Hamza Hassani Juma: Waziri Mbwatukaji Ovyo Wa SMZ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamza Hassani Juma: Waziri Mbwatukaji Ovyo Wa SMZ!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Aug 23, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  salim said salim, zanzibar
  NI kawaida katika nchi nyingi kusikia taasisi za ndani na nje zinafanya utafiti wa masuala ya siasa, uchumi, utamaduni, michezo na burdani na kutoa matokeo.
  Zanzibar imeshuhudia taasisi za nje ya visiwa hivi hasa ya REDET iliyopo Dar es Salaam zikitoa matokeo ya tafiti zao ambazo watu huzishitukia tu.
  Lini tafiti hizo zilifanywa, nani alizifanya, wapi utafiti ulifanyika na vigezo viliotumika huwa hayawekwi wazi.
  Vile vile, REDET huleta Zanzibar wale inaowaita wataalamu wa masuala ya demokrasia ambao hutoa elimu ya demokrasia wakati hawaelewi undani wa siasa za Zanzibar, zilizogubikwa na uongo, unafiki, uzandiki, chuki na ubaguzi.
  Karibu taarifa zote za REDET, hasa uchaguzi mkuu unapokaribia, huonyesha CCM ni nambari wani na kuwa na muelekeo wa kupata ushindi. Hata wakati mmoja Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) haijawahi kulalamikia ripoti za REDET, labda kwa sababu ripoti zake zote huzipigia debe.
  Ninakumbuka wakati wa kuelekea uchaguzi mdogo kisiwani Pemba mwaka 2001, taasisi moja ilisema mchuano ungekuwa mkali. SMZ haikulalamika kwamba utafiti ule ulikuwa si wa kitaalamu na haukuonyesha hali halisi iliokuwepo wakati ule.
  Uchaguzi ulifanyika na CCM ilipata chini ya asilimia 12 katika majimbo yote isipokuwa Mkanyageni. Sijui wataalamu wale wa utafiti waliotoa kauli ya kutegemea ushindani mkali katika uchaguzi ule walipata wapi dalili za kuwepo hali ile.
  Hivi karibuni taasisi moja ijuliknayo kama Steadman ilisema utafiti wake juu ya mbio za urais wa Zanzibar mwaka 2010 unaonyesha katika orodha ya wanaotajwa kutaka kugombea anayeongoza ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alitajwa kuwapiku wale wa CCM.
  Sijui vipi Steadman ilifikia hitimisho hili wala sielewi njia ilizotumia kuendesha huo utafiti au lengo la kufanya hivyo. Sikua na taarifa ya kufanyika utafiti huo, licha ya udogo wa Zanzibar, kama REDET walipofanya (kama walifanya) utafiti wa aina hii siku za nyuma.
  Kinachonishangaza ni kuwa SMZ haikulalamikia matokeo ya tafiti za REDET kwa vile yaliisafishia njia kwa CCM. Wapinzani walidai REDET ilikuwa inajenga mazingira ya kuhalalisha wizi wa kura katika chaguzi ziliopita. Ukweli au uongo wa madai hayani suala linalohitaji utafiti usiokuwa na utashi wa kisiasa.
  Tunaambiwa kitendo cha Steadman si cha kiungwana kwa vile kibali ilichopewa na SMZ si cha kushughulikia mambo ya siasa. Waziri wa Nchi katika Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, alieleza kuwa kilichofanywa na Steadman ni utapeli.
  Hapa pamejitokeza hisia kuwa ni taasisi za kiungwana kama za REDET tu ndiyo zenye haki ya kufanya tafiti juu ya chaguzi za Zanzibar kwa vile ni safi na watafiti wake ni waungwana. Wengine huwa hawana nia njema na Zanzibar.
  Waziri Hamza alisema hata Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Juma Duni Haji, huenda angetaka kuwa mgombea, lakini Steadman haikumjumuisha katika orodha ya wanaosemekana wanataka kugombea Urais. Labda hapa waziri angelisema haelewi kwa nini na yeye hajaingizwa katika orodha hiyo kama alivyotaka aingizwe Duni.
  Lakini la kujiuliza hapa ni je kwa waziri Hamza kumsemea Duni juu ya mbio za kuelekea urais wa Zanzibar na kumfikilia anataka kugombea wakati mwenyewe hajawahi kusema hivyo ni uungwana? Au uungwana hutarajia kitoka upane mmoja tu?
  Ni vizuri kwa viongozi wa SMZ kuwa na uvumilivu na si kutaka kila taasisi itoe matokeo yatakayowafurahisha. Hii ndiyo dunia ya leoÂ…huyu anasema hili na yule anasema lile. SMZ pia haikupaswa kulalamikia kauli ya nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na nchi nyingine za Ulaya na Marekani, juu ya kutofurahishwa na namna zoezi la uandikishaji wapiga kura linavyoendeshwa kisiwani Pemba.
  Kwanza tukumbuke kuwa ni nchi hizi ndio zinazotusaidia kufanya huo uchaguzi na kwa hivyo zina haki ya kutaka kuuona ni huru na wa haki na sio fedha zao kutumika kukandamiza demokrasia.
  Kama kweli Tanzania, na hasa Zanzibar, inahisi hakuna anayeweza kuinyooshea kidole basi Tanzania nayo isingelinyooshea kidole nchi nyingine wala kupeleka majeshi yake Comoro, Darfur, Sudan na nchi nyingine. Au tunataka tuamini kuwa nchi hizi ni sehemu ya Tanzanika na kwa hivyo tulikuwa hatuingilii mambo ya nchi nyingine?
  Vile vile tujiulize kwa nini waliofanya mauaji ya haliki Rwanda wanashitakiwa Arusha? Je, kwa mtazamo wa kila mtu ashughulikie nchi yake si kuingilia mamo ya ndani ya Wanyarwanda?
  Ni vizuri tukaanza kuyaangalia mambo kwa sura moja au mbili, lakini zaidi ya hizo. Wakati tukifurahia wanaotupigia debe na kutusifu tusinune wanapotokea wale wanaofanya kinyume na hayo. Tuwe wavumilivu, iwe tunapokosolewa au hata kuwekwa hadharani mambo ambayo hatupendi yawe wazi.
  Vile vile tusiwe mahodari kuwaita wachochezi wale wanaotaka watu wajiandikishe kupiga na kuwasifia kama malaika, masheha wanaowanyima watu haki hio au watu wanaopiga watu mapanga na nondo kwenye vituo vya uchaguzi. Tusisahau kuwa pakiwa na wanaokupenda pia wapo wanaokuchukia, iwe kwa sababu za msingi au kwa chuki zao binafsi. Dunia ya sasa si rahisi kuibadili ili ikuridhie unavyotaka wewe kila wakati na kwa kila jambo.


  SOURCE: TANZANIA DAIMA.
   
  Last edited: Aug 23, 2009
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Bado sijuwi nani msemaji wa SMZ, kila jambo namsikia Hamza na "Mzee wa Donge" kimya, au amefulia???
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na Jabir Idrissa
  NI Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, aliyesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaimarisha ulinzi kwenye vituo vya uandikishaji wapiga kura kwa kutumia vikosi vyake vya ulinzi vikisaidiana na Jeshi la Polisi.
  Hamza, mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kwamtipura, mjini Unguja, alitaja vikosi vikiwemo vya SMZ kwamba vitaongeza nguvu pale Polisi ilipoonyesha udhaifu kuhakikisha ulinzi na usalama kwenye vituo vya uandikishaji.
  Hakusita kutoa kauli ambayo bado naichukulia ni ya kejeli kwa wananchi. Kwamba wananchi wasishangae wakiona zana za kijeshi kama vile vifaru zikipita mitaani kwani ni moja ya hatua za serikali kutekeleza azma hiyo ya kusimamia ulinzi kwenye vituo.
  Si uongo. Siku mbili tu wananchi walishuhudia barabarani vifaru na magari yaliyobeba silaha za kijeshi zikipelekwa mjini Wete ambako uandikishaji wapiga kura ulilazimika kusitishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wiki mbili zilizopita baada ya wananchi wa Ole kugoma kuandikishwa.
  Sasa nimfahamishe Hamza kwamba maelezo yake, yaliyoambatana na kejeli kwa wananchi, si lolote bali ni maonyesho ya vitisho na misuli isiyo sababu kwa wananchi.
  Alichokifanya ni muendelezo unaothibitisha kile ninachoamini kwamba uandikishaji wapiga kura watakaoingizwa katika Daftari la Kudumu la Wapira Kura (DKWK) la Zanzibar ambao ni zoezi la kiraia, umekuwa ukiendeshwa na kusimamiwa kijeshi.
  Ni vizuri Hamza na wenzake katika SMZ na Chama cha Mapinduzi (CCM), wakaelewa serikali wanayoongoza imeshtadi hulka za kidikteta. Wanataka wafanye na kuonyesha nini tena hata dunia iamini kuwa serikali inayoongoza Zanzibar inashikwa na wanaoamini katika uongozi wa mabavu?
  Hivi waziri wa serikali anapojitapa kuwa vifaru vitatumika kulinda vituo vya uandikishaji wapiga kura ndio anaonyesha nini kwa watu? Kutamba kutumia vifaru katika zoezi la kiraia ambalo wananchi hawabebi hata fimbo, hakujatosha tu kuonyesha namna SMZ inavyoendesha mambo kihuni? Huko si kuua mbu kwa kutumia mzinga? Na huo si ndio uongozi wa kiimla?

  Kuongoza serikali ni utaratibu wa kisiasa usiotaka silaha. Kauli nzuri, nia njema na heshima juu ya haki na utu wa wale unaowaongoza hakika vinatosha. Siasa ni mipango endelevu ya kustawisha jamii. Ajabu Hamza hajawahi kusikia vilio vya wananchi kutaka uchaguzi usimamiwe na Umoja wa Mataifa. Vilio hivi vimesikika Zanzibar mara kadhaa, baada ya kuthibitika serikali ya CCM haitaki demorasia ya kweli.
  Upo ushahidi wa kutosha kuwa SMZ siyo tu haijapata kuendesha uchaguzi huru, wa haki na ulio wazi, bali pia imeshindwa kuonyesha inao uwezo wa kufanya hivyo katika uchaguzi uliokwishafanyika tangu mfumo wa vyama vingi uliporudishwa mwaka 1992.
  Inajulikana wazi kwamba ukiacha uchaguzi wa 1995 uliofanyika vizuri katika hatua za mwanzo – baadaye ukavurugwa katika ujumuishaji kero na utangazaji matokeo – uliofuata wote ulikuwa uchafuzi. Popote pale ulipofanyika uchaguzi na matokeo yake kutangazwa chini ya mtutu wa bunduki, hapakuwa na uchaguzi huru na wa haki.
  Uchaguzi huru, wa haki na ulio wazi huendeshwa kwa kusimamia misingi ya demokrasia na utawala bora. Hata siku moja huwezi kujinasibu umefanya uchaguzi huru, wa haki na ulio wazi wakati uandikishaji, upigaji kura, uhesabuji na ujumlishaji wa kura pamoja na utangazaji matokeo ya kura, vimefanyika chini ya matumizi ya nguvu, hila na usiri mkubwa.
  Kadhalika, huwezi kutamba umefanya uchaguzi safi wakati serikali ilithubutu kufyatulia wananchi risasi za mipira na zile za moto kutokomeza wapiga kura kwenye vituo na mitaani na kupora visanduku vya kura mikononi mwa waliostahili kuvilinda.
  Bali pia huwezi kutamka umepata kuendesha uchaguzi safi wakati hadi leo watu hawajasahau madonda ya kuuawa kwa ndugu zao wakati wa uandikishaji wapiga kura na baada ya matokeo kutangazwa.
  Kama SMZ imeshindwa kuendesha uchaguzi mzuri kwa vigezo vya kimataifa, hata vile ambavyo ZEC iliridhia na kusaini kama "Maadili ya Uchaguzi Huru" ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kwanini watu wasitamani kuchagua chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa?
  Ni jambo la kuudhi watu ndani ya nchi yao, kutaka wapige kura chini ya usimamizi wa wageni. Lakini wafanyeje iwapo wameridhika kuwa serikali yao imeshindwa kuheshimu misingi ya uchaguzi mzuri?
  Zipo kila sababu Umoja wa Mataifa kuombwa kusimamia uchaguzi wa Zanzibar. Kwa kuwa vitendo vya kiharamia vimekuwa ada katika hatua mbalimbali za uchaguzi tangu mwaka 1995, na kwa kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano nayo haijachukua hatua yoyote ya maana kudhibiti ushenzi huo, basi hiyo ni sababu nzuri ya Umoja wa Mataifa kuingia.
  Ni ujanja na majigambo ya bure viongozi wa SMZ kukemea na kulaani vilio vya wananchi na indhari ya balozi za Umoja wa Ulaya, Canada, Marekani na Japan kutaka uandikishaji wapiga kura ufanywe kwa misingi ya haki. Hata ningekuwa sehemu ya serikali nisingenyamaza. Ila sasa, natakiwa nitambue kuwa ujanja na mbinu zangu zimeanikwa.
  Ule ujasiri wa kujificha kwenye minjugu ukadhani huonekani wakati una shingo ndefu, hauna nafasi? Haufai nyakati hizi. Dunia ni chumba kidogo sasa wala si kijiji tena.
  Akiwa katika ziara ya nchi saba za Afrika, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, kila alipopita, alihimiza sana umuhimu wa uongozi unaofuata misingi ya utawala bora na haki za binadamu.
  Clinton anaamini – na ndivyo inavyoaminika na wapenda amani na maendeleo – bila ya kuwepo utawala bora na haki za binadamu (vyote vikifungwa pamoja katika dhana ya utawala wa sheria), hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kupatikana popote.
  Hii ni nukuu yake alipokuwa nchini Kenya: "Maendeleo ya kweli ya uchumi hayategemei tu kujituma kwa mamilioni ya watu wanaoamka kila siku na kufanya kila wanachoweza, mara nyingi katika mazingira magumu. Maendeleo mara nyingi hutegemeana na serikali wajibikaji ambazo hukataa rushwa na kufuata utawala wa sheria na kuleta matokeo mazuri kwa watu wao."
  Ni mafunzo kwa viongozi wa SMZ. Ni kuchukua na kuyatumia. Wanapoona hata watu wa kawaida wanatoa sifa nyinginezo za mtu anayestahili kuwa rais wa Zanzibar, hawajatambua tu kwamba kila mtu ameamka sasa?
  Wanaambiwa sasa "Zanzibar haihitaji rais mwenye tamaa ya kujilimbikizia mali yeye na familia yake pamoja na marafiki zake. Inataka achukie vitendo vya wizi wa mali ya umma, ubadhirifu na ufisadi, awe amepagawa na 'roho mtakatifu' na 'asiwe amepagawa na roho mtakavitu.'"

  Wafuate wasifuate, ni hiari yao. Hiari yashinda utumwa. Nifunge kwa kumsihi Hamza kwamba kamwe hawezi kuifichia SMZ madhambi. Ni hayo yanayoipa rekodi kuwa ni serikali yenye utawala katili.

  source: MwanaHalisi.
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Poleni sana. Ila kazi ipo sana na Allah atasaidia kuepusha madhara.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Labda anafuata nyayo za Shamuhuna...
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Baada ya 2010 tutegemee kuona list ya the Hague, haitakuwa tofauti sana na ile ya Kenya lakini tuwe wavumilivu kidogo tu mpaka hapo nyavu zitakaponasa wahusika kwani hawaoni, hawasikii, na pua zao zimekufa hawanusi,
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Naona kama yatamshinda maana asipopita Kwamtipura, ambako 2010 vita ya jimbo lake itakuwa kali sana, ndo itakuwa mwisho wake, mwenzake Juma Mrisho Matogo nimesikia kawa fundi makubadhi siku hizi. Hamza asitege kelele anazopiga za "kimasikani" zitamsadia, serikali ijayo "muujiza wa karne", asiache kufufua duka lake la kushona sidiria mapema, maana mtaji ndo ushaongezeka hivyo.
   
Loading...