonevu tuu?? Mkisema uchaguzi urudiwe, si mmewaonea CUF kuwa mbona mlikubali ule wa JMT? Mkisema kuwa Maalim ndo mshindi halali, si mtakuwa mmetaka kumwibia ushindi?? Uaminifu wenyu uko wapi??
Nakuunga mkono mkuu, Uchaguzi huu wa Zanziba, ni zaidi ya tunayo yaona au kuyajua na pia tunayo ambiwa. Taifa la ghilibaaaa. JPM ya Ngoswe mwachiye Ngoswe. Aliyelianzisha yuko mbalii anakuangalia utakavyo limaliza
 
Nijuavyo mm hata watanganyika wote waletwe zanzibar kuivamia zanzibar kijeshi haitosaidia kuwaziba mdomo wazanzibar wasidai mamlaka yao yaliyoporwa na wavamizi ya mwaka 1964,haki ya mtu haipote bali mtaichelewesha tu,maamuzi ya wananchi yaheshimiwe.
 
Acha uvivu wa kusoma je ingekua kitabu si ungekitupilia mbali

Angeipeleka kwenye gazeti la Raia Tanzani/Mwema ingekua mahala muafaka kabisa. Ingekua ni JAMES HADLEY CHASE ningesoma na nikamaliza leo hii.
 
Tujifunze kusoma jamani, yaaani hizo page mbili watu tunalalamika.

Tunasoma sana mkuu isipokua looks like jamaa ameona JF ndio sehemu ya kujifunza kuandika makala kabla kuomba kazi Raia Tanzania. Hapa ni mwendo wa summary ili tuhamie kwenye siredi nyengine - sasa kila mmoja akianza kutundika makala tutafika kweli? Mwisho watasababisha ajali barabarani.
 
Kuna watu wana comment huku kwamba uchambuzi huu ni mrefu na mletaji angeufupisha tu bas! Sitaki kupingana nao sana ila naona TATIZO kubwa letu Watz ni kwamba hatupendi/ hatutaki kusoma. Tutaendelea hadi lini kutaka vitu vya shotcut!? Tumesahau kwamba ujuzi mwingi na elimu nyingi iko kwenye maandishi? Namaanisha maandishi haswa na siyo summary tunazozitaka! Jamani embu turudishe hobby ya kusoma maana tunapitwa na elimu nyingi mno iliyofichwa/ hifadhiwa kwenye maandiko.
 
Nimeisoma kwa mda wangu na nimeipenda sana hii mada ya huyu jamaa. Amekomaa sana katika uandishi na pia anajua sana mambo muhimu ya kuzingatia. Mungu wabariki Wazanzibari wamalize yao kwa amani tubaki na muungano mkamilifu na amani ya kudumu. Amina.
 
Duh! Nashukuru sana mkuu, makala yako imeniwezesha niijue Zanzibar na siasa zake kwa undani zaidi. Ujasiri wa viongozi wa serikali ya CCM Zanzibar unahitajika ili kumaliza mgogoro na kuanzisha zanzibar mpya.
 
Back
Top Bottom