Hamad Rashid ataka Maalim Seif afungwe

Hamad Rashid ataka Maalim Seif afungwe

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]
Hamad-Kikao(2).jpg
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 20 August 2012 08:59 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

James Magai

MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake wameendelea kuwang’ang’ania wadhamini wa Chama cha Wananchi (Cuf), wakiiomba Mahakama Kuu iwatie hatiani na kuwafunga kutokana na kitendo cha kufukuzwa kwao uanachama.
Licha ya wadhamini hao, wengine ni wajumbe wa Baraza Taifa la Uongozi la chama hicho akiwamo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad. Januari 10, mwaka huu Rashid na wenzake 10 waliwasilisha mahakamani hapo maombi wakitaka iwaite wadhamani wa chama chama hicho, wajieleze sababu za kutotiwa hatiani na kufungwa kwa kosa la kupuuza amri ya mahakama.
Maombi hayo yalitokana na uamuzi wa Baraza la Taifa la Uongozi la chama hicho wa Januari 4, mwaka huu kuwafukuza uanachama wa chama hicho na kuwasimamisha wengine. Pia, katika maombi hayo wanaomba mahakama ibatilishe uamuzi wa Baraza hilo wa kuwavua uanachama kwa madai kwamba walikiuka Katiba ya Cuf.
Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, Hamad na wenzake katika hoja zao za maandishi walizoziwasilisha mahakamani kupitia kwa Wakili wao, Augustine Kusalika wanadai baraza hilo liliwafukuza uanachama wakati tayati likiwa na amri ya mahakama kuzuia kuwafukuza.
Amri hiyo ya mahakama ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa Januari mwaka huu kufuatia maombi waliyoyawasilisha Januari 3, chini ya hati ya dharura. Mwisho

Chanzo mwananchi
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Hivi kumbe Hamad hajafukuzwa!!!! Sheria tamu kweli hasa kale kakipengele ka Court Injunction kana neno tamu linasema status quo! Hiyo status quo inaweza kudumu kwa miaka 5 yaani bunge likaisha jamaa ana status quo!
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]
Hamad-Kikao(2).jpg
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 20 August 2012 08:59 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
James Magai

MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake wameendelea kuwang’ang’ania wadhamini wa Chama cha Wananchi (Cuf), wakiiomba Mahakama Kuu iwatie hatiani na kuwafunga kutokana na kitendo cha kufukuzwa kwao uanachama.
Licha ya wadhamini hao, wengine ni wajumbe wa Baraza Taifa la Uongozi la chama hicho akiwamo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad. Januari 10, mwaka huu Rashid na wenzake 10 waliwasilisha mahakamani hapo maombi wakitaka iwaite wadhamani wa chama chama hicho, wajieleze sababu za kutotiwa hatiani na kufungwa kwa kosa la kupuuza amri ya mahakama.
Maombi hayo yalitokana na uamuzi wa Baraza la Taifa la Uongozi la chama hicho wa Januari 4, mwaka huu kuwafukuza uanachama wa chama hicho na kuwasimamisha wengine. Pia, katika maombi hayo wanaomba mahakama ibatilishe uamuzi wa Baraza hilo wa kuwavua uanachama kwa madai kwamba walikiuka Katiba ya Cuf.
Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, Hamad na wenzake katika hoja zao za maandishi walizoziwasilisha mahakamani kupitia kwa Wakili wao, Augustine Kusalika wanadai baraza hilo liliwafukuza uanachama wakati tayati likiwa na amri ya mahakama kuzuia kuwafukuza.
Amri hiyo ya mahakama ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa Januari mwaka huu kufuatia maombi waliyoyawasilisha Januari 3, chini ya hati ya dharura. Mwisho

Chanzo mwananchi[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Muandishi amekosea kidogo hapo, alitakiwa aseme "afungwe JELA" Maana kuna kifungo cha nje......sasa anachotaka MHE. Hamad Rashid yeye anataka wafungwe jela na sio kifungo cha nje au faini. Jela! Baaaasi
 
Hahaha afungwe jela akanyolewe ndevu zake ili ajue Nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria. Yani Makamu WA Raisi anadharau Amri ya Mahakama! Huyu ni jela tu! Hahahaaaa.
 
Amuulize Yusuf Raza Gilan wa Pakstan. Aliichezea mahakama na mahakama ikamvua Uwaziri Mkuu!
 
Hata bila kuingia kwenye undani wa sheria, maalim Seif na mwenzake Lipumba wameishiwa kulhali. Wamekiuza chama kwa magamba na kujifucha nyuma ya serikali ya umoja. Serikali ya umoja gani iwapo inamnufaisha mmoja yaani Seif aliyewekwa kinyumba kwa kupewa cheo kisicho hata kuwepo kikatiba ukiachia mbali kutengwa huku makamu wa pili akionekana kuwa mtendaji? Seif, Mrema, Lipumba, Cheyo, Mbatia, Dovutwa na nyemelezi wengine wa kisiasa wanapaswa kuondolewa kwa njia yoyote inayokubalika kisheria. Hawafai zaidi ya kuhangaikia matumbo yao.
 
huyu bahamadi aage wenziwe tu hapo bungeni kwani hatorudi tena hapo labda apitie kwengine ,chadema hamumtaki huyu jamaa ?
 
Nafikiri angeachana tu na cuf na kujiunga na cdm
 
I hope watanganyika ifikapo 2015 mtahakikisha kua cuf haipati jimbo hata moja huku bara kwa kua tunajua ni chama cha kigaidi na sio chama kinachojali maslahi ya wana bara so tafadhalini uchaguzi ujao wapigwe wote chini pamoja na mwenye kiti wao na mchague chama kitakacholinda maslahi ya watanganyika
 
Wewe sema hapo ,CDM haigaiwi tena jimbo 2015 usijifanye hujui kama CUF ilipokonywa ushindi na kupewa nyinyi yule aliewagaia bado hajafa.
 
kwa sasa anakusanya pesa kwa ajili ya kuimarisha chama chake cha ADC kitakapo pata usajili wa kudumu
 
Wewe sema hapo ,CDM haigaiwi tena jimbo 2015 usijifanye hujui kama CUF ilipokonywa ushindi na kupewa nyinyi yule aliewagaia bado hajafa.

ile thread yako ya kijinga moderators wameifuta ..... teh teh teh
 
Ba Hamadi. Siku zote ukipanda upepo utavuna Dhorba. Sasa kazi kwako.

Siku zote kama hutakiwi kwenu basi Ng;atuka.
 
aah, kumbe Mkuu Baru kuna siku nawe unamwaga Hekima! Hapo ulichosema nakuunga mkono! Ba Seif cuf iko mdomoni lakini rohoni kipo kitu kingine! Na asipo ng'atuka asubiri dhoruba! Asijidanganye kutembea na motorcade akafahamu inawapendeza wanacuf!
 
Back
Top Bottom