Hatari ya TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatari ya TANESCO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 29, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Nimeguswa sana na alalysis ya Haule' kwa kweli nashindwa kuelewa kuwa what should be the end in mind then?!?

  Nikiwaangalia wenzetu ambapo nimepata kutembelea sehemu mbali mbali hadi za vijiji vya wamarekani, kwa kweli nakiri kuwa TEKNOLOJIA RAHISI INAHITAJI WATU WALIO MAKINI. Kila kitu kimepangika kikiangalia usalama wa maisha ya watu wao. Utashangaa nilipata bahati ya kutembelea mkulima mkubwa kabisa jimbo la Iowa, eneo la Atlantic jana, huwezi amini hadi mitaro ya kupitisha maji machafu, yeye kama yeye anakuwa responsible kuweka mashine all along mitaro kunyonya maji machafu ili kucontrol harufu mbaya. Achana na mitaro ya chini ya ardhi ambayo inapitisha maji yanayotiririka mashambani yanakwenda hadi kwenye mabwawa ambayo yako recycled back mashabani ili mbolea isipotee.

  Sielewi ni kutojali, kutoelewa umuhimu, ama negligence kwani I'm sure hata makampuni yenyewe yangelazimishwa kuhakikisha yanachukua hatua za makusudi za kuhakikisha usalama wa watu zaidi ya assumptions za kuwa cables ziko juu lakini je zikianguka itakuwaje!!!

  Jambo la msingi sana sana ni kuwa je haya mazungumzo very sensitive na ushauri wa bure kama huu watendaji na waamuzi unawafikia. Ningetoa wito kwa JF kuwa na sessions za ku - classify some very alarming matters zikawekwa kwenye table on face to face meetings ili kuangalia the best alternative ways ya kubadilisha mambo. Nisingeona wise mambo yanayozungumzwa kwenye mtandao wetuyanaishia kusugua vichwa tu I think it's high time tunawezaku - imput masuala mbalimbali na alternative solutions na kufanya follow - ups.

  Mambo mengine ni ya kufanywa na community zetu bila serikali kulazimika kufanya yenyewe. Mfano nilipata kusifia serikali yao mbele ya mama mmoja mstaafu mjini Ames kuwa serikali yao itakuwa imewafanyia makubwa sana hadi hizi barabara ndogo ndogo za kati ya nyumba na nyumba na za kuingia kwenye recreational parks akasema no, serikali iko responsible kwenye barabara kubwa tu hizi za kati ya nyumba na nyumba na za kuingia kwenye mabustaninyetu ziko managed na vyama vya wanacommunity wenyewe na si serikali kuu.

  Waungwana,
  Nimesikia Masudi akiwaasa wamachinga eneo la ubungo ni hatari kwa maisha yao. Anasema hao wafanya biashara wapo hatarini endapo mitambo ya TANESCO ikilipuka inawezapoteza maisha yao.

  Sioni kama alicho sema ni uongo bali naona ni uonezi au upendeleo usio wa lazima.
  Eneo la ubungo ni hatari zaidi siku hizi sio tu kwa milipuko bali kwa wale wenye BP ile mitambo inavyo cheua tu nihatari kubwa.
  Najaribu kuangalia utashi wa Selikali kwa hili. Selikali ikijua fika pale ni hatari ikaamua kujenga stendi ya daladala pale ambapo daladala za kwenda kilakona ya jiji waipata. hii sio hatari ingawaje inakusanya watuwengi katika maeneo hatarishi???

  Kana kwamba haitoshi, mwaka 2000 kama sikosei ikaamua kuhamishia stendi ya magari yaendayo mikoani Ubungo nakuongeza mkusanyiko huu wale wenyeji wa dar si munakumbukamiaka michache kabla maeneo yale yalikuwa na mashamba ya mpunga na minazi hata kituo kilikuwa kinajulikana kama minazini.
  Mwakumbuka ajali ya moto ambapo mataki ya mafuta ya ndege yalilipuka 2002? fikiria ule mlipuko ungetokea asubuhi ingekuwaje? fikiria yule aliyejitosa kwenda kufunga koki ya mafuta angependelea maisha yake zaidi ubungo ingekuwaje? je tusingekuwa tunaongelea ajali kama ya MV bukoba?

  Sasa tumeongeza mitambo yagesi eneo hilo amabalo sasa limeongeza watu zaidi. tena mitambo ya Agreco, richimundi nayo imewekwa hapo kuongeza hatari hii kwa wale wanao pita kuelekea sehemu nyingine za jiji au kutoka mikoani na au wale wanaotafuta usafiri ktk maeneo hayo achilia mbali wale wanao kuja kupata huduma Tanesco, maji au ubungo plaza na makaziya jirani. maziwa waliahidiwa kuhamishwa tangu 2004 hadi leo imebaki stori
  TEKNOLOJIA RAHISI INAHITAJI WATU WALIO MAKINI.  HAULLE, Evaristo
  I cant teach you violence because I dont know, I can only teach you not to bow your heads before any one, even at the cost of your life - Gandhi  Long live JF
  Mpinga J J - USA

  haulledict <haulledict@yahoo. co.uk>

   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Nami naungana kwa kutoa taarifa sawa ila hatua gani zichukuliwe na serikali, sasa kwa kuwa imesiaha onekana pale sio sehemu nzuri kuna hatari basi dawa ni kuweka doria ya polisi na kuhakikisha watu wanakitumia kituo hicho kwa safari tuu na si biashara ndogo ndogo,

  Wakati mwingine siilaumu serikali, maana wakati wanapanga kuweka TANESCO hapo huenda jiji lilikuwa na watu kama Milioni 1.2 hivi (nahisi), kwa sasa tunakadiria kuwa wakazi wa DAR ni Milioni 4.5. hata tano kama sikosei,

  Ukiangalia pale jirani na TANESCO kunastand ya daladala na standi kuu ya mabasi yakwenda nje na ndani ya Tanzania, hakika ukitaka kwenda mkoani uanzie UBungo jirani na TANESCO! ukitaka kwenda katikati ya mji Ubungo ni mahali pa kuanzia je ikitokea milipuko!!!! itakuwaje?,

  Juzi bwana nilikuwa pale jirani na TANESCO namsubiri jamaa yangu, ghafla mtambo wa gesi ukapumua ilikuwa balaa, binafsi ilibidi nihame mara mmoja! je wale wanafanyia biashara pale kila jioni wanajisikiaje ama ndo wameishazoea?

  Jamani taadhari hii ipewe kipaumbele na kutoa katazo kali tusisubiri maafa yatokea, Kinga ni bora kuliko tiba
   
 3. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,018
  Trophy Points: 280
  Serikali bado ina jukumu la kuhakikisha usalama wa wananchi wale kwa kutafuta mbinu mbaadala. Si nilishawakusikia kuwa wananchi wale watahamishwa, imekuwaje au mpaka waungue kama 100 hivi ndio serikali itaamka
   
Loading...