Hamad Rashid ainyooshea kidole CUF

Hamad Rashid ainyooshea kidole CUF

mkada

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
1,200
Reaction score
908
Mbunge wa Wawi (CUF) Hamad Rashid Mohammed, alisema Zanzibar itaingia katika machafuko makubwa endapo hakutafanyika jitihada za haraka kukomesha chuki za kidini zinapandikizwa miongoni mwa raia wake.
Alisema hali si shwari visiwani humo, akiifananisha na ‘yai jeteta' ambalo kupasuka kwake, kunaathiri watu wote.
Hamad alisema kihistoria Zanzibar ni nchi iliyokuwa na watu wenye uvumilivu wa kidini kwa miaka mingi na hakuna aliyetarajia siku moja watu watatengana na kuhujumiana kwa sababu ya tofauti za kiimani.

Alisema matukio ya kumwagiwa tindikali kwa Katibu wa Mufti Fadhili Soraga na tukio la hivi karibuni Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae kupigwa risasi na watu wasiojulikana ni baadhi ya matokeo ya chuki hizo zilizopandwa na wanasiasa.
"Hali ya Zanzibar inasikitisha sana, matukio yote mawili ya kujeruhiwa viongozi wa kidini ni jambo la kulaaniwa kwa nguvu zote na inathibitisha kuwepo kwa watu wanaochochea hali hiyo kwa manufaa yao," alisema Hamad.
Alisema kumekuwepo na viongozi wa kisiasa wanashindwa kukemea hadharani jambo hilo kwa sababu wanahusika kuwashawishi na kuwachochea viongozi wa dini kushiriki vurugu hizo.

"Uongozi wa kisiasa umeshindwa kukemea kwa sababu kuna baadhi ya wanasiasa wanahusika, wakati mwingine wanakwenda kwa viongozi wa dini zote kuchochea, lakini ikumbukwe ikitokea vurugu hakuna atakayepona," alisema.

Mbunge huyo asiyetambuliwa na Chama Cha Wananchi (CUF) alichokitumia kugombea na kushinda kiti hicho, alisema suluhu ya tatizo hilo ni kuanzishwa mjadala wa kitaifa kujadili kuhusu chanzo halisi na namna ya kufikia suluhu ya kudumu.
Pia Hamad alisema hakuna viongozi wenye maoni na nguvu ya kuzuia jambo hilo, kwa vile viongozi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa wanatofautiana kiitikadi.

Katika suala hilo alionyesha kufadhaishwa na msimamo wa viongozi wa CUF kutokuwa na upande wa kusimamia kuhusu Muungano, moja ya madai yanayotajwa kutumika kama kigezo cha kuchochea vurugu visiwani humo.
"Ndani ya CUF kuna watu wanataka Muungano wa Mkataba na wengine wanataka Muungano wa serikali tatu, tofauti na CCM ambao wana msimamo mmoja wa serikali mbili," alisema.

"Hili ni jambo baya sana kwa viongozi wa CUF kutokuwa na msimamo wa kimaadili, haiwezekani chama kuwa na makundi mawili yenye tofauti ya msimamo, kutokana na hili huwezi kusimamia serikali hata mara moja," aliongeza kusema.
Naye Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alielekeza lawama kwa jeshi la polisi na kusema linafanya kazi kisiasa na kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Profesa Lipumba alisema kama polisi wangefanya kazi kwa weledi na kuachana na kutumika kisiasa, matukio yanayotokea Zanzibar yasingekuwepo kwa sababu wahusika wote wangekamatwa.
Hata hivyo alipinga hoja ya Hamad kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imeshindwa kutekeleza wajibu wake katika kuidhibiti hali hiyo......Source Mzalendo.net
 
Huyu naye tumemchoka na ubunge wake wa mahakamani , si aende zake ADC !
 
Back
Top Bottom