Hapa Sijaelewa!!!

Mrimi

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
1,691
Reaction score
641
TCRA wanasema local chanels 5 (TBC1,ITV,EATV,StarTV&Ch.10) zitakuwa free kwenye ving'amuzi,kwa maana kwamba hata mtu asipolipia ataendelea kuziona.Sasa,je ikitokea watu wenye ving'amuzi wakaridhika kutazama hizo chanels 5 tu na wasiendelee kulipia nini kitatokea?Je haya makampuni yatajiendeshaje?

Kwa upande mwingine,ukweli ni kwamba watu wanaotumia satelite dishes huu mchakato hauwahusu,ni kwa nini serikali wametumia nguvu nyingi kuhimiza watu kununua ving'amuzi vya kulipia badala ya kuwahimiza kununua madishi na kupata matangazo free? Je,serikali ina mpango wa kuondoa local chanels zote kwenye madishi na kuingiza kwenye ving'amuzi,kama walivyofanya ATN?

Nionavyo mimi mtu anayetumia satelite dish ana advantage zaidi kwa kuwa ana uwezo wa kupata chanels nyingi bure kuliko hizo 5 watakazoonesha bure kwenye ving'amuzi.Na watalamu wa mambo haya wanasema asilimia kubwa ya chanels zinazouzwa katika ving'amuzi zinaweza kupatikana bure kwenye haya madish!

Au nyie wenzangu mnalionaje hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…