IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
- Thread starter
-
- #21
Dark City kama huelewi tofauti ya success na failures sana itakuwa jambo lingine hlo.
Pia Msanii aliahidi kupitia na kurekebisha mikataba ya sekta ya madini. Kwa kweli mpaka leo mimi sijaelewa kabisa deliverables muhimu katika hili?
Suala la mpasuko wa kisiasa Zanzibar alilojifanya kuongea kwa hisia kali sana, mpaka leo ni kitendawili.
Suala la nyumba za serikali walizoziuza wakati wa Mkapa aliloahidi kulipitia mpaka leo anasuasua tu.
Hoja:
Kama ameshindwa kuyafanya yote hayo na mengineyo kipindi cha kwanza cha miaka mitaka (hadi mwakani) ikiwa ingekuwa ni vyema kwa ajili ya kugombea kipindi cha pili, sidhani kama kipindi cha atakuwa na changamoto yoyote muhimu kwani anajua hataweza kugombea kwa mujibu wa kikatiba.
Kumbukeni hata Chinga Mkapa alifanya madudu sana kipindi chake cha pili.
Kazi kwetu.
La muhimu ni wa Tanzania ni kuchagua wabunge wengi wa upinzani ili kuweza kulipa bunge guvu ya kuidhibiti serikali.
Jambo lililo dhahiri ambalo JK, watangulizi wake, TANU na CCM ni kushindwa kudeliver a very basic right kwa kila mtu nayo ni maji safi na salama. Hata pale yanpopatikana kiasi basi ngonjera za kuchemsha maji haziishi!
Unless kiswahili kimebadili maana ya mafanikio, lakini mafanikio ni hali chanya kuelekea lengo fulani, kama vile la maendelea, sasa kama uanendelea kuelekea nyuma hayo ni matatizo sio mafanikio tena
Mkuu Kaizer, kuna mafanikio negative pia. Kuna mafanikio ya kubomoa, kuna mafanikio ya wizi, kuna mafanikio ya kudhalilisha, kuna mafanikio ya kuharibu vile vile na mafanikio mengine mengi yasiyofaa. Kinachofanya mafanikio hayo kuwa chanya au hasi ni nia ya jithada zinazotumika kuyafanikisha.
Maane hebu ni evidence gani utahitaji kuona kama jamaa anaweza hata kumsariti hata rafiki yake mpenzi(Rowasa)
ndugu isaya mwita, mi nadhani unakashughuli kanakokupatia vijisenti na imekuwa ni kama pazia ambalo uwezi kuona maendeleo ya wenzio, maendeleo ya nchi ayapimwi kwa kipato cha mmoja mmoja.
1. tuliambiwa kutakuwa na ajira 100000, naona wewe upo miongoni mwa hizo
2. kuna mabilioni ya kikwete, labda wewe ndio umetokea humo
ukiona kwenye nchi mpaka chumvi inapanda bei basi hiyo ni balaa
jaribu kuwa muungwana basi watanzania wenzako wanakuomba umwage mafanikio aliyoyafanya huko Mpiganaji
Kituko;
Wito wangu wana Jamii forums tunatokaje 2010?
Kule Mara najua CCM hawatakuja kabisaaa!!!!!!!!,
Mnakumbuka sherehe za CCM 2009 zilifanyikia wapi?
Eti kuimarisha chama.......... wapi Mkoani Mara????????
Mkuu I Mwita, mbona sherehe za CCM 2009 (miaka 32) zilikuwa Shinyanga? Au kuna nyingine unaongelea?
Kwa jinsi Muungwana anavyo wajibika kwa sasa si ndiyo anazidi kukiruka kiunzi 2010? hatujui tutamrushia madongo yapi, kwani yeye kama yeye hakika anaendelelea kuisafisha ile njia,
Tuangalie tusije tukakosa mshiko, !!!!!
Nadhani zile hoja za kufichua ufisadi tungeanza sasa si mwaka jana, hawa jamaa wanaendelea kujisafisha
Sijaelewa kwamba wanapowapeleka akina Mramba baada ya uchaguzi watawafutia kesi zao ama?
Nimeipenda ile style yao.
Ama nina makengeza?
The man is trying to play out cards. However its too late!
sayamwita;375997]
Dark City;
walichinja nini huko shy?
Sijapata kusikia habari ya sherehe za Serengeti. Labda makada wa Chama Chao humu ndani watatupa data.Mkuu wangu kama sikosei pale serengeti kulikuwa kunaadhimishwa nini?
Mkuu naona unataka idendity yangu kwa nguvu au? Soma profile yangu kwanza ujue niko wapi halafu ndo upigie mistari miwili (conclusion) kwamba niko mjini.Dark City;mimi kama mimi najua mabadiliko yanakuja japo wewe Dark City; haujafanya chochote katika mkoa wako na watu wako, nakushauri toka huko mjini rudi kule kwenu kijijini kawaelimishe ndugu zako kawaambie jinsi CCM WALIVYOTUFANYA MIAKA 48 hii.
Dark City; acha kung'ang'ania mjini
mnamtafuta mshindi wa 2010 kwa ticket ya CCM, Chadema, TLP au CUF? Nijuavyo mimi kila chama kitapitisha na kitamsimamisha mgombea wake, baada ya hapo wananchi wapima sifa kila mgombea. CCM hawajesama kuwa JK ndiyo mgombea wao, vyama vingine pia wavijasema mgombea atakuwa yupi hapa tupambanisha nani na nani?
Uchumi
Yapo matatizo ya kidunia mbayo hata JK asingeweza fanya miujiza ya kuibadili TZ haraka hivyo, USA yenyewe pamoja na kuwa na uchumi wenye nguvu kwa hali yao ya sasa wanasema hawawezi jichomoa over night sembuse TZ? Hata hivyo kisiasa inakubarika na mtu anaweza itumia kuisambaratisha CCM au kumuangusha mtu hata kama mtu huyo siyo factor. Hilo ndio tatizo la siasa ama wanasiasa......kutungushia maneno ili wapate kura.....
baadhi ya mafaniko ya Jk
1. kajenga chuo kikuu Dodoma
2. makusanyo ya kodi yameongezeka kutoka bilioni 195 wakati wa Mkapa hadi bilioni 400
kila mwezi ambayo ni mara mbili
3. kapunguza ujambazi.
4. kapeleka watuhumiwa wa EPA mahakamani
5. Kamwachisha kazi Waziri Mkuu Lowassa
6. Amenunua Panton jipya Kigamboni linabeba magari 60 na abiria 2000
7. Ameokoa shirika la ndege ATCL kwa kuwapa mtaji mpya
8. Amerudisha nyumba za serikari 120
9. amesimamisha ununuzi wa magari ya serikali ( mashangingi) na pesa hizo ziende katika ununuzi wa matrekta.