Hamis Kigwangala kuhamia CHADEMA

Kuna taarifa za kuaminika kuwa Dr.Hamis Kigwangala Mbunge wa Nzega ameonesha nia ya kuhamia CHADEMA.

Kwa taarifa hizo zilizotufikia zinasema kwamba Kigwangala anatarajia kuhamia CHADEMA mara baada ya Bunge kuvunjwa June 30, 2015.

Atakutana na mwanafunzi wake aliyewahi kumtibu kichaa. Sijui kama wataelewana. Bado mengi yatajitokeza. Tusubiri.
 
Na waje tu kama wanakuja lkn style yao mi sijaipenda kwani wanapokuja kupitia mikutano na waandishi wa habari au mikutano mikubwa ni wazi kuwa wanahamia kwenye chama na status quo zao. Wanaendelea kuwa nation level kitu ambacho kina wavunja moyo vijana na wanachama wetu waliokipigania chama mpaka level hii kwa majasho na wakati mwingine damu zao. Ingekuwa pouwa zaid wangekuja kwenye chama waje kama wanachama wa kawaida na wakajenge chama kama sisi tunavyofanya huku kwenye misingi! Chama kimeshajengwa hiki na wajenzi wetu bado wapo na wana ari ya kufanya finishing pia bado wana ujuzi wa kutosha bila kuchanganya na hao waoga type ya kina kigwangala. Ki ukweli kama wanataka waje lkn mikia yao wakunjie ndani ya miguu yao. Wawe na adabu lkn wakumbuke huku cheo kinapatikana baada ya hard work ya kutoa chama level flan kwenda level ya juu nzuri. Hapa cdm tunafanya kazi kama mchwa. Kiufupi siungi mkono kupokea makapi
 
Kuna taarifa za kuaminika kuwa Dr.Hamis Kigwangala Mbunge wa Nzega ameonesha nia ya kuhamia CHADEMA.

Kwa taarifa hizo zilizotufikia zinasema kwamba Kigwangala anatarajia kuhamia CHADEMA mara baada ya Bunge kuvunjwa June 30, 2015.
Sema hivi anakohamia zitto ndiyo wataenda wote kundi la wezi na wapuuzi.
 
Kigwangala ni ccm damu haendi kokote, nami namuunga mkono abaki hapohapo mpaka,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,--------''''"""",,,,,,.
 
cc: HKigwangalla

Mheshimiwa soma thread hii uone jinsi unavyoboa watu.

CCM hawakutaki, soma hawa
Sema hivi anakohamia zitto ndiyo wataenda wote kundi la wezi na wapuuzi.

kigwangala siyo mtu wa kumuamini

Ikiwa ni ukweli basi ujuwe anachunguzwa na TAKUKURU na vyombo vingine vya uchunguzi kuhusiana na escrow.

Tutasikia na kuona mengi kuelekea uchaguzi, ya uongo haya, ya kweli haya, ya porojo haya.

Aende tu huko CHADEMA mtu mwenyewe akili hana

Huyu ana laana ya kumtelekeza baba yake, Aende tu mwana kwenda

Ahamie sasa hivi, asisubiri mwisho wa bunge.

na CHADEMA hawakutaki pia.

Jiulize kulikoni???????
 

Wanaojiandaa kujiunga ukawa wakimwagwa huko ugambani ni wengi sana. Lengo lao kuu ni kupitishwa kugombea nafasi haswa za ubunge. Wanachama wanasubiri kuona busara za viongozi wa ukawa watakavyowachukulia hawa wahamiaji haramu. Wakitaka kujiunga wachukuliwe kama wanachama wapya tu na wasipewe nafasi yoyote ya uongozi wala fursa ya kugombea nafasi yoyote. Pia wapewe miezi sita ya kupimwa.
 
tatizo ni mchumia tumbo uku cdm apawezi au kisa mwenyekiti wa mtaa wake anatoka ukawa nin?:clap2:
 
CCM Hapo mnapima upepo sio kweli huyo jamaa kuhama, nenda kaangalie chanzo cha kushinda ubunge wake ndio utajua
 
Huyu tunamfahamu sana, hana maana. Is a great opportunist. Hata haeleweki anataka nini wala kusimamia nini. Watu wa namna hii nyumbani kwao ni CCM.

Wawahi kabla hajafunga milango
 
wanamapinduzi hawabagui hawatengi huongeza nguvu ikibidi hata ya watoto ccm ni jabali linalotisha unahitaji kuongeza kila mmoja unayempata na kuwapunguza kwao hata watano kila asubuhi .kumbukeni hatuendi kugawana maini tunaenda kujena nchi iliyohujumiwa kwa mda mrefu
 
 

CCM tangu izaliwe imeishawahi kumfukuza nani zaidi ya Mansour Himid? CCM haina uwezo wa kumfukuza yeyote uanachama
 
Tunajua Dr Hamis Kigwangala ni member wa JF, kama unasoma thread hii basi wathibitishiea watu juu ya tetesi hizi. Je, ni kweli unahamia CHADEMA au si kweli?
 
Kuna taarifa za kuaminika kuwa Dr.Hamis Kigwangala Mbunge wa Nzega ameonesha nia ya kuhamia CHADEMA.

Kwa taarifa hizo zilizotufikia zinasema kwamba Kigwangala anatarajia kuhamia CHADEMA mara baada ya Bunge kuvunjwa June 30, 2015.
Bado bunge halijavunjwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…