El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 263
- 502
Kuna namna ambayo hata kama Sina chuki na mtu, hainizuii kutoa dukuduku lililo moyoni mwangu juu ya mtu huyo.
Binafsi, Leo sijafurahi kabisa kusikia mwamba huyu anarudi kwenye ulingo wa siasa akiwa na nafasi ya uenezi kwenye chama kinachotawala nchi.
Matendo na vituko vya Makonda havijawahi kunifanya kuwa sehemu ya wale wanaomuunga mkono. Mimi huwa sivutiwi kabisa na tabia ya huyu jamaa mbele ya watu( kumbuka Sina shida na udhaifu wake mwingine anaoweza kuwa nao ambayo hautugusi sisi jamii) hivyo shida yangu kwake sio personal.
Nikija Sasa kwenye uchambuzi wa mada yangu, Namuona Makonda kwenye nafasi hii kuwa irrelevant. Mwenezi wa chama kwa lugha rahisi ni mwenezaji wa chama kwa jamii( wananchi) tujiulize
1) Tabia ya Makonda mbele ya jamii ni uenezi ( publicity) inayofaa?
Kumbuka unapofanya biashara yoyote watu huanza kukununua wewe kabla ya bidhaa unayoiuza.
People buy you first before they buy what you sell. Tujiulize, kwa tabia alokuwa nayo Makonda ananunulika? Is he buyable?
Kazi ya uenezi wa chama na itikadi yake naona inakuwa ngumu na labda kuchangia kuporomosha chama maana haiba ya huyu ndg kwa jamii haivutii. Kujiamini kuliko pitiliza, ulevi wa madaraka na kutojali ndo picha jamii iliyonayo juu ya ndugu huyu, cjui kama wateuzi wake hawakuliona hili
2) Kama unajua kusoma tabia za watu, Makonda ni mtu mgumu ( rigid). Lugha yake imejaa mamlaka zaidi kuliko utetezi. Hana lugha ya kujishusha. Kwangu Mimi alifaa hata kama ni kumtafutia nafasi basi hata katibu mkuu wa wizara. Huyu bwana ni burecratic Hana asili za udiplomasia kabisa.
Kazi ya kueneza chama unapaswa kuwa na lugha laini ya mwananchi, lugha ya kushawishi, na lugha ya kujishusha mbele ya wale unaotaka kuwavuta. Sioni Makonda akiwa na tone hii. Ebu msikie tu hata tone yake anapoongea. Ni makaripio na maagizo hata pasipo penyewe.
Makonda bado hajawa na uchama wa kuwa msemaji wa chama tawala. Katokea uvccm. Waone uvccm wanafanya siasa gani. Si za ushawishi Bali nguvu na hata ugomvi. Wasikie wanavyotamba mtaani, " atayechezea CCM atatuona." Naogopa katibu mwenezi aliyejaa mamlaka tu na Hana lugha ya ushawishi kama atakisaidia chama.
3 ) Huyu bwana ndo atakuwa msemaji wa chama, mwelekeo wa Rais ni siasa za maridhiano, je huyu mwenezi ni mtu wa haiba hiyo ya ku engage watu kwenye maridhiano?
Natabiri siasa Kali na misimamo mikali hapa mbele katika siasa za Tanzania. Namuona mtu ambaye hawezi kabisa kuwa friendly labda mahali hapo awe amekutawala tu.
Mwenezi mwenye misimamo mikali na ukada uliopitiliza ( fanatism) atakifanya chama kiwe na maelewano na vyama vingine inapobidi?
4) sijajua kama huwa tunajua maana ya kuwa na uwezo wa kuongea na kumudu lugha. ( verbal intelligence)
Verbal intelligence imewafanya watu wengi huko duniani kupata maendeleo makubwa.
Je mwenezi huyu ana verbal intelligence? Kazi yake inahusisha kuongea, je anaweza kuongea vizuri?
Kuongea vizuri siyo tu kutoa sauti lazima uwe na substances katika usemaji wako. Does he talk substantively so to speak? Na je anaimudu lugha?
Huyu bwana ni msukuma mwenzangu, hata bila kusema mengi lugha yake ni ngumu haichambuki kirahisi. Huongea mambo rahisi tu lakini katika hali ngumu kama vile ni mafumbo. Atavutia kweli kwa hii namna anavyoongea? ( verbal intelligence)?
Namalizia kwa kusema Tena" mie ni mtu mwema na huwa Sina vita na watu, Shida yangu Niko so principled.
Nisema uteuzi wa halmashauri kuu ya CcM juu ya Makonda haujanivutia hakika. He is so irrelevant for the job.