Hasara kwenye mfumo wa elimu

Hasara kwenye mfumo wa elimu

Diwani

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2014
Posts
2,824
Reaction score
3,021
Amani iwe nanyi,

Kwanza kabisa ningependa kufafanua neno "Hasara" kwenye Kichwa cha uzi huu. Ikiwa 'Moderators' haitawapendeza basi, maamuzi yenu yataridhiwa. Hakukuwa na haja ya kuweka 'Upungufu', ama 'Changamoto' ama 'Matatizo', kwa maana kwa Uzito wa maana yenyewe halisi iliyonigusa kuandika uzi huu itapimwa kwa kiwango cha 'hasara'.

'Hasara' ambayo kimsingi ni Upotevu wa mtaji ama rasilimali iliyowekwa kwa ajili ya uzalishaji wa Mali ama Amali fulani ndilo jambo nililoliona katika mfumo wa Elimu wa nchi nyingi za Afrika, Mathalani Tanzania.

Licha ya uwepo wa Shule nyingi sana na jitihada lukuki za Serikali (JMT) ya kukuza kiwango cha Elimu kwa watu wake, lakini kuna upotevu mkubwa sana wa rasilimali unafanyika.

Rasilimali zipi?
Pesa, Muda, Nguvukazi, na mbaya zaidi kuna upetevu wa rasilimali UJUZI ASILI (Kipaji) ama Rasilimali "Uwezo wa kuzalisha" kama navyoweza kuita.

Hakuna mtu, ama Familia duniani, ambayo Uchumi wake unamea bila Uzalishaji Mali ama huduma. Hakuna. Mtu ni Familia, na familia ni koo, kisha kuwa "Taifa", hivyo basi Msingi wa Taifa ni Mtu Mmoja (Individual); lengo langu si kutetea ama kulinda hoja za 'Kibepari' ama Falsafa za Mabwana wakuu (Master Philosophy) lengo langu ni kuweka sawa, Uhusiano wenye tija kati ya mtu binafsi na Mfumo wa Elimu wa jamii ambayo mtu huyo anaishi.

Mfumo wa Elimu, mathalan Tanzania ni mfumo tulio rithishwa na Waliowahi kuwa Watawala wetu, Wajerumani baadae, Waingereza, Je kabla yao, mfumo wa Elimu ulikuwaje?

Ikumbukwe kuwa, "The role of Education must be determined by its Purpose to the people" Elimu ya Kabla ya Ukoloni na baada ya Ukoloni zilikuwa Purpose (Malengo) gani?

Kwa Kuelewa tu maana ya Ukoloni, mbali na uvamizi wa kisiasa ambao hufanywa na nchi moja dola imara, kwa nchi nyingine dola dhaifu, ukoloni pia unahusisha uvamizi wa kitamaduni na lengo kuu la jamii husika. Ikiwa tumerithi muundo, basi tumerithi pia 'goal' hata kama maudhui ni tofauti. Lengo la Elimu kabla ya ukoloni ilikuwa ni kujenga jamii 'Productive' na hivyo ndivyo mtu alikula na kukuza uchumi wa nyumbani kwake, ilikuwa ni lazima uzalishe, kama si kweli, basi Wakoloni wasinge hangaika kuanzisha Uchumi wao kwenye Makoloni kwa kuharibu mfumo wa Uzalishaji wa Waafrika (Destructive methods) ikiwamo kuharibu viwanda vya mikono, biashara na hata kufukuza Waafrika kwenye maeneo yao ya makazi na uzalishaji.

Lengo la Elimu yao lilikuwa ni nini?
Lengo ni kujenga Muundo wa Master to Servant (Servi in latin means 'slave'). Mmoja amtawale Mwingine kwenye nyanja zote; Kijamii, Kisiasa na Kiuchumi. Waafrika walielimishwa kwa malengo makuu mawili; Wawe WATUMISHI na pia wawe SOKO.

Tukarithi mfumo huu wa kuunda WATUMISHI na SOKO, ule utamaduni wa kutumia mikono yetu kuzalisha (Handicraft Industry) ukafifishwa na Elimu iliyozalisha Watumishi kwenye sekta za muundo wa Serikali. Kwanini nimeuita utamaduni?

Wakati Mwl. J.K.Nyerere anaelezea kuhusu maana ya Jamii ya Kijamaa alisema "Waafrika ni Wajamaa kwa Asili yao, kwa sababu kila mtu kwenye Jamii alikuwa na Wajibu wa kuzalisha kwa ajili ya watu wengine" Ujamaa: Essays on Socialism.

Kumbe, "Kama sio Mzalishaji Mali" you don't make sense, hiko ndicho kiliwafanya akina Vasco Da Gama kufanya Voyages za kutafuta ma Bullions huko India na Afrika. Na ndivyo mfumo wa Elimu ya Jamii za Kiafrika ulitaka uwe, sio ku Serve Master, NO!

LEO HII.

Tuna Elimu ambayo; inazalisha fikra ya kuajiriwa, Shida sio nini Kinafundishwa, kwa sababu hiko kina serve purpose ya Elimu (Ambayo tumerithi), Shida hapa ni PURPOSE which makes the system and content.
images%20(17).jpg


Suala la KUJIAJIRI lina uhusiano wa moja kwa moja na nini unazalisha, SISI TULIELIMISHWA ili tuwe SOKO" ndio mana leo hadi vijiti vya kuchokonoa meno "Made in China" ni kwa sababu, Elimu ya WESTMINSTER ili target tuwe 'importers' hapa ndo tukapoteana. Mfumo wa Elimu badala ya ku Support talanta ya mtu, umejengeka kufundisha Falsafa za Watu wengine ambazo Kimsingi hazimfanyi mtu kuwa Mzalishaji, badala yake zinamfanya kujenga mipaka ya namna anavyopaswa kutafsiri KIPAWA chake, kwa mawazo ya watu wengine.

TAIFA KAMA HALINA WAZALISHAJI, LIMEKUFA. Leo mtu anakuja kuuliza JF ni nini asomee, yani As if tulizaliwa wote, yaani yeye mwenyewe hajui anataka kuproduce kitu ama huduma gani, shameful!

Elimu inauwa UBUNIFU, UWEZO WA KUJITEGEMEA n.k Kwa sababu ili uwe Maana nyingine ya SERVANT ni DEPENDANT.
images%20(18).jpg


Wengi wetu tunaitwa Watumishi, bila kujua UTUMISHI ni UTEGEMEZI, tunaitwa WAAJIRIWA, bila kujua kuwa MWAJIRIWA ni TEGEMEZI.

Tunaendelea, maendeleo ni mchakato, sio matokeo. Tutafika

Mwisho
images%20(16).jpg
 
Back
Top Bottom