Hama hama ya watangazaji wa radio za Bongo, maana yake ni nini!?

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Watangazaji sasa wanabadilisha vituo kama team za soccer.

Gadner katoka Efm kaenda Clouds.

PJ na Hando wametoka Clouds wameenda Efm.

Jabir saleh na Bi Hindu wametoka Times fm wameenda Efm.

Dj Senyorita na Mami wametoka East Africa radio wameenda Clouds.

Kuna tetesi Clouds sasa wanamtaka Kitenge kwa pesa yoyote anayotaka, Kitenge akichukuliwa na Clouds Shafii amesema ataondoka na Efm wanataka kumchukua kwa pesa ndefu.

Ni mwendo wa kutangaziana dau.

Hapa haieleweki ni jeuri ya pesa?

Stunt za kuongeza kusikilizwa?

Tasnia chovu ya utangazaji inakua?

Nani anaefaidika na hii game?

Au umjini mjini?

Efm wanakwambia huu mchezo hauitaji hasira!

Tusubirie kuona mwisho wa huu mchezo au labda ndio mwanzo wa sinema.

Mjini kuzuri sana!
 
Ngoja Lemutuz na yeye afungue radio yake am sure atakomba watangazi wote, ila kwenye ishu hii naona wamiliki wa radio ndio ambao wanacheza na akili za watangazaji kwamfano issue ya PJ na Gerard hando unawezaka kukuta labda efm waligoma kumuachia gardnar mpk wapewe hawa hando na PJ kama soka tu vile
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom