Chama hakifanyi kazi kama banda la wauza miwa.
Uongozi hufanya kazi kwa mujibu wa taratibu na kanuni.
Zitto amepewa tuhuma zake kwa mujibu wa taratibu hizo hizo
Amezijibu kama anavyodai, tusubiri sasa hatua itakayofuata.
Zitto hajakatazwa kutembelea waliompa kura. Na hakuna kiongozi wa Chadema atakayemkataza kufanya hivyo. Kwanza katiba haimzuii Zittop kufanya anachofanya. Wanaosema Zitto anafanya makosa wanazo sababu nyingine. Ngoja nikusaidie baadhi ya hizo sababu
1. Ziara za Zitto zinaratibiwa kwa ukaribu sana na vijana waliofukuzwa Chadema na kuhamia CCM
2. Ziara za Zitto zina malengo ya kuwauzia mgogoro wake binafsi watu wa kigoma. Kwamba ionekane kuwa Zitto ameadhibiwa kutokana na Ukigoma wake na sio UHUNI wake.
3. Ziara za Zitto sio za kujenga Chama. Ukiacha Kigoma kaskazini kwa wapigakura wake, Zitto "ameandaliwa" ziara za Kasulu na wilaya zingine za kigoma ambapo Slaa alipita siku za karibuni. Hatujengi chama kwa staili hiyo.
4...
5....
....
Mkuu, haki ipi na usawa upi unaoutaka? Haki ipi Zitto ameikosa? Zitto ameteuliwa kuwa mlezi wa kanda ya Magharibi, Alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Amekuwa Naibu Kiongozi wa kambi ya Upinzani, Amekuwa Waziri kivuli wa fedha. Zitto alifukuzwa na Samwel Sitta Bungeni bunge lililopita, Chama kilimbeba, kilizunguka nae, kilifanya nae mikutano nk. Zitto alisitisha uteuzi wa wagombea ubunge wa Chadema kwenye jimbo la Pinda kisirisiri tena akiwa peke yake bila kushauriana na viongozi wenzake. Chama kilimheshimu kama naibu katibu mkuu ingawa hakufata utaratibu na ilikuwa kinyume cha kanuni kama kiongozi. Hatukuona ukisifia busara za Chama nyakati zote hizo. Ila Zitto na wahuni wenzie kuandaa mkakati wa kukiua chama kwa kufanya mapinduzi ndio unalilia usawa na haki? Acha unafiq wewe