Shagiguku
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 409
- 138
Ndugu zangu great thinkers,
Watanzania tumekuwa na tabia ya kulalamika sana linapokuja suala la kuchangia gharama mbali mbali za mambo yanayohusu "maendeleo" yetu kama watanzania.
Nitatoa hapa baadhi ya mifano ambayo tumekuwa tukiilalamikia.
1: Gharama za matibabu hospitalini
2: Gharama za elimu shuleni
3: Gharama za maji mijini na vijijini
4: Gharama za umeme mijini na vijijini
5: Gharama za kuzoa uchafu mitaani kwetu
6: Gharama za............................!
Hapa ukiangalia kuhusu gharama zote hizi utagundua kwamba zote ni za muhimu kwa "maendeleo" ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Na kuzikwepa ni vigumu sana.
Utakuta mzazi kaletewa barua na mtoto wake ya kuitwa kwenye kikao shuleni lakini haendi shuleni kwaajili ya kuweka mambo sawa, kesho akisikia kwamba wazazi wamekubaliana kuanzisha mchango wa madawati anaanza kulalamika.
Mwenyekiti wa kijiji/mtaa akiitisha mkutano wa hadhara, utakuta baadhi ya wanakijiji/mtaa hawahudhurii katka mikutano hiyo, na maazimio yanapopitishwa utakuta hao hao wasiofika ndo walalamikaji wakubwa.
Sasa kwa upande wangu ninakuja na wazo moja la namna ya kuchangia hii michango inayotuhusu na haswa ya elimu.
Ningependa tuyatumie makampuni ya simu, vituo vya mafuta na migodi tuliyonayo kutuwezesha kuchangia michango mbali mbali pasipo kubughuziana na mialiko ya mara kwa mara shuleni ama kijijini/mtaani.
Na hapa ninafahamu kuna watumiaji wa simu za mkononi Tanzania zaidi ya 25,666,455 kwa mujibu wa takwimu za 2011 zilizotolewa International Telecommunication Union, 2012. Na sasa kwa idadi hiyo ya watumiaji wa simu za mkomnoni tunaweza kujiwekea mkakati maalumu wa kuanza kuchangia "maendeleo" yetu tukianza kwa mfano na elimu, kwamba tunaanza kuchangia elimu kwa kanda ya ziwa viktoria kwa kulimaliza kabisa tatizo la madawati kwa shule zote za msingi na sekondari. Kisha tunageukia kwenye tatizo la vitabu, kisha kwenye tatizo la madarasa, maktaba na maabara nk nk nk.
Katika kuchangia michango hii, tunaweza kuruhusu wenye makampuni kuweka matangazo yao (alama za utambulisho wa kampuni husika) ili kuyafanya yaongeze kasi ya kusaidia kukusanya hiyo michango yetu.
Na namna ya kuikusanya sasa hiyo michango ni kwa kutukata Tsh. 100/= tu kwa wiki kwa kipindi cha miezi labda 6 ambapo ukifanya hesabu za haraka haraka kwa kuchukua watumiaji wa simu za mikononi milioni 25 tu, hesabu yetu itakuwa nyepesi kama ifuatavyo (ombi kwa TRA wasiikate kodi hii michango)
Tsh. 100 x 25,000,000 = 2,500,000,000/= kwa wiki moja
Tsh. 2,500,000,000/= X wiki 4 = 10,000,000,000/= kwa mwezi mmoja
Tsh. 10,000,000,000/= X miezi 6 = 60,000,000,000/=
Kwa hesabu hiyo nyepesi tunakuwa tumefanya jambo kwenye madawati. Baadaye tunaingia kwenye maeneo mengine pia.
Angalizo tu: ili kuleta ufanisi wa zoezi zima la ukusanyaji wa fedha hizi ningependekeza kuwa idara na watu wote wa serikali wasihusike, wao wasubirie tu kuja kukabidhiwa hivyo vifaa basi, maana uzoefu unaonesha kwamba wamekuwa walaji wakubwa wa michango ya wananchi, kuanzia ngazi ya wizara hadi mtaa/kijiji. Hivo itakuwa vizuri kama inaundwa tume maalumu ama makampuni yenyewe yakahusika pia katika kuchongesha hayo madawati, kununua vitabu, kujenga majengo nk,nk.
Na kama kuna mwananzengo (mwananchi) mwingine anaweza kuwa na mawazo mazuri zaidi ya kuboresha uchangiaji wa "maendeleo" yetu katika maeneo ya elimu, afya, maji, nishati nk, basi ningemuomba achangie hapa ili kuboresha zaidi wazo langu hili. Kwa maana ninauhakika humu kuna watu makini sana na wengine ni viongozi wa serikali na vyama vya siasa. Ninafahamu kwamba watu kama nnape nnauye, zitto kabwe, januari makamba, john mnyika, prof tibaijuka, deo filikunjombe, moses machari (rafiki yangu huyu tulisoma pamoja), wenje (pia rafiki yangu huyu tulisoma pamoja), nk, nk, nk. watakuwa wanasoma thread hii kwa muda huu, na kwa sababu wao wapo katika ngazi fulani fulani za maamuzi ningependa pia walichukue hili na kulifikisha mahala ambapo wao wanaona linaweza kufanyiwa kazi ipasavyo.
Tukumbuke kuwa wananzengo unapowaita na kuanza kuwachangisha labda tuseme Tsh. 10,000/= ya madawati huwa wagumu sana kuchangia, lakini ukiwakata ka - shilingi mia kao mara moja kwa wiki hawaataona kuwa wamechangia pakubwa. Lakini pia hii itasaidia na kuwezesha hata wanafunzi, wafanyabiashara, wafanyakazi, wakulima, wafanyakazi wa ndani, wapiga debe stendi, makonda, nk, nk, nk kuweza kuchangia.
Vivyo hivyo michango tunaiendeleza katika vituo vya mafuta, migodi nk ambako tunaona tunaweza kukusanya fedha kwaajili ya "maendeleo" ya wataanzania. Tusisubiri serikali itufanyie, hapo hatutafika tutabaki kuwa watu wa kulalamika kila siku kuwa serikali haifanyi lolote (najua na kufahamu kuwa pengine huu ni wajibu wa serikali). Lakini je, wewe umeifanyia nini Tanzania????? Basi ninaamini kwamba kwa hicho kidogo utakachoifanyia basi historia itakuweka katika kumbukumbu zake kuwa uliwahi kuifanyia kitu Tanzania.
Tuepuke kuwa watu wa kulalamika, tufanye kile kidogo tunachoweza kukifanya maana ninaamini kwamba tunaweza kabisa kufanya kama tutakuwa na utashi. (Najua kuna watu walishaanza kuilalamikia hata hii thread kwa kusema kwamba labda ni ndefu mno, au hili haliwahusu wao ni la serikali nk, nk.)
Karibuni kwa kuboresha wazo hili.
Napenda kuwasilisha.
Nakala kwa:
1: Watanzania wote - Tutimize wajibu wetu kwa taifa letu kwa manufaa yetu na vizazi vyetu vijavyo.
2: Viongozi wote mliomo humu jf - tunaweza uongozi wenu waweza kuanza kuonekana hapa kupitia hili wazo dogo
3: Great thinkers wote - kwa kuchangia ktk kuboresha.