HARDtalk: 20 years of hard-hitting interviews - BBC News

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,304
24,192
Maadhimisho ya miaka 20 ya HardTalk
Katika maadhimisho ya miaka 20 ya uwepo wa HARDtalk ktk BBC, waendesha kipindi hicho nguli waliopita na ambao wanakiendesha kwa sasa Zeinab Badawi, Stephen Sackur, Tim Sebastian na Sarah Montague wanazungumzia umuhimu wake ktk muda huu tulionao wenye mazingira mapya na kukumbushana mahojiano yapi yalisababisha mada moto ya malumbano kutoa cheche na kushika vichwa vya habari walipowahoji watu tajika kama kuanzia kina Nelson Mandela, Donald Trump, Jean Pierre Bemba, Hugo Chavez, Meles Zenawi n.k walioonesha uwezo na umahiri wao wa kuruka mitego ya maswali magumu ya kiudadisi mithili ya waendesha mashtaka ya waendesha kipindi cha HardTalk.

Celebrating 20 years of HARDtalk, current and former presenters Zeinab Badawi, Stephen Sackur, Tim Sebastian and Sarah Montague talk about what the programme means in today's news climate. There is a look back at special moments on the programme, including footage that never made it to air.

Source : BBC News
 
Hiki kipindi ukitaka ufurahi fuatilia mjadala wa mualikwa kutoka Palestina au Israel ...hii ndio mijadala iliyokipa kiki hiki kipindi.
 
hapa tanzania ni nani aliehojiwa na mahojiano yake yaliacha mjadala mkubwa hapa bongo kama ya lissu the greatest?
Unakikumbuka kipindi cha kitimoto cha bwana mayala,unakumbuka zile za jenerali ulimwengu zilizomfanya kuhojiwa uraia wake enzi za nkapa?.Tatizo huku kwetu uhuru wa vyombo habari unamipaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakali katika kipindi hicho ni wawili tu Tim Sebastian na Steven Sackur usiombe kukutana hata Kagame alitaka kurusha ngumi siyo mchezo
 
Kuna MTU inabidi tumkamate kinguvu tumpeleke huko dunia ikashangae kituko tulichonacho!
 
hapa tanzania ni nani aliehojiwa na mahojiano yake yaliacha mjadala mkubwa hapa bongo kama ya lissu the greatest?

Nothing, No one!!

Nimeangalia ya Benjamin Mkapa mwaka 200, jamaa (Mkapa) alikuwa anatamani kukimbia ama amtie makofi mtangazaji....

Lakini mara lilipomjia hilo, alikumbuka kuwa yuko abroad ama nje ya nchi yake!!!
 
Back
Top Bottom