Hashim Rungwe Spunda yuko ITV sasa hivi

Hashim Rungwe Spunda yuko ITV sasa hivi

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,345
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chaumma, Hashim Rungwe Spunda yuko kwenye kipindi maalum ITV. Akinadi sera zake, wananchi kadhaa wamehojiwa na kuonesha kuwa wana imani naye, hasa maeneo ya Kigoma ambako ni kwao!

Chaumma hoyeee!
 
unajua huyu mzee kanipa shida kichwani sikuwaza kumjua sana kwani sio vile kama ninavyoona na kufikiri na kufahamu ila nilikuwa anjiuliza sana kwa nn anaamua kusimama yeye kama yeye? juzi nimejua kwa nini............kumbe wa kwetu.......wale wale........wao wanaweza zaidi
 
Huyu huwa kama komedian,kila kitu anagombea na hashindi
 
Rungwe anagombania urais lakini ni dhahiri hatopata ata 1% ya kura.
Je kuna faida gani kutumia pesa kufanya kampeni wakati ushindi ni ndoto?
 
Tuna taka dunia ijue kwamba Tz ni ya wote na yeyote mwenye sifa anaweza kuchaguliwa kuwa rais na sio kama wanavyo dhani baadhi ya watu kuwa nchi hii ni yao na chama chao eti bila wao hakuna Tz
 
Rungwe anagombania urais lakini ni dhahiri hatopata ata 1% ya kura.
Je kuna faida gani kutumia pesa kufanya kampeni wakati ushindi ni ndoto?
Wanapiga ruzuku ndefu asikwambie mtu ndo mana ata ACT wamesimamisha
 
ITV mi penda sana nyie hata hambagui..naomba spencer lameck ufikishe hilo wazo kama inawezekana kurusha kipind cha bbc swahil mkirushe tu..tuondoke kbs star tv
 
Huyu huwa kama komedian,kila kitu anagombea na hashindi

Kumbe ukishindwa unakuwa komedian, basi UKAWA kumejaa makomedian maana tangu 95 wanaangukia pua, kila mmoja kwa nafasi yake.
 
Wanapiga ruzuku ndefu asikwambie mtu ndo mana ata ACT wamesimamisha

Ruzuku? Ruzuku hutolewa kwa vyama vilivyopata asilimia 5 ya kura za Urais mzee.
 
Rungwe namkubali sana ni mpenda mabadiliko ya kweli. Hana urafiki na mafisadi yaliyojazana ukawa bado wiki moja tu ataanza kumnadi magufuri.

Kataa mafisadi kwa nguvu zote , kura yangu ni kwa Magufuri.
 
Back
Top Bottom