GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,651
- 14,318
Wadau naomba tuweze kuwasaidia wachezaji wa team zetu kimawazo. Tufaham kwanza wachezaji wetu wengi hawana Elimu na pia hawana ushauri wa kisaikolojia. Hawajajengwa kifikra au Kisaikolojia kuwa super stars. Hii inawafanya sifa za msimu mmoja tu walewe mpaka kujitapikia.Tujiulize akina okwi walitamba misimu mingapi hapa Bongo?akina Tambwe n.k nini kimwapata watu kama akina Msuva? Kwa nini akina messi na ronaldo wanaendelea kuwa wazuri. Ni nini wachezaji wetu wanakuwa mara nyingi msimu mmoja au miwili? Hasa kwa kizazi hiki. Zamani tulikuwa na wachezaji wazuri kwa muda mrefu. Tuwasaidie kwa kuwapa ushauri nasaha, ushauri wa kitaalamu na pia waelewe mpira ni kazi si sehemu ya kutafutia umaarufu na wanawake.Tuwape ushauri na pia kuwaonya/kuwaadhalisha