Harambee kwa Jimbo la Ukonga - Dar es Salaam

Harambee kwa Jimbo la Ukonga - Dar es Salaam

Bourgeoisie

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
656
Reaction score
162
RAIS KIKWETE KUONGOZA HARAMBEEKUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI UKONGA
​
Na Dotto Mwaibale

RAIS Jakaya Kikwete anategemewa kuwa mgeni rasmi katika harambeeya kupambana na Umasikini Jimbo la Ukonga ambapo jumla ys Sh Mil.600zinatarajiwa kukusanywa.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mbunge waJimbo la Ukonga, Eugen Mwaiposa alisema wameazimia kufanya harambee hiyoitakayofanyika Aprili mwaka huu ili kusaidia kupunguza mambo mbalimbaliyanayowakabili wananchi wa Jimbo la Ukonga.

Alisema fedha zitakazo patikana kwa awamu ya kwanza zitasaidiakuwainua kiuchumi wafanyabiashara ndogondogo na wajasiriamali waliopo ndani yajimbo hilo kwa kupata elimu na mitaji ya kuboresha biashara zao ili ziweze kuwazenye tija na bora.

Alisema mradi huu utawasaidia wajasiriamali kufikia malengo yaona hata kwa wale wenye ndoto za kuanzisha kilimo wataweza kupata fursa hiyo.

''Mradi huu umegawanyika katika maeneo matatu awamu ya piliitashughulikia changamoto za elimu wakati awamu ya mwisho watajikita zaidikwenye changamoto ya maji safi na salama pamoja na afya " alisemaMwaiposa.

Aliongeza kuwa ili kufikia malengo hayo kunahitaji nguvu yapamoja baina ya serikali, wananchi, taasisi mbalimbali na jamii kwa ujumla nawapenda maendeleo.

Mwaiposa alisema jitihada za kuanzisha mradi huu zilitokana nautafiti uliofanyika katika Jimbo hilo na kuonesha wananchi wengi wana nia yakujiajiri katika kilimo na biashara ndogo ndogo lakini hawana elimu ya biasharana mitaji.

Alisema katika uchunguzi uliofanyika ilibainika wananchi wengiwaliojiunga na VICOBA mwaka 2010 walishindwa kufanikiwa kwa malengowaliyojiwekea na kufeli kwa miradi au biashara zao walizokuwa wamezianzisha.

Mwaiposa alifafanua kuwa VICOBA 102 vyenye jumla ya wanachama2010 vilijiunga pamoja na kuunda taasisi ya saccos mwaka jana inayoitwa UkongaVicoba Saccos Ltd, (UVICOSA), ambayo hadi sasa ina mtaji wa Sh 8,000,000 ambaoni mdogo ukilinganisha na wingi wa wanachama.


Source:mwaibale.blogspot.com

My take: Sidhani kama hivyo vilivyotajwa kama vipaumbele kuanza kwenye awamu ya kwanza ya uchangishaji huo ndivyo wanavyohitaji wakazi wa hili jimbo.

Jimbo hili lina changamoto nyingi kama barabara na umeme ambavyo ni vitu muhimu kuanza kushughulikiwa kabla ya hizo biashara ndogo ndogo.

Kuna eneo linaitwa Bombambili-Kivule walikohamishiwa wakazi wa kipawa kwa ahadi kemkem za maji safi, barabara, shule,hospitali na umeme lakini hadi sasa yapata mwaka wa tano vitu hivyo kwao vimekuwa ni hadithi!

Ushauri wangu kwa Mbunge huyu ni kuwapatia wapiga kura wake hayo niliyotaja kwanza na mengine kufuata.

Nawasilisha.


 
Back
Top Bottom