HAMAS ilijiandaa hasa

The Whistleblower

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2022
Posts
269
Reaction score
459
Wakati HAMAS wanaivamia Israel October 7 na kuua kikatili Waisrael zaidi ya 1200 na wengine kuwachukua mateka, walijua wazi kuwa Israel wangelipa kisasi kikatili pia,na walijua kabisa kuwa maelfu ya raia wasio na hatia wakiwemo watoto wangeuawa.
HAMAS waliamua kuuza Damu za ndugu zao kwa Bei bure kabisa.
Kwa jinsi walivyokuwa wamejipanga , HAMAS waliamini kuwa wangeishinda Israel na kuumiliki mji wa Jerusalem pamoja na msikiti wa Alqsa.
Mbinu waliyoiamini HAMAS kuwa wataitumia na kushinda vita ni kupigana vita bila kuvaa sare za jeshi na kutumia Hospital na shule kujificha pamoja na makazi ya watu.
Israel ilijua mbinu za HAMAS,na ndo sababu raia wengi wasio na hatia wanakufa kwa sababu Israel inapiga mabomu popote walipo HAMAS baada ya intelligence yake kubaini.
Ni kazi ngumu sana kuwabaini HAMAS kwa sababu hawavai sare za jeshi na wanajichanganya na raia.
Israel isingepigana kikatili ingeshindwa vibaya mno hii Vita.
Kwa hiyo mauaji ya Gaza yametengenezwa na HAMAS wenyewe kwa sababu Israel inajilinda.
Ndoto za HAMAS ni kuwafuta wayahudi,kwa hiyo wasipokuwa makini watafutwa kweli.
There's no Genocide in Gaza, Israel defends itself.
 
Waendelee na vita hata wakipigwa hadi waishe sawa tu, vita inaleta heshima. Kufa kupo tu hata usipopigana vita kufa utakufa tu. Haki haiombwi, inadaiwa, na inapiganiwa. Sipendi ugaidi lakini vita vi vita.
 
Israel wakilemaa wanafutwa kweli; all possible means should be used to defend themselves! Nyoka ni nyoka tu awe mkubwa au mdogo ni kuuwa tu.
 
Ndio kitu nimekua nikiwaelimisha wafia haya mavitu akina brazaj yaani Israel ingetaka kufuta hapo Gaza wangepiga carpet bombing to na kila kitu kife, ila kwa sasa wanashambulia pale rockets zinakotokea, HAMAS hurusha mizinga wakiwa wamejificha katikati ya watoto, hivyo Israel hujibu na kupiga papo hapo.
Ingekua taifa la kikatili kama China au Urusi tungeongea mengine, wale hupiga bila kujali...

Israel wapambane tu maana ikitokea washindwe vita, watafutwa moja kwa moja, ndio maagizo kabisa kwenye dini ya uislamu, sijaandika mimi yapo kabisa kwenye maagizo ya vitabu vyao na naweka hapa kielelezo chenyewe

sahih muslim 2921
Abdullah b. 'Umar reported Allah's Messenger (ﷺ) as saying:
You and the Jews would fight against one another until a stone would say: Muslim, here is a Jew behind me; come and kill him.

 
Wewe una mapenzi na mahaba tu na Israel.Israel wanazingua sana, kuna watu wanaitwa Settlers wazungu kutoka Ulaya hawa - wakipenda nyumba yako - wanakutoa, ukizingua unakula chuma - Pale kuna uonevu mkubwa..
Pili hizo jamii mbili zote zina- ubaguzi: wanajiskia wote .Duniani watu wengi wameishachangamana- wayahudi wanajiona kama superior race - palestina nao hawataki kubaki inferior...kinachofuata mtifuano..Warudishe mipaka kabla ya 1967
 
Hivi kwa maandiko hayo Israel ikiuwa ili i-survive wana kosa gani. Maana hao maadui zao wameamrishwa na mungu wao wauwe wayahudi wore! Dunia inafahamu existence ya maandiko ya kutisha kama hayo?
 
Israel defend itself haiondoi genocide lakini sasa hakuna taifa la kuvumilia October 7 attack, Wapalestina 34,000 wamelala bila hatia lawama ziende kwanza kwa Hamas kabla ya kwenda kwa Israel, na huu ni mwanzo tu, as lonh as they is holding captives 102 na huku Israel ina captives zaidi 7000 ngoma bado mbichi, mpaka mwaka unaisha kutakuwa na umwagaji damu mkubwa.
 
Hamas wanatumiwa kufanikisha agenda za Israel, huo ndio ukweli
 
Pia viongozi wa Hamas wajifunze kwa Mandela baada ya Sharpville na SOWETO masscree na Mandela kufungwa miaka 27 lakini aliomba umoja na mshikamano kati ya wazungu na waafrika, aliona wazungu wana uwezo mzuri kwenye mambo ya uchumi na maendeleo kuliko waafrika bado akawacha washuke sector hiyo huku waafrika wajikite na mambo ya utawala wakishirikiana na wazungu bega kwa bega, ndo usalama wa South Afrika, ila kama waafrika wa South Afrika wangesema hawataki wazungu na wanataka waangamize waafrika wa South Afrika wangefutwa kabisa, kinachosumbua Palestinians na Israel ni dini, kama wayahudi wangekuwa waislamu au wapalestina wangekuwa ni wayahudi kwa dini basi vita hiyo isingekuwepo.
 

kama Wayahudi wangekua waislamu bado wangeuawa tu, ukanda huo kuna maugomvi mengi hata baina ya waislamu....
 
Kumbe sera ya Hamas ni kuifuta Israeli kwenye uso wa dunia.
Sera ya Kipumbavu kabisa.
Unalifutaje taifa kwa mawazo yako?
Huku ukiwa unachelelewa tu.
 
Yaani walokole kwa kuipenda Israel wanaamini ukiibaliki na ww utabalikiwa yaani aliewadanganya kaweza kweli wayahudi wamemuua hata huyo mungu wenu walimpga mpk wamemsulubisha na chupi hao ilibidi ndio wawe maadui wenu kwa waliyoyafanya kwa yesu lakini ndio mnawakumbati huko Israel wakristo wenzenu hawana hata uhuru wa kuabudu nyinyi huku mnawaabudu
 
Gaza hakuna vita bali Kuna kikundi Cha watu wameomba kupelekwa kwa Munyaazi wakiamini huko Wana fungu lao na Israel ameridhia ombi lao na ndicho anachotekeleza huko Gaza kwahiyo hizo story za vijiweni mzipuuze maana ni propapaganda .
 
ISRAEL wanatafutaga sababu ya kuangamiza palestine na palestina wantafuta sababu ya kuingamiza israel
sasa israel kapata sababu, hadi operation inaisha yatabaki magofu matupu kwa wapalestina
 
Kuna Israel mbili, kuna Israel ya propagandalist na Israel inayojulikana kwa usawa wake bila kujali Diversity zao.
Mimi ninaijua Israel ambayo Judge Muarabu aliwai kumhukumu Waziri mkuu myahudi kwenda jela miaka 6.
Lakini wengine wanaijua Israel ambayo mwarabu anawindwa kama digidigi ndani ya Israel.
 
Mimi kitu ambacho najiuliza kuhusu jeshi la israel ni kuwa. Jeshi la tanzania lilitumia chini ya wiki kuwachambua wanyarwanda katika nchi ya tanzania mwaka 2012 baada ya rais kusema. Hebu angalia ukubwa wa tz na udogo wa gaza kisha angalia. Hivi upelelezi wa jeshi la israel lilishindwa kuwatambua hamas kwa muda wote ambao wameishi nao hata kabla ya shambulio la october 7. Hivi tukipeleka tiss pale gaza miezi 6 haiwezi ikaja na orodha ya wanamgambo wa hamas na sura zao kiasi kwamba muda wa kuwauwa tukatumia tu hata bastola? Maana ni kumfata mumoja baada ya mwingine
 
Ila kipigo walichopata gaza ni hatari sana kumebaki magofu matupu netanyahuu aliapa kipigo atakachowapa kitakuwa historia kwa magaidi na vizazi vyao israel sio taifa la kuchezewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…