Hashim Rungwe apinga kurudiwa uchaguzi Zanzibar

wembeee

JF-Expert Member
Jan 16, 2015
2,708
1,353
Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMA kimesema kuwa hakikubaliani na mazungumzo yoyote ya kutafuta suluhu ya uchaguzi wa Zanzibar.

Mwenyekiti wa chama hicho Hashim Rungwe amesema mazungumzo hayo hayakushirikisha wagombea kutoka vyama vingine na hivyo chama hicho hakiyatambui na pikia hakikubaliani na suala la kurudiwa kwa uchaguzi visiwani.

Rungwe pia amekemea na kulaani vitendo vya kibaguzi vilivyooneshwa katika sherehe za Mapinduzi Zanzibar siku ya tarehe 12, Januari.
 
Huyu mzee anafanya siasa safi.Na si mnafiki.Rungwe ni mzalendo wa kweli.si Zitto anajifanya mzalendo kumbe ni kaburu mweusi
 
hv kwann akisema zitto ni MNAFIKI, ila akisema rungwe spunda mnamwita MZALENDO?
 
hv kwann akisema zitto ni MNAFIKI, ila akisema rungwe spunda mnamwita MZALENDO?
Mimi akisema zito simuiti mnafiki na wala simuiti mzalendo.

Akisema Rungwe ninamuita mzalendo.

Akisema Slaa, Ni mzalendo.

Mbowe Ni msaliti.
 
Huyu mzee anafanya siasa safi.Na si mnafiki.Rungwe ni mzalendo wa kweli.si Zitto anajifanya mzalendo kumbe ni kaburu mweusi

Ayoutollah Zito Jamani anatangaza kampuni, aah sorry chama chake. Sasa asiposhiriki aims, visions zake hazitafikiwa,ie, uenyekiti WA PAC etc, etc, etc, etc!
 
Kwa kuwa ufutaji wa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar haukufanywa na ZEC bali ulifanywa na a single person anayeitwa Jecha, kwa maana hiyoulikiuka waziwazi Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na sheria za uchaguzi Zanzibar,.

Kwa hiyo kwa mazingira yoyote uamuzi wa kuurudia uchaguzi huo nao utakuwa ni uamuzi haramu.

Kwa hiyo solution pekee ya mkwamo huo wa kisiasa wa huko Zanzibar ni wa aina moja tu, ambao ni kukamilisha kumtangaza mshindi wa kiti cha Urais kwa uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015, uchaguzi ambao ulithibitishwa na waangalizi wote wa ndani na nje ya nchi kuwa ulikuwa huru na wa haki.
 
Huyu mzee anafanya siasa safi.Na si mnafiki.Rungwe ni mzalendo wa kweli.si Zitto anajifanya mzalendo kumbe ni kaburu mweusi
acha unafki kama unamkubali anafanya siasa safi mbona hukumpa kura? Wala hukujaribu hata kumpigia kampen kwenye mitandao
 
Back
Top Bottom