Hapa piga ua, talaka yangu utatoa tu...

Ma Mshuza

Senior Member
Feb 26, 2019
192
1,021
Binadamu si wa kuwaamini hata. Yaani mtu mwingine ni rafiki lakini kumbe hakutakii mema. Nliusikia huo wimbo wa Bend moja hapa nchini. Wanaimba wanasema hapa piga ua talaka yangu utatoa, ama sivyo ee bwana we nitakuonesha..

Nikaandika kwenye status yangu HAPA PIGA UA TALAKA YANGU UTATOA. Chini kabisa nikaandika jina la Band.

Watu hawakuona jina wameona tu hayo maneno. Walianza kububujika whatsapp wakiniambia tena mume wangu wala asinizingue kama akinipga tena nikamshtaki.

Wengi wamenipa pole na wakaka kutaka nitoke nao ili kupoteza mawazo. Nikawa nashangaa...marafiki zangu wananambia heri niwe huru wanaume wapo wengi.

Waswahili ni wanafiki sana tena wambea.wanawake kwa wanaume.yaani wanaamini mtu msomi anaweza weka maisha yake kwenye mitandao? sikuwajibu kitu. After 24 hrs nmeweka picha nipo na mume wangu wamenyamaza mpaka muda huu kimya.

Nyie jamani sisi binadamu hatupendani kabisa.yaani tunashawishiana kwenye mabaya utadhani sijui nini.khaaaah...mi nmewashindwa kabisa. Wao walishaamini maneno ya huo wimbo ndo maisha yangu.
 
Mkuu tania lingine sio talaka itakunyemelea tu ni suala la mda achana utani katika divorce in a blink of an eye mambo yana badilika tena......unalia na hilo bandiko lako linakua relevant kabisa
 
Msondo ngoma hapa moshi, ngurumo pale momba, masharubu na pembeni mabela na romarii.
Nimekua sina raha apa nyumbani kila Siku maneno yako mama hayaishi mama, nimekua sina amani apa nyumbani kila Siku maneno yako mama hayaishi mama.
Nakupa talaka kwa shingo upande.
 
Huwa nawashangaa sana watu ambao mambo ya ndani ya familia yako mara unaweka status whatsap au any social media hili iweje sasa utakuta mara ndoa yangu ina shida shame on you sasa unataka matatizo yako unamtangazia nani, wanawake hizo tabia mnazo sana acheni mambo ya uzungu matatizo yanatatuliwa ndani sio kwa watu wa nje

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mapenzi ya utoto na ujinga kujianika mitandaoni na kuonyesha kila kinachotikea kwenye mahusiano yako kwenye mitando. Kumbuka hayo ni mahusiano yako sio community project. Ebu jitaidini kustili furaha zenu na huzuni zenu moyoni mwenu sio mtuwekee kwenye mitandao kututangazia binadam sio wazur
 
Waswahili ni wanafiki sana tena wambeya.wanawake kwa wanaume.yaani wanaamini mtu msomi anaweza weka maisha yake kwenye mitandao.sikuwajibu kitu. After 24 hrs nmeweka picha nipo na mume wangu wamenyamaza mpaka muda huu kimya.
Ndo ushaweka kwenye mtandao🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom