Hatari Vituo mabasi ya mwendo kasi

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
16,841
25,340
Nimesikitishwa sana na ajali iliosababisha kituo cha mabasi cha mwendo kasi cha Baruti maeneo ya Kimara kuharibiwa vibaya,nililiona hili muda mrefu lakini nikajua labda hawa watu wa Strabag watakuja kulirekebisha lakini hawakulifanyia kazi na hatimaye ajali zimeanza kutokea.Vituo ambavyo viko kwenye hatari hiyo ni Korogwe,Bucha,Baruti,Kona,Rombo na Ubungo,vituo hivi havikujengewa ukuta unaotenganisha barabara ya magari ya kawaida na barabara ya mabasi yaendayo kasi,ule ukuta unaanza baada ya kupita kituo kitu ambacho kinasababisha magari hayo yote kukutana na uwezekano wa kuotokea ajali ni mkubwa sana.Naomba wahusika kulitupia jicho hili na kulifanyia kazi mapema
 
Back
Top Bottom