Hapa CHADEMA Mlichemka Na iwe FUNDISHO baadae

Hapa CHADEMA Mlichemka Na iwe FUNDISHO baadae

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
1,487
Reaction score
913
Kwa miaka mitatu Na nusu amekuwa Kwenye kamera Za Chama, mkimchunguza Na ku-pile ushahidi wa kutosha Kwamba this is a bitting snake!!, then mnamwita circle Na kumwondolea magamba ambapo everybody realize this is a true snake..hiyo Bado haitoshi mnafanya makosa ya Karne ya kumsihi ati ajitetee kwanini asinyukwe kichwa ilihali keshajua wote mmeshauona unyoka wake mnadhani atafanyaje..?! Ndo hiki tunachokushuhudia Leo!

Ni somo la kujifunza namna nzuri ya kuwatendae majoka, Kama sio kuwagonga vichwa Na MCHEZO kwisha Basi itafutwe njia nyingine, mwalimu Nyerere aliwaleta very closer majoka Na kuwafrustrate vibaya..

Mambo ya kutimuana uanachama ni utoto Na woga, ukimtimua uanachama yapo mafisi flan kutoka chama la Majambazi wako tayari watoe mihela yao kufadhili mbio Za mliyemtimua anye-anye Na kuharisha all corner of the country party. Mtaacha kujenga Chama Na kuhangaikia kinyesi Cha mjinga mmoja. Makamo ya Chama Kwa Sasa lazima wawe Na mastermind zilizo tulia kusolve such problem sio kutegemea vikao.

Unaweza kuchukua au ukaacha..
 
Nakuunga mkono!!Chadema wangechukua uamuzi mgumu kungali bado mapema!!leo tungekuwa tunaongelea habari zingine na si za huyu mnafiki
 
Kama sielewi hivi!!

Unamaanisha "wangemfuta" kabisa!!?
 
siku bado zipo lakini mwisho wa siku watajua kuwa zitto ni jembe.
 
siku bado zipo lakini mwisho wa siku watajua kuwa zitto ni jembe.

ImageUploadedByJamiiForums1387780108.099981.jpg
 
siku bado zipo lakini mwisho wa siku watajua kuwa zitto ni jembe.
.
Matumizi makubwa ya Jembe ni Kwa shughuli Za kilimo, yamkini jembe halo Hilo hutumika kuchimbia makaburi Sijui Kama unafaham hicho my friend. Usipoelewa hapa hutaelewa Daima..
 
Chadema hakifugi wahuni...

kamanda, mie pia ni mwanaCDM na bado nitaendelea kuwa hivyo pamoja na kwamba naona uongozi wetu wa chama umetuangusha ktk sakata la zito.
bila unafki uongozi hauna consisteny kabisa ktk jambo hili.
- chama hakijawahi kutoa ushahidi na vielelezo vya usaliti wa akina zito.
- dr slaa aliwahi kukaririwa kufunga mjadala huu - hii ilibaki kuwa kauli rasmi ya chama.
- dr slaa, mbowe na hata lema wamesikika majukwaani wakimnanga zito.

*baadae zito nae anaanza ziara mkoani kigoma lakini kwa upande wake inaonekana ni makosa.

sasa wengine tulio huru tunahoji - kwa nn hakuna haki na usawa ndani ya chama?!
kwa nn tusifikiri kwamba kwa mtiririko huu zito anahujumiwa ndani ya chama - haswa kwa kuwa dr slaa kama katibu mkuu wa chama jana amesikika akimhukumu as if mawazo yake ni sawa na ya wajumbe wote wa cc.
 
kamanda, mie pia ni mwanaCDM na bado nitaendelea kuwa hivyo pamoja na kwamba naona uongozi wetu wa chama umetuangusha ktk sakata la zito.
Chama hakifanyi kazi kama banda la wauza miwa.
Uongozi hufanya kazi kwa mujibu wa taratibu na kanuni.
Zitto amepewa tuhuma zake kwa mujibu wa taratibu hizo hizo
Amezijibu kama anavyodai, tusubiri sasa hatua itakayofuata.
Nilidhani ungekuwa na malalamiko kwa Zitto kuwa pamoja na taratibu zilizowekwa, bado Zitto anaongoza makundi ya wahuni kufanya fitna.
bila unafki uongozi hauna consisteny kabisa ktk jambo hili.
Consistency unayoitaka ni ipi mkuu gastone? Ngoja nikukumbushe..
1. Chama kilinasa waraka wa mapinduzi haramu
2. Kikachunguza
3. Katika VIKAO HALALI wahusika wa mapinduzi waliitwa, wakahojiwa, wakakiri, wakaomba kujiuzuru nafasi zao
4. Kikao kikaamua wavuliwe nyadhifa zao wabaki kuwa wanachama na wajieleze kwa nini wasivuliwe uanachama
5. Inasubiriwa wakae waamue baada ya utetezi wao kufika chamani.
Unaitaka Consistency ipi mkuu?
- chama hakijawahi kutoa ushahidi na vielelezo vya usaliti wa akina zito.
Ungesema hivi, kwako wewe, waraka wa mkakati wa mabadiliko sio ushahidi tosha wa usaliti wa akina Zitto ningeheshimu maoni yako. Lakini kusema chama hakijatoa ushahidi wa usaliti wa Zitto ni matusi kwa Chama, ni kejeli kwa viongozi wa chama na ni dharau kwa wafuasi wenye nidhamu kwa chama. Unataka ushahidi upi zaidi ya huo mkakati wa kufanya mapinduzi ya uongozi wa Chama?
- dr slaa aliwahi kukaririwa kufunga mjadala huu - hii ilibaki kuwa kauli rasmi ya chama.
Ilitegemewa kuwa Team ya wafuasi wa Zitto wangeheshimu kauli hii ya katibu mkuu. Lakini pia hata Zitto mwenyewe tulitegemea angekuwa mfano kwa wafuasi wake kuheshimu kauli ya katibu mkuu. Lakini nadhani na wewe unaona wanavyofanya Zitto na team yake..Kosa sio kauli ya Slaa, Kosa ni matendo na response za team ya Zitto na Zitto mwenyewe.
- dr slaa, mbowe na hata lema wamesikika majukwaani wakimnanga zito.
Huu ni uongo. Ni ishara ya kutojiamini. Baada ya Zitto kuvuliwa nyadhfa zake, hakuna hata mmoja aliyemnanga Zitto. Labda useme kunanga ni kufanyaje lakini wao kama viongozi walikuwa wakitoa ufafanuzi wa nini kilitokea kwenye kamati kuu. Hakuna mahala Zitto amelalamika kunangwa na hao viongozi. Sasa kama Zitto mwenyewe hajalalamika wewe umeona wapi Zitto akinangwa?

baadae zito nae anaanza ziara mkoani kigoma lakini kwa upande wake inaonekana ni makosa.
Zitto hajakatazwa kutembelea waliompa kura. Na hakuna kiongozi wa Chadema atakayemkataza kufanya hivyo. Kwanza katiba haimzuii Zittop kufanya anachofanya. Wanaosema Zitto anafanya makosa wanazo sababu nyingine. Ngoja nikusaidie baadhi ya hizo sababu
1. Ziara za Zitto zinaratibiwa kwa ukaribu sana na vijana waliofukuzwa Chadema na kuhamia CCM
2. Ziara za Zitto zina malengo ya kuwauzia mgogoro wake binafsi watu wa kigoma. Kwamba ionekane kuwa Zitto ameadhibiwa kutokana na Ukigoma wake na sio UHUNI wake.
3. Ziara za Zitto sio za kujenga Chama. Ukiacha Kigoma kaskazini kwa wapigakura wake, Zitto "ameandaliwa" ziara za Kasulu na wilaya zingine za kigoma ambapo Slaa alipita siku za karibuni. Hatujengi chama kwa staili hiyo.
4...
5....
....

sasa wengine tulio huru tunahoji - kwa nn hakuna haki na usawa ndani ya chama?!

Mkuu, haki ipi na usawa upi unaoutaka? Haki ipi Zitto ameikosa? Zitto ameteuliwa kuwa mlezi wa kanda ya Magharibi, Alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Amekuwa Naibu Kiongozi wa kambi ya Upinzani, Amekuwa Waziri kivuli wa fedha. Zitto alifukuzwa na Samwel Sitta Bungeni bunge lililopita, Chama kilimbeba, kilizunguka nae, kilifanya nae mikutano nk. Zitto alisitisha uteuzi wa wagombea ubunge wa Chadema kwenye jimbo la Pinda kisirisiri tena akiwa peke yake bila kushauriana na viongozi wenzake. Chama kilimheshimu kama naibu katibu mkuu ingawa hakufata utaratibu na ilikuwa kinyume cha kanuni kama kiongozi. Hatukuona ukisifia busara za Chama nyakati zote hizo. Ila Zitto na wahuni wenzie kuandaa mkakati wa kukiua chama kwa kufanya mapinduzi ndio unalilia usawa na haki? Acha unafiq wewe
kwa nn tusifikiri kwamba kwa mtiririko huu zito anahujumiwa ndani ya chama - haswa kwa kuwa dr slaa kama katibu mkuu wa chama jana amesikika akimhukumu as if mawazo yake ni sawa na ya wajumbe wote wa cc.
Zitto akikihujumu chama wewe unasema ni haki na usawa. Tuliowapa haki ya kutazama chama wanapofanya kazi yao unakuja na hoja za Zitto Kuhujumiwa.
Nikuulize, Zitto anahujumiwa ili iweje?
Ni faida gani Chama kitapata kikimhujumu Zitto?
Ni lini Chama kilianza kumhujumu zitto?
Na unayaona matendo ya Zitto kwenye chama ni sawasawa?
Jana Slaa ameonya, kuwa timu inayomshauri Zitto haimsaidii. Itasababishwa Zitto afukuzwe. Wewe unaona mchezo wa ile timu ni sawasawa ila kauli ya Slaa ni ya kumhujumu Zitto?
 
"3. Ziara za Zitto sio za kujenga Chama. Ukiacha Kigoma kaskazini kwa wapigakura wake, Zitto "ameandaliwa" ziara za Kasulu na wilaya zingine za kigoma ambapo Slaa alipita siku za karibuni. Hatujengi chama kwa staili hiyo.
4..."

Ameandaliwa ziara hizo na maccm, ambao wanashangilia kama nini!!! Wasichokijua ni kwamba wanafacilitate ZZK kufukuzwa uanachama. Sijui kama watampokea?
 
zitto ni kiboko ya wanafiki kwani zile siku 14 hazijafika tu wajamani

Chama kina taratibu zake,kupeleka ushahidi si laziwa hukumu itolewe siku hiyo! siku 14 zilikuwa ni kwa ajili ya yeye na wahuni wenzie kupeleka ushahidi wao na si muda wa CC kukaa na kutoa maamuzi.kama hutanielewa basi utakuwa na boga badala ya kichwa!
 
sisi hatulii ila tutaheshimu maamuzi ya viongozi wetu ila na wao kama wakweli mbona mpaka leo kimya kunanini nyuma ya pazia

au ndio kweli kutimua zitto sawa na kugawa chama
 
chadema chama kisicho na miiko kila mtu na mambo yake ulaghai ndiyo slaha ya chama.
 
.
Matumizi makubwa ya Jembe ni Kwa shughuli Za kilimo, yamkini jembe halo Hilo hutumika kuchimbia makaburi Sijui Kama unafaham hicho my friend. Usipoelewa hapa hutaelewa Daima..

tufahamiane kwanza wewe upo chadema ipi kwanza.
 
kuhusu huyo zitto mfukuzeni tu haina haja ya kumtungia uongo kwenye mitandao. kwani kamati kuu si yenu, hata mkimfukuza hamna wa kuwahoji.
na kwa bahati mbaya kabisa kumbe na nyinyi ni wachumia tumbo tu kama haya maccm a.k.a chama cha majizi.
eti mnatetea wanyonge! wanyoge wawapi wanafiki wakubwa nyie.

Back
Top Bottom