Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 277,399
- 720,833
Leo tarehe 21 mwezi March katika elimu ya Jiografia ni kwamba Jua lipo katika mstari wa Ikweta ambao unaigawa dunia katika sehemu mbili yaani *hemispheres* kwa maana ya upande wa Kakazini na Kusini ... *Northern Hemisphere* and *Southern hemispheres*. Kwa maana hiyo leo tarehe 21 mwezi Machi na tarehe 23 mwezi September jua linakuwa katika mstari wa Ikweta ambao unaigawa dunia katika sehemu mbili yaani Kaskazini na Kusini.
Hivyo leo sehemu zote duniani urefu wa mchana na usiku unalingana. Yaani kwa maana nyingine sehemu zote duniani zinapata urefu sawa wa mchana na usiku. Hali hii kijiografia inajulikana kama *Equinox* yaani maana yake *equal night and equal day*.
Hii inamaanisha nyakati zingine zote ukitoa hizi siku mbili yaani tarehe 21 Machi na 23 Septemba urefu wa usiku na mchana hutofautiana.
Nakutakia siku njema ya *Equinox* yaani Equinox day ambayo sehemu zote duniani urefu wa usiku na mchana unalingana.
*I like Geography*
Jr