Hapa kazi tu, Nani kapata nani kakosa?

Mar 17, 2016
71
91
Kwa kipindi tukiwa tunaelekea uchaguzi mkuu wa mwaka jana tulikua na mjadala mkubwa wa aina gani ya kiongozi(rais)anatufaa hasa kutokana na mwenendo wa hovyo wa muongo mmoja wa uongozi wa JK uliokua unaishia ambao uliacha kila mtu mwenye nafasi ajifanyie na kujitwalia chochote anachotaka kana kwamba serikali haipo.Watu kadhaa walipiga kelele kwamba serikali haitimizi wajibu wake wa na baadhi wakaweka rekodi sahihi kabisa kwa kusema "rais ni dhaifu" hivyo tulipaswa kupata raisi jasiri asiyesita kufanya maamuzi sahihi bila kuonea haya mtu.

Labda katika hali ya kukata tamaa wapo pia baadhi ya wananchi walienda mbali zaidi na kusema tunahitaji raisi mwenye "UDIKTETA KIDOGO" kurudisha taasisi na watumishi wa umma kwenye msitari ulionyooka.
Andiko langu litajaribu kuibua mjadala wa wazi kwa kuzingatia tamthini fupi ya kijumla ya uongozi wa awamu ya tano ndani ya takribani miezi saba tangu kuingia madarakani.

Kwanza tuyatambue makundi ya watu/wananchi na matarajio yao kuhusu matokea ya uchaguzi na nini yalikua matamanio/matarajio yao na serikali ya awamu ya tano;

WANANCHI WA KAWAIDA
Hawa ni wananchi huru (free from strong political affiliation) ambao kwa kiasi kikubwa ndio walikua wahanga wakubwa wa mambo ya hovyo kwenye serikali iliyopita.Ni kundi kubwa ambalo japokua kwa kiasi walikua wanaunga mkono vyama fulani lakini hawakua na maslahi binafsi na ya moja kwa moja katika vyama vya siasa wala msukumo wa kiitikadi(vyama vyote havina msingi wazi wa kiitikadi),hivyo matarajio yao makubwa yalikua ni uimarishwaji wa huduma za kijamii na kupungua kwa ugumu wa maisha.

Hawa ndio ambao kwa miaka yote hamsini ya uhuru wanaguswa moja kwa moja na kila tatizo hata yale ya aibu(kulingana na umri wa taifa letu),watoto wao kukosa madawati,ukosefu wa madawa ya msingi,ubovu wa miundo mbinu,ukosefu wa maji safi na salama,ughali wa gharama za maisha, kukosekana kwa huduma za msingi za afya n.k kiufupi hili ndio lile kundi linaloishi "KAMA MASHETANI".

WALICHOPATA.
Kwanza niweke wazi kwamba kwa asilimia kubwa hili ni kundi na watu wasio na information za kutosha na kwa kiasi kikubwa hawana muda na vitu venye kufikirisha sana.Maelezo pekee ya hali hii inaweza kukosa uelewa/upeo (si kwa matusi) au wanazongwa zaidi na kupambana na ugumu wa maisha hivyo hawana luxury ya kuumiza kichwa kwenye mambo wanayoona hayawagusi moja kwa moja.

Hili ndio kundi mpaka sasa lililoridhika zaidI kati ya makundi yote kwani kwa kawaida huguswa sana na matamko na maamuzi popular na kwa bahati nzuri serikali ya awamu ya tano si haba kwa mambo hayo . Matukio kama kushughulikiwa kwa watuhumiwa wa ufisadi,wakwepa kodi,watumishi wazembe,sera ya elimu bure ya msingi n.k yamewapa imani kubwa na wananchi wa kundi hili.Ni nadra sana kukuta kundi hili likijikita kwenye tathmini ya kina ya tija na athari za maamuzi ya serikali kwenye vitu kama sera,mwenendo wa bajeti mpya,uhuru wa mihimili ya serikali,uhuru wa vyombo vya habari,mipango ya kupunguza ukosefu wa ajira,sera na sheria za kodi,masuala ya hifadhi ya jamii badala yake huridhika kirahisi na vitu vinavyoshikika.
Pamoja na hayo ukweli ni kwamba, katika siasa za nchi maskini kama yetu huwezi kudharau matakwa ya kundi hili kwani kwa bahati mbaya ndio kundi kubwa zaidi(kutokana na uwekezaji mdogo kwenye sekta ya elimu) hivyo ndio mtaji mkubwa wa wapiga kura.

Vilevile vitu vinavyotarajiwa na kundi hili kama uboreshaji wa huduma za jamii na miundo mbinu ndio msingi mkuu wa serikali zetu.Jambo la msingi hapa ni kule kukosekana kwa uelewa kwamba vile vitu vinavyozungumzwa sana na makundi mengine ndio hasa hupelekea(overriding factors) za upatikanaji wa haya mambo yanayotazamwa kama mambo muhimu zaidi na kundi hili.

VYAMA VYA UPINZANI
Hili ni kundi linajumuisha vyama vya siasa kama taasisi,wapenzi na wanachama 'kindakindaki' na viongozi wao.Ni watu waliokua wanalalamikia sana (most vocal)mwenendo wa hovyo wa serikali ya awamu ya nne hasa katika eneo la ubadhirifu wa mali za umma na kukosekana kwa mipango na nia thabiti ya kuondoa umaskini nchini.

Kwa kipindi chote walikua mstari wa mbele kuonyesha udhaifu wa serikali na kuibua kashfa nyingi za ufisadi kama EPA,RICHMOND,ESROW na ubadhirifu mkubwa kwenye miradi ya maendeleo na serikali za mitaa.Kutokana na haya yote na kukosekana kwa hatua thabiti kutoka kwa serikali hasa rais wakajumuisha kwa kumpa lebo(anayostahili) ya "rais dhaifu".

WALICHOPATA.
Mwanzoni mwa utawala wa serikali ya raisi Magufuli vyama vya upinzani vilionekana kupata changamoto kubwa.Hii ilitokana na mtindo wa utendaji kazi wa raisi kwenye kushughulikia kwa haraka kasoro nyingi serikalini ambazo kwa kipindi kirefu zilikua ndio msingi mkubwa wa hoja za ushawishi wa upinzani.Huku akichagizwa na kauli yake aliyoirudia mara kwa mara kwamba yeye ni rais wa wanyonge. Ilionekana wazi vyama vya upinzani vilitakiwa vijipange upya kimkakati kama vilitaka vibaki na ushawishi kwa watanzania wa kawaida ambao walianza kumuona raisi Magufuli kama mwokozi wao.

Hatua yoyote ya kumkosoa raisi ilionekana kama ni "political suicide" huku proganda kubwa ikipigwa kwamba wanaomkosoa au kumpinga rais kwa baadhi ya hatua zake hasa kutoheshimu utawala wa sheria na kuingilia mihimili mingine basi ni mafisadi au watetezi wa mafisadi.Wapinzani waliandamwa kwa kile kilichoonekana ni unafki kwani raisi aliyepita walidai DHAIFU huyu wa sasa anatenda kwa haraka wanamuita DIKTETA.Swali dogo la kujiuliza hapa tangu lini tofauti ya UDHAIFU ikawa ni UDIKTETA?

Lakini kama ilivyo kawaida siku zote muda hauongopi kwani baada ya hatua za mwanzo ambazo kwa kiasi kikubwa zilikua nzuri na popular uzito wa nafasi ya urais na udhaifu wa busara za kiuongozi ukaanza kua wazi. Serikali ikaanza kuonyesha wazi dhamira ya kukamata mihimili mingine hasa bunge na sasa ilionekana wazi nchi inaanza kuendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja.Kukaanza kuwepo maamuzi mengi yasiyotumia busara kama la wanafunzi wa UDOM,matamshi ya kukurupuka yasiyoendana na uzito wa nafasI ya urais na zaidi kushindwa kuhimili ukosoaji na kuzuia shunguli za vyama vya upinzani.Haya yote yakageuka ni 'blessing in disguise' kwa wapinzani kwani wamepata mifano hai ya kuonyesha elements za kidikteta za utawala wa awamu ya tano.

Hii kwa upande wa serikali na CCM imekua ni moja ya textbook definition ya political blunder.Kwahiyo kiujumla wapinzani wamepoteza kiasi hasa kwenye ule uhuru wa kufanya shughuli zao za kisiasa na ile nafasi ya kuvumbua kasoro za kifisadi ambazo kisiasa zilikuwa zina uwezo wa kugusa wananchi kirahisi lakini kwa upande mwingine wamepata changamoto ya kuvihulisha vyama vyao na kua na agenda nzito za kisera huku zikiipa presha serikali ambayo imeonyesha ina udhaifu mkubwa wa kuhimili pressure za kisiasa na mikakati ya kisera kumaliza changamoto za kimaisha za wananchi ikiwekeza zaidi kwenye kufanya maamuzi ya kufurahisha macho na masikio ya wananchi.

CHAMA CHA MAPINDUZI
Kwa muktadha wa hapa simaanishi wanachama bali wenye chama chao hasa.Maana siku zote nimekuwa nikiwa na msimamo kwamba inahitajika uwendawazimu kiasi kwa mwananchi wa kawaida,maskini asiye na manufaa ya mojakwamoja kujinasibisha kwamba yeye ni mwana CCM.....Kama wasemavyo (CCM ina wenyewe).Hili ni kundi dogo la viongozi serikalini na katika chama ambao kwa muda wote wamekua wanufaika wakubwa wa uozo wa serikali zilizopita.Ndio ambao wakati vyama vya upinzani,wananchi na asasi za kiraia zikipiga kelele kwamba nchi imegeuka shamba la bibi walikua wakibeza na kusifu kwamba MAMBO YAKO SAWA KABISA,ACHA TUMEZOEA KELELE ZAO,SISI TUNASONGA MBELE!.

WALICHOPATA
Usishangae wale watu waliokua wakipinga bandarini na taasisi zingine hakuna wizi huku wakibeza wananchi,asasi za kiraia na viongozi wa vyama vya upinzani kwamba wanajifanya wana habari za ndani za usamalama wa taifa wameenda wapi?bado wamo serikalini na ndani ya chama na leo ndio wapiga zumari wakubwa kwamba huyu ndio rais sasa,hajawahi kutokea baada ya Mwl.Nyerere na hapaswi kukosolewa ni msafi kama theluji kifupi ni malaika.Kwao umahiri wa unafiki ndio mtaji kwani in petty politics there is no nobility to be on loosing side.

Wanajipiga kifua kwamba wamepata walichotaka kana kwamba hakuna mtu anayefahamu kwamba Rais wa sasa ni zao la msuguano ndani ya chama na wala si mpango maalumu wa chama.Ukweli unabaki kwamba kwa kiasi kikubwa wamepoteza vingi kwani walizoea kuishi kwa kupiga 'deal' na sasa wamepoteza hata ule ushawishi ndani ya serikali na chama kwakua bwana mkubwa kwa hulka yake ya kujua kila kitu amewabakiza kama picha tu. Kitu pekee kinachowapa nguvu ni ule umahiri wao wa kuifanya kila hali kua na manufaa kwao(angalau hadharani) lakini habari njema ni kwamba wakikaa wao kwa wao wanaambizana ukweli "WE ARE SUCH LOOSERS!"

HITIMISHO.
Mwl.Nyerere aliwahi kusema kutokana na mamlaka makubwa aliyopewa na katiba kama raisi angeweza kua dikteta kama angetaka.Mzee huyu aliona hatari iliyopo kama nchi haitopata kiongozi mwenye busara hivyo mjadala wa katiba mpya uliokwama unahitajika kuhuishwa.

Kiufupi siasa ni dubwasha la ajabu(complex) sana,bahati mbaya katika nchi zetu limedogoshwa na kurahisishwa sana kwamba mtu yeyote mjanja mjanja, mwenye fedha au mwenye elimu(bookish education) na malundo ya vyeti anaweza kuifanya.Lakini ukweli si kila mtu anaweza kufanya siasa(sio uchwara)kwa umahiri.Kunahitajika mtu aliyezama na kujielimisha kwenye mambo mengi ya kiuchumi na kijamii,fikra pevu,busara zisizo na kipimo,dhamira njema na uwezo mkubwa wa kusikiliza na kuunganisha watu.

Hata ukipewa madaraka makubwa kiasi gani kukiwa na upungufu mkubwa wa haya mambo utabaki tu kama mtu yeyote wenye uchungu wa kubadili muelekeo au hali ya jamii na wala usifanikiwe lolote.

TUTAFAKARI NA TUJILIMISHE.

VERDICT AS WE STAND;

WANANCHI WA KAWAIDA-jury still out

VYAMA VYA UPINZANI-WINNING(they still get to earn it )

CCM-LOOSERS (big time)
 
Kwa kipindi tukiwa tunaelekea uchaguzi mkuu wa mwaka jana tulikua na mjadala mkubwa wa aina gani ya kiongozi(rais)anatufaa hasa kutokana na mwenendo wa hovyo wa muongo mmoja wa uongozi wa JK uliokua unaishia ambao uliacha kila mtu mwenye nafasi ajifanyie na kujitwalia chochote anachotaka kana kwamba serikali haipo.Watu kadhaa walipiga kelele kwamba serikali haitimizi wajibu wake wa na baadhi wakaweka rekodi sahihi kabisa kwa kusema "rais ni dhaifu" hivyo tulipaswa kupata raisi jasiri asiyesita kufanya maamuzi sahihi bila kuonea haya mtu.
Labda katika hali ya kukata tamaa wapo pia baadhi ya wananchi walienda mbali zaidi na kusema tunahitaji raisi mwenye "UDIKTETA KIDOGO" kurudisha taasisi na watumishi wa umma kwenye msitari ulionyooka.
Andiko langu litajaribu kuibua mjadala wa wazi kwa kuzingatia tamthini fupi ya kijumla ya uongozi wa awamu ya tano ndani ya takribani miezi saba tangu kuingia madarakani.

Kwanza tuyatambue makundi ya watu/wananchi na matarajio yao kuhusu matokea ya uchaguzi na nini yalikua matamanio/matarajio yao na serikali ya awamu ya tano;

WANANCHI WA KAWAIDA
Hawa ni wananchi huru (free from strong political affiliation) ambao kwa kiasi kikubwa ndio walikua wahanga wakubwa wa mambo ya hovyo kwenye serikali iliyopita.Ni kundi kubwa ambalo japokua kwa kiasi walikua wanaunga mkono vyama fulani lakini hawakua na maslahi binafsi na ya moja kwa moja katika vyama vya siasa wala msukumo wa kiitikadi(vyama vyote havina msingi wazI wa kiitikadi),hivyo matarajio yao makubwa yalikua ni uimarishwaji wa huduma za kijamii na kupungua kwa ugumu wa maisha.Hawa ndio ambao kwa miaka yote hamsini ya uhuru wanaguswa moja kwa moja na kila tatizo hata yale ya aibu(kulingana na umri wa taifa letu),watoto wao kukosa madawati,ukosefu wa madawa ya msingi,ubovu wa miundo mbinu,ukosefu wa maji safi na salama,ughali wa gharama za maisha n.k kiufupi hili ndio lile kundi linaloishi "KAMA MASHETANI".

WALICHOPATA.
Kwanza niweke wazi kwamba kwa asilimia kubwa hili ni kundi na watu wasio na information za kutosha na kwa kiasi kikubwa hawana muda na vitu venye kufikirisha sana.Maelezo pekee ya hali hii inaweza kukosa uelewa/upeo (si kwa matusi) au wanazongwa zaidi na kupambana na ugumu wa maisha hivyo hawana luxury ya kuumiza kichwa kwenye mambo wanayoona hayawagusi moja kwa moja.
Hili ndio kundi mpaka sasa lililoridhika zaidI kati ya makundi yote kwani kwa kawaida huguswa sana na matamko na maamuzi popular na kwa bahati nzuri serikali ya awamu ya tano si hapa kwa mambo hayo . Matukio kama kushughulikiwa kwa watuhumiwa wa ufisadi,wakwepa kodi,watumishi wazembe,sera ya elimu bure ya msingi n.k yamewapa imani kubwa na wananchi wa kundi hili.Ni nadra sana kukuta kundi hili likijikita kwenye tathmini ya kina ya tija na athari za maamuzi ya serikali kwenye vitu kama sera,mwenendo wa bajeti mpya,uhuru wa mihimili ya serikali,uhuru wa vyombo vya habari,mipango ya kupunguza ukosefu wa ajira,sera na sheria za kodi,masuala ya hifadhi ya jamii badala yake huridhika kirahisi na vitu vinavyoshikika.
Pamoja na hayo ukweli ni kwamba, katika siasa za nchi maskini kama yetu huwezi kudharau matakwa ya kundi hili kwani kwa bahati mbaya ndio kundi kubwa zaidi(kutokana na uwekezaji mdogo kwenye sekta ya elimu) hivyo ndio mtaji mkubwa wa wapiga kura.Vilevile vitu vinavyotarajiwa na kundi hili kama uboreshaji wa huduma za jamii na miundo mbinu ndio msingi mkuu wa serikali zetu.Jambo la msingi hapa ni kule kukosekana kwa uelewa kwamba vile vitu vinavyozungumzwa sana na makundi mengine ndio hasa hupelekea upatikanaji wa haya mambo yanayotazamwa kama mambo muhimu zaidi na kundi hili.

VYAMA VYA UPINZANI
Hili ni kundi linajumuisha vyama vya siasa kama taasisi,wapenzi na wanachama 'kindakindaki' na viongozi wao.Ni watu waliokua wanalalamikia sana (most vocal)mwenendo wa hovyo wa serikali ya awamu ya nne hasa katika eneo la ubadhirifu wa mali za umma na kukosekana kwa mipango na nia thabiti ya kuondoa umaskini nchini.Kwa kipindi chote walikua mstari wa mbele kuonyesha udhaifu wa serikali na kuibua kashfa nyingi za ufisadi kama EPA,RICHMOND,ESROW na ubadhirifu mkubwa kwenye miradi ya maendeleo na serikali za mitaa.Kutokana na haya yote na kukosekana kwa hatua thabiti kutoka kwa serikali hasa rais wakajumuisha kwa kumpa lebo(anayostahili) ya "rais dhaifu".

WALICHOPATA.
Mwanzoni mwa utawala wa serikali ya raisi Magufuli vyama vya upinzani vilionekana kupata changamoto kubwa.Hii ilitokana na mtindo wa utendaji kazi wa raisi kwenye kushughulikia kwa haraka kasoro nyingi serikalini ambazo kwa kipindi kirefu zilikua ndio msingi mkubwa wa hoja za ushawishi wa upinzani.Huku akichagizwa na kauli yake aliyoirudia mara kwa mara kwamba yeye ni rais wa wanyonge. Ilionekana wazi vyama vya upinzani vilitakiwa vijipange upya kimkakati kama vilitaka vibaki na ushawishi kwa watanzania wa kawaida ambao walianza kumuona raisi Magufuli kama mwokozi wao.Hatua yoyote ya kumkosoa raisi ilionekana kama ni "political suicide" huku proganda kubwa ikipigwa kwamba wanaomkosoa au kumpinga rais kwa baadhi ya hatua zake hasa kutoheshimu utawala wa sheria na kuingilia mihimili mingine basi ni mafisadi au watetezi wa mafisadi.Wapinzani waliandamwa kwa kile kilichoonekana ni unafki kwani raisi aliyepita walidai DHAIFU huyu wa sasa anatenda kwa haraka wanamuita DIKTETA.Swali dogo la kujiuliza hapa tangu lini tofauti ya UDHAIFU ikawa ni UDIKTETA?
Lakini kama ilivyo kawaida siku zote muda hauongopi kwani baada ya hatua za mwanzo ambazo kwa kiasi kikubwa zilikua nzuri na popular uzito wa nafasi ya urais na udhaifu wa busara za kiuongozi ukaanza kua wazi. Serikali ikaanza kuonyesha wazi dhamira ya kukamata mihimili mingine hasa bunge na sasa ilionekana wazi nchi inaanza kuendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja.Kukaanza kuwepo maamuzi mengi yasiyotumia busara kama la wanafunzi wa UDOM,matamshi ya kukurupuka yasiyoendana na uzito wa nafasI ya urais na zaidi kushindwa kuhimili ukosoaji na kuzuia shunguli za vyama vya upinzani.Haya yote yakageuka ni 'blessing in disguise' kwa wapinzani kwani wamepata mifano hai ya kuonyesha elements za kidikteta za utawala wa awamu ya tano.
Hii kwa upande wa serikali na CCM imekua ni moja ya textbook definition ya political blunder.Kwahiyo kiujumla wapinzani wamepoteza kiasi hasa kwenye ule uhuru wa kufanya shughuli zao za kisiasa na ile nafasi ya kuvumbua kasoro za kifisadi ambazo kisiasa zilikuwa zina uwezo wa kugusa wananchi kirahisi lakini kwa upande mwingine wamepata changamoto ya kuvihulisha vyama vyao na kua na agenda nzito za kisera huku zikiipa presha serikali ambayo imeonyesha ina udhaifu mkubwa wa kuhimili pressure za kisiasa na mikakati ya kisera kumaliza changamoto za kimaisha za wananchi ikiwekeza zaidi kwenye kufanya maamuzi ya kufurahisha macho na masikio ya wananchi.

CHAMA CHA MAPINDUZI
Kwa muktadha wa hapa simaanishi wanachama bali wenye chama chao hasa.Maana siku zote nimekuwa nikiwa na msimamo kwamba inahitajika uwendawazimu kiasi kwa mwananchi wa kawaida,maskini asiye na manufaa ya mojakwamoja kujinasibisha kwamba yeye ni mwana CCM.....Kama wasemavyo (CCM ina wenyewe).Hili ni kundi dogo la viongozi serikalini na katika chama ambao kwa muda wote wamekua wanufaika wakubwa wa uozo wa serikali zilizopita.Ndio ambao wakati vyama vya upinzani,wananchi na asasi za kiraia zikipiga kelele kwamba nchi imegeuka shamba la bibi walikua wakibeza na kusifu kwamba MAMBO YAKO SAWA KABISA,ACHA TUMEZOEA KELELE ZAO,SISI TUNASONGA MBELE!.

WALICHOPATA
Usishangae wale watu waliokua wakipinga bandarini na taasisi zingine hakuna wizi huku wakibeza wananchi,asasi za kiraia na viongozi wa vyama vya upinzani kwamba wanajifanya wana habari za ndani za usamalama wa taifa wameenda wapi?bado wamo serikalini na ndani ya chama na leo ndio wapiga zumari wakubwa kwamba huyu ndio rais sasa,hajawahi kutokea baada ya Mwl.Nyerere na hapaswi kukosolewa ni msafi kama theluji kifupi ni malaika.Kwao umahiri wa unafiki ndio mtaji kwani in petty politics there is no nobility to be on loosing side.Wanajipiga kifua kwamba wamepata walichotaka kana kwamba hakuna mtu anayefahamu kwamba Rais wa sasa ni zao la msuguano ndani ya chama na wala si mpango maalumu wa chama.Ukweli unabaki kwamba kwa kiasi kikubwa wamepoteza vingi kwani walizoea kuishi kwa kupiga 'deal' na sasa wamepoteza hata ule ushawishi ndani ya serikali na chama kwakua bwana mkubwa kwa hulka yake ya kujua kila kitu amewabakiza kama picha tu. Kitu pekee kinachowapa nguvu ni ule umahiri wao wa kuifanya kila hali kua na manufaa kwao(angalau hadharani) lakini habari njema ni kwamba wakikaa wao kwa wao wanaambizana ukweli "WE ARE SUCH LOOSERS!"

HITIMISHO.
Mwl.Nyerere aliwahi kusema kutokana na mamlaka makubwa aliyopewa na katiba kama raisi angeweza kua dikteta kama angetaka.Mzee huyu aliona hatari iliyopo kama nchi haitopata kiongozi mwenye busara hivyo mjadala wa katiba mpya uliokwama unahitajika kuhuishwa.
Kiufupi siasa ni dubwasha la ajabu(complex) sana,bahati mbaya katika nchi zetu limedogoshwa na kurahisishwa sana kwamba mtu yeyote mjanja mjanja, mwenye fedha au mwenye elimu(bookish education) na malundo ya vyeti anaweza kuifanya.Lakini ukweli si kila mtu anaweza kufanya siasa(sio uchwara)kwa umahiri.Kunahitajika mtu aliyezama na kujielimisha kwenye mambo mengi ya kiuchumi na kijamii,fikra pevu,busara zisizo na kipimo,dhamira njema na uwezo mkubwa wa kusikiliza na kuunganisha watu.Hata ukipewa madaraka makubwa kiasi gani kukiwa na upungufu mkubwa wa haya mambo utabaki tu kama mtu yeyote wenye uchungu wa kubadili muelekeo au hali ya jamii na wala usifanikiwe lolote.
TUTAFAKARI NA TUJILIMISHE.
Hivi Kinana ameishia wapi? Juzi nilimuona anakubali kuwa people have to speak their mind!
 
Back
Top Bottom