Hatari Ya Kupuuza Mafundisho Na Maarifa Sahihi

Hatari Ya Kupuuza Mafundisho Na Maarifa Sahihi

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,118
Reaction score
1,565
Mit 19:27 SUV
[27] Mwanangu, acha kusikia mafundisho, Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa.

Mtu akitaka kuwa bora kwenye maisha yake, kazi yake, utumishi wake, biashara yake, na kwenye familia yake, anapaswa kupata mafundisho sahihi ya kumsaidia kusimama vyema katika nafasi yake.

Mtu asiye na maarifa juu ya kile anafanya, anaweza akafanya vibaya, au anaweza asifanye katika viwango vinavyotakiwa.

Rahisi sana mtu kukosea na asijue kama anakosea kwa kukosa kwake maarifa sahihi juu ya hilo jambo analolifanya, hii inaweza isiwe na matokeo mazuri katika utendaji wake.

Mtu asipopenda kujifunza, mtu huyo amekataa kuwa bora katika kile anafanya, atafanya ila sio kwa viwango vinavyotakiwa.

Maarifa yanayaweza kutokana na neno la Mungu, mtu akiwa na maarifa ya neno la Mungu atakuwa salama katika maisha yake, hasa asipopuuza maarifa hayo.

Mtu akikataa kusikiliza mafundisho sahihi, amekaa kuwa na maarifa sahihi ya kumsaidia katika maisha yake, na amekataa kuwa na hekima ya ki-Mungu katika maisha yake.

Tunapaswa kujiuliza, tunapenda kujifunza tuelimike? Au tunapenda tuwe na maarifa ya kubishana na watu, kama lengo ni hilo tujue hatutafaidika sana katika maisha yetu.

Tunaweza tukajua sana maandiko kwa kuyakariri, ila tukawa tunaishi kinyume na neno la Mungu, ila mtu anayejifunza na kuliweka moyoni neno na kwenye matendo, mtu huyo atafaidika na neno sana.

Tuwe na moyo wa kupokea mafundisho sahihi kwa unyenyekevu mkubwa, na tuwe na bidii ya kutafuta maarifa sahihi kwa nia njema ili kutusaidia katika maisha yetu.

Mtu akipuuza maarifa sahihi na akayaasi maarifa ya ki-Mungu, ajue amejitenga na hekima ya Mungu, jambo hili lina athari kubwa sana katika maisha yake ya wokovu au ya kawaida.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom