Haraka ya serikali katika hili la gesi ya mtwara linatia shaka!

Haraka ya serikali katika hili la gesi ya mtwara linatia shaka!

nsami

Senior Member
Joined
Jun 11, 2010
Posts
175
Reaction score
9
Wakuu,

Hii haraka ya serikali katika hili la gesi ya mtwara linatia shaka, nachelea kusema kuna kinachofichwa. Mwl Nyerere aliwahi kusema madini hayaozi hatuna haraka nayo lakini kwa serikali ya awamu ya nne imekuwa kinyume. Hiyo gesi ya mtwara utadhani nyanya iliyoiva shambani kwamba usipoitoa leo basi ama itaoza au kuliwa na ndege.

Serikali makini ni ile inayosikia kero za wananchi na kuzishughulikia pamoja na matatizo ya kisera ndipo iruhusu shughuli zote za kuvuna gesi huku kukiwa hakuna anayelalamika wala kunung'unika. Kufanya hivyo kutafanya wananchi wa maeneo yote yatakayohusika na kuvuna na/au hata kusafirisha gesi hiyo kushiriki kikamilifu katika kufanikisha mradi ikiwa ni pamoja na kufichua mbinu chafu za kuhujumu mradi kutoka kwa maadui wa mradi.

Hali ilivyo sasa ni dhahiri wananchi wenyewe wa maeneo yatakayohusika kuvuna na/au kusafirisha gesi ndio wamekuwa maadui wa kwanza wa mradi. Hata wakinyamazishwa/kutishwa kwa virungu, mabomu risasi na hata vitu vizito au vyenye ncha kali, bado havileti amani maana amani sio kutokuwa na maandamano!

Mchawi katika hili la mtwara sio CDM wala CUF kama wengi wanavyodhani, mchawi ni serikali yenyewe. Na kama wanadhani wananchi wa mtwara wanachochewa na kutumiwa kisiasa, nawashauri serikali na chama tawala (CCM) waelekeze nguvu zao za kisiasa mtwara ili nawenyewe wawachochee kutokufanya vurugu. Yuko wapi Kinana, maana akiwekeza nguvu zake Mtwara angalau Tembo wapumue kidogo maana nilisikia kuwa nguvu yake ya uchumi iko serengeti.

Wapumzike kwa amani wote waliopoteza maisha katika vurugu za leo-Amen
Nawasilisha.
 
Ni kweli haraka ipo na itaendelea kuwepo. Hata wawekezaji washajua kwamba hawa jamaa mwisho wao ni 2015. Sasa kwa nini wasijichotee kabisa ili watakaokuja watapambana na mikataba feki wakati jamaa wanakula bata majuu.
:A S 576::kev::nod:
 
Wakuu,

Hii haraka ya serikali katika hili la gesi ya mtwara linatia shaka, nachelea kusema kuna kinachofichwa. Mwl Nyerere aliwahi kusema madini hayaozi hatuna haraka nayo lakini kwa serikali ya awamu ya nne imekuwa kinyume. Hiyo gesi ya mtwara utadhani nyanya iliyoiva shambani kwamba usipoitoa leo basi ama itaoza au kuliwa na ndege.

Serikali makini ni ile inayosikia kero za wananchi na kuzishughulikia pamoja na matatizo ya kisera ndipo iruhusu shughuli zote za kuvuna gesi huku kukiwa hakuna anayelalamika wala kunung'unika. Kufanya hivyo kutafanya wananchi wa maeneo yote yatakayohusika na kuvuna na/au hata kusafirisha gesi hiyo kushiriki kikamilifu katika kufanikisha mradi ikiwa ni pamoja na kufichua mbinu chafu za kuhujumu mradi kutoka kwa maadui wa mradi.

Hali ilivyo sasa ni dhahiri wananchi wenyewe wa maeneo yatakayohusika kuvuna na/au kusafirisha gesi ndio wamekuwa maadui wa kwanza wa mradi. Hata wakinyamazishwa/kutishwa kwa virungu, mabomu risasi na hata vitu vizito au vyenye ncha kali, bado havileti amani maana amani sio kutokuwa na maandamano!

Mchawi katika hili la mtwara sio CDM wala CUF kama wengi wanavyodhani, mchawi ni serikali yenyewe. Na kama wanadhani wananchi wa mtwara wanachochewa na kutumiwa kisiasa, nawashauri serikali na chama tawala (CCM) waelekeze nguvu zao za kisiasa mtwara ili nawenyewe wawachochee kutokufanya vurugu. Yuko wapi Kinana, maana akiwekeza nguvu zake Mtwara angalau Tembo wapumue kidogo maana nilisikia kuwa nguvu yake ya uchumi iko serengeti.

Wapumzike kwa amani wote waliopoteza maisha katika vurugu za leo-Amen
Nawasilisha.

kwa hilo mimi hujanishawishi sanasana nikuweka kundi moja na wale wachochezi sisi tunataka maendeleo y halaka na wewe unaleta zako porojo huu uchochozi adhabu yenu mungu anaijua.
 
Gesi kwanza, amani na utulivu wa Bagamoyo baadae!!!!!!!!
 
kwa hilo mimi hujanishawishi sanasana nikuweka kundi moja na wale wachochezi sisi tunataka maendeleo y halaka na wewe unaleta zako porojo huu uchochozi adhabu yenu mungu anaijua.

Hayo maendeleo ya haraka kama yepi?? IPTL, DOWANS, MEREMETA na Makaa ya mawe vilitangazwa nchi nzima kuwa sasa mgao wa umeme kwisha na bei zitashuka hadi watanzania watapikia, tena makaa ya mawe tukaambiwa yatasambazwa ili watu wapikie pia lakini mpaka sasa hara rangi hayajulikani. Yote tuliyoambiwa yanaleta maendeleo na upatikanaji wa umeme leo ni MAJANGA MATUPU na kuviziana kwa kuficha taarifa na kukataa kuziongelea faida zilizotangazwa.

Pia rejea uchimbaji wa madini huko kanda ya magharibi, Wananchi tuliaminishwa taifa kunufaika na madini lakini kinachoshuhudiwa ni maumivu pekee huku Deni la TAIFA LIKIZIDI KUNENEPA.

KIUFUPI HUU NI WIZI UNAOFANYWA MCHANA KWEUPEEE NA VIONGOZI WETU,
WITO WANGU NAOMBA WAREJEE ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI, SERA ZA CHAMA Pamoja na Azimio la Arusha ambalo ndio msingi wa CHAMA CHETU.

Huyu ni Sawa na Jambazi anapokuingilia katika ofisi yako anadai kila kilichopo na ukikataa kutoa anaweza kutoa hata uhai wako. Ndicho kinachooneshwa na Serikali yetu sasa. VIONGOZI CHONDE CHONDE ACHENI UBABE WA KUJALI MASLAHI BINAFSI BADALA YA TAIFA.
 
kwa hilo mimi hujanishawishi sanasana nikuweka kundi moja na wale wachochezi sisi tunataka maendeleo y halaka na wewe unaleta zako porojo huu uchochozi adhabu yenu mungu anaijua.

Mkuu mimi ku.

Sikutegemea kuungwa mkono na watu wanaokuja jamvini kutafuta 7,000 ya siku. Maendeleo ya haraka? Haraka ni miaka mingapi? CCM imekuwa madarakani miaka zaidi ya 50, leo wanadai wana haraka ya maendeleo. Au kwako wewe maendeleo ni kuua wananchi wasio na hatia? Wananchi wameona hawasikilizwi, wakaona njia pekee ya kulazimisha masikio ya watawala wao kutega sikio ni kuandamana na kupaza sauti zao. Matokeo yake ni kuwageuzia mitutu ya bunduki na mabomu?

Aibu zenu mafisadi nyie, narudia tena. Kama serikali na CCM wanaamini vurugu za mtwara zinatokana na uchochezi wa kisiasa, CCM ni chama cha siasa, tena kikongwe, si waende pia wakawashawishi wananchi kisiasa ili wawaelewe?

Serikali yetu, ingependa kila kitu kiwe Dar, kwani huko Dar kuna nini? Je mtwara sio Tanzania? Mimi naamini kuwa serikali kama ingekuwa na uwezo wa kuhamisha mlima kilimanjaro, machimbo ya tanzanite mererani, mbuga ya serengeti, machimbo ya dhahabu ya geita na kwingineko, nk wangevipeleka vyote vilundikane huko Dar. Shame on them. Kama tembo wangeweza kufugiwa lumumba, nadhani tembo wote wangehamia huko, ili kinana asihangaike kwenda kuwasaka porini.

Na kama huo ndio uchochezi, wacha niwe mchochezi pia.
 
....kweli mkuu M.M Nkunya, katika vurugu zote, mabomu,mauji ya padri,arusha maandamano,udini n.k sikuwahi kusikia kauli ya rais ikitoka haraka kiasi hiki..! mtwara kunanini mbona wamekuja haraka na kwa vitisho namna hii...!!??
 
Last edited by a moderator:
....kweli mkuu M.M Nkunya, katika vurugu zote, mabomu,mauji ya padri,arusha maandamano,udini n.k sikuwahi kusikia kauli ya rais ikitoka haraka kiasi hiki..! mtwara kunanini mbona wamekuja haraka na kwa vitisho namna hii...!!??

Serikali ingekuwa na haraka ya kuwaburuza mafisadi mahakamani, kushughulikia matukio ya vurugu za kidini, kushughulikia madai ya walimu na madaktari, ujenzi wa barabara, kutetea wachimbaji wadogo migodini nk tungeisifu sana. Lakini sasa tuisifu kwa lipi? Haraka zipi? za kusafirisha twiga hai mpaka ugaibuni? kugawa vitalu vya uwindaji? kufyonza gesi? au haraka ya kuunda tume ya kuchunguza kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa kidato cha nne 2012 huku matokeo ya utafiti wa kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa kidato cha nne 2010 hayajafanyiwa kazi? Hawana haya kabisa hawa!
 
Tulipigwa na tunaendelea kupigwa. Kuna muswada wa marekebisho ya ile sheria ya kulinda rasilimali uko bungeni muda huu. Unaondoa kabisa ile oversight ya bunge na kuhamishia kwa baraza la mawaziri. Nikawaza nishushe uzi kuelezea madhara yake lakini nikajisemea acha tu iwe hivyo. Nchi imepigwa na itaendelea kupigwa sana.
 
Back
Top Bottom