kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,155
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa tamko na kuipongeza Korea Kaskazini kwa msimamo wake thabiti dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Siku chache zilizopita, Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini ilitoa tamko na sambamba na kutangaza kuliunga mkono kikamilifu taifa la Palestina ilisema, ni haki ya taifa hilo kupigania haki zake. Vile vile ilisema itauadhibu vikali utawala haramu wa Israel kwa kuthubutu kuuvunjia heshima uongozi wa nchi hiyo.
Katika taarifa yake hiyo, Korea Kaskazini imeutaja utawala wa Kizayuni kuwa 'mmiliki pekee haramu' wa silaha za nyuklia katika eneo la Mashariki ya Kati na hivyo ni tishio kwa usalama wa dunia nzima.
Kauli hiyo ya wakuu wa Pyongyang imekuja baada ya Waziri wa Vita wa Israel, Avigdor Lieberman kumtaja kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kuwa eti ni "mwendawazimu" ambaye anasimamia, "kundi la watu wenye misimamo mikali" ambao "wanavuruga utulivu wa dunia."
Kwa mujibu wa shirika la habari la Quds (Qudsuna), harakati ya HAMAS sambamba na kuishukuru Korea Kaskazini kwa kuunga mkono mapambano ya haki ya wananchi wa Palestina, imesema kwamba, HAMAS inaamini kuwa ukosefu wa amani na utulivu katika eneo hili unatokana na kuweko utawala wa Kizayuni ambao unaongoza vitendo vya kigaidi.
Msimamo mkali wa Korea Kaskazini dhidi ya Israel umewatia hofu viongozi wa utawala wa Kizayuni na kuwafanya waanze kulaumiana wao kwa wao. Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel amemlaumu vikali waziri wa vita wa utawala huo Avigdor Lieberman na kumwambia kuwa, kupayuka kwake kumeutia hatarini usalama wa Israel.
source;Parstoday.sw
My take; Hahaaa hivi korea na israel zingekua jirani kidogo umbali labda kama pale pakistani ilipo hahaaa sijui ingekuaje maana hawa ni wababe haswa