Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,188
- 10,668
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imeiomba Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ilisaidie taifa la Palestina katika kukabiliana na uvamizi na ukaliaji wa mabavu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Dk Ahmad Abu Halabiya, mjumbe wa mrengo wa "Mabadiliko na Mageuzi" katika bunge la Palestina wenye mfungamano na harakati ya Hamas, amewataka viongozi washiriki wa kikao cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kinachofanyika nchini Uturuki watekeleze majukumu na mas-ulia waliyonayo kuhusiana na kuiunga mkono Quds na kuuimarisha muqawama wa Palestina.
Abu Halabiya amesisitizia ulazima wa kufanywa jitihada na kuchukuliwa hatua za kuususia kisiasa na kiuchumi utawala wa Israel na kukomesha harakati zote za kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo na kuhakikisha viongozi wake wanashtakiwa na kuhukumiwa kwa jinai walizofanya dhidi ya wananchi na ardhi ya Palestina.
Mwanachama huyo mwandamizi wa Hamas amesisitiza pia juu ya umuhimu wa vyombo vya habari vya Kiarabu na vya Kiislamu kuzungumzia zaidi suala la Quds na malengo matukufu ya Palestina.
Katika siku ya kwanza ya kikao cha siku mbili cha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kilichoanza hapo jana mjini Istanbul, Uturuki, washiriki wa kikao hicho walisisitiza juu ya kuiunga mkono Palestina, kutatuliwa hitilafu baina ya nchi za Kiislamu na kuwa na umoja katika kupambana na ugaidi na misimamo ya kufurutu mpaka