IsayaMwita huyo muungwana anafanya usanii tu na ni watu kama wewe mnaozugika na tabasamu lake mnafikiri ndio maendeleo!! Huyu muungwana akiwa majukwaani analaani RUSHWA lakini kwa hisia na vitendo vyake anatetea wala rushwa ama sivyo Lowassa, Rostam, Karamagi na Msabaha mpaka sasa wangekuwa lupango. Angalia kwenye chaguzi za CCm, yeye ni mwenyekiti; wagombea wanapeleka ushahidi wa waziri wake anatoa hongo kwenye uchaguzi wa uwT, badala ya kumuadabisha yeye anayetoa hongo tena waziri wa utawala bora ndio kwanza anakwenda kumpigia debe eti msomi; huko ndio kuipiga vita rushwa kweli!! Aaangalieni wasiopenda rushwa wakina Kagame wanavyofanya
Nakubaliana na nawe IsayaMwita, kuwa makini ni lazima kama tunataka kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi ; inatubidi tuwe na mkakati wa kuwaelimisha wenzetu hasa wale waishio vijijini ambao ndio wanateseka sana na matokeo ya ufisadi ya CCM. Unfortunately, CCm ndio inawalenga hao hao inaowatesa, kwa kuwahonga khanga na fulana wakati wa uchaguzi na kuifanya kama hazina yao ya kupata kura za kutawala nchi!! Operasheni kama hii ya SANGARA isiwe nguvu ya soda bali ipambe moto kwa wanachama wa vyama vya upinzani hasa CHADEMA na CUF katika sehemu ambazo wanajua wanawafuasi wengi huko ndio waanze kujiimalisha kabla ya kwenda kwenye sehemu mpya. Ni muhimu kukaa na kustrategize badala ya kukurupuka na ni vizuri pia kama matayarisho yakaanza sasa badala ya kungoja karibu na uchaguzi!! Chadema na Cuf wasitegemee ruzuku bali wawategemee wanachama wao kutoa michango ya hali na mali ili kufanikisha mobilisation campaign zao.
Maane hebu ni evidence gani utahitaji kuona kama jamaa anaweza hata kumsariti hata rafiki yake mpenzi(Rowasa)[/QUOTE]
Ama kweli huyu ni IsayaMwita.