Hatari: Nimenusurika kifo

 
pole sana mkuu, ila hilo jina lako linashabiiana na yalokutkea
 

pole sana chipa
 

Pole sana Ndugu

Huu ujinga ulibatizwa jina la kizaramo Mob Justice unadhihirisha ni jinsi gani nchi zetu za kiafrika zilivyo na uongozi dhaifu na hazifuati sheria za nchi kiasi wananchi wanashindwa kuziamini mamlaka na kuanza kujichukulia sheria mkononi.

Mie nimewahi kuibiwa i know how it pain, ila sishabikii, sipendi, na siwezi kukuta mwizi anapigwa nikajumuika kumpiga na kumtoa uhai, Japo police wanashabikia kwani ukitoa taarifa wanakuuliza wanampiga kwani ameshakufa?

Naomba tubadilike ili kuepusha kuuwa ndugu zetu wasio na hatia kwa kisingizio cha mwizi, ilihali katika wale wote wanaompiga hakuna hata mmoja anaweza kudhibitisha kwamba anayepigwa amemuibia.
 
Am really sorry for the Man, bcoz he has got embarrased with his wife but at the other point, amejua ukweli pia.

Acha mkuu inaumiza sana ila damu isiyo na hatia lazima Mungu ailipie jamaa mpanga njama naskia amekuwa kama chizi ivi....!
 
POLE SANA
ila Marehemu alitakiwa awaambie wale wanaompiga kuwa mbaya wake ni fulani na ANAMDAI HELA YA MAUZO YA NYAMA
naona Wasamaria wema wangemuelewa.
Lakini mara zote Marehemu huwa ana makosa
Haya mambo yapo
(Kuna jamaa mmoja yangu Ismail Kyarumbika R.I.P.alifanyiwa hivyo huko Mombasa alipoenda kumdai kinguvu mdaiwa wake)
 
POLE SANA
ila Marehemu alitakiwa awaambie wale wanaompiga kuwa mbaya wake ni fulani na ANAMDAI HELA YA MAUZO YA NYAMA
naona Wasamaria wema wangemuelewa.
Lakini mara zote Marehemu huwa ana makosa

Kaka usiongee kama ujui matukio ya kumkamata jambazi huwa hana nafasi ya kujitetea kweny snerio kana hiyo ingawa yeye ikuwa jambazi fake!

Unajua kwa mjibu wa sura ya tukio maeneo hayi kulikuwepo na tukio la ujambazi, mpaka leo watu wengi wanaamini walimuua jambazi hakuna ata mtu aliyefuatilia mama yake mzee sana. Mke wake ndiyo hawa wasichana wetu wa mjini kuona jamaa kafa kaamua kurudi alikotoka make ata kwao na jamaa apajui.

Ni shida sana.
 

Mbaya Sana hii!! Rushwa iliyokithiri kwenye mamlaka za serikali esp Polisi ndo imetufikisha hapa!

IMANI IMETOWEKA.
 

Mnyenz nausubiria kesho mkasa wenyewe naomba na picha uweke za makovu...... alafu kama ulikuwa na mpenzi wakati huo alisemaje? je ndugu jamaa na marafiki walisemaje? asante na wewe pia
 
Pole sana Mkuu ila Mwizi hana alama alafu siku hizi wezi wanavaa smart sana ni ngumu kuwatambua.
 
Poleni sana sana,ilinitokea Kunduchi mwaka 2005,tupo bar flani hivi watu wengi kwelikweli tunaangalia mpira,ile niweke mguu vizuri jamamaa akaniitia mwizi kwamba nataka kumchomolea simu,acha bwana watu wakaanza kupanic,nilichofanya ni kutoa fungu nililokuwa nalo mfukoni pamoja na simu yangu,nikamuonesha jamaa na kuanza kumkolomea.Wananchi walinielewa hawakunigusa.
 
Dah.Ni hatar sana sana.Ni hivi TZ huwa kuna hili kundi linalojulikana kama 'WANANCHI WENYE HASIRA ' inabidi kushukuru kwa kutoka salama . Hili kundi mainly huwa ni watu wenye hasira na maisha magumu ingawa ndo waliochagua chama tawala na stress nyingine.Hasira zao huwa wanazitolea popote pale penye kaloop hole ingawa kwenye ballot za uchaguzi huwa hawazitolei huko
 
Pole sana mkuu,nadhani kuna haja ya wananchi kuyachunguza kwanza matukio ya kuchukua sheria mkononi kabla ya kuchukua hatua ili kunusuru maisha ya watu wasio na hatia...
 
Ni Hatari kuchukua sheria mkokoni.

BR,
~Amalinze The Cat.
 
Mimi ilinitokea nilikua safar kibiashara eneo nilipokua jirani kulikua na duka nikaenda kununua vocha tukakutana na mama momoja mm mfukoni nilikua na sh. 9000 nikatoa sh 2000 nikanunua vocha ya buku ile chenj alionipa nikachanganya na zile nyingine ikabak elf nane.

Sasa yule mama nae sijui ni kitu gan alinunua akawa anadai chenj yake mwenye duka ambayo ni sh elfu nane mwenye duka akasema we mama bado ujatoa pesa akakataa akasema umetoa akamwambia mwenye duka umetoa ila huyu kaka amechukua, mwenye duka akatoka nje nakuanza kuniambia toa pesa kabla sijakuchinja nikasachiwa huku nimekunjwa ikakutwa hiyo elfu 8 akasema pesa hii apa mwizi mkubwa nikapigwa makof shat langu likachanika nikaomba msamaa wakaniachia nikaondoka iliniuma sana baada ya siku3 ilikuandio safar nikapita pale kununua maji nikamkuta yule jamaa akaniambia samahan ulipondoka yule mama aliiona pesa yake kwenye sidiria amekutafuta sana akuombe msamaa nikamwambia we ndio ulie nipiga chukua wewe.

Kweli sio wote wanauwawa wameiba tuwe makin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…