Halotel wanatuibia kwenye bundle la intaneti

Mutu Imara

New Member
Joined
Aug 19, 2021
Posts
0
Reaction score
1
Nilinunua intaneti yenye mega bite (MB) 1024 kutoka kwny kifurushi cha wiki cha Mega bundle,ila cha ajabu kila nikifungua video zinachukua muda mrefu sana kufungua au mara nyingine hazifunguki kabisa,nikijaribu kupiga simu katika kitengo cha huduma kwa wateja simu zao zinakuwa zinatumika muda wote (busy)

Sasa imebaki siku moja kifurushi kiishe muda wake na sijaweza kukutumia.

Huu sio wizi jamani?
 
Pole. Ikiisha nunua la week tena ata la buku, linafufua lile lililoexpire.

Hapa ndio ninapo penda Halotel.

Mfano mimi nanunuaga la week. Nikiwa na hela nanunua GB7 kwa buku 5. Kiki expire nazimua na MB 500 ya buku kwa wiki inafufua ata ile ilioexpire.

Jana nilinunua la buku.


Ikafufua ilioexpire.

 
Ni kweli kabisa mimi hununua ile ya mwezi ya 4G GB 10 kwa elfu 10. Ikikaribia kumalizika muda na bado kuna GB zangu 4 naongeza cha wiki cha elfu mbili then inaunganishwa na salio langu la 4gb maisha yanasonga.
 
Hii itakuwa kwako tu
 
Vifurushi vyao bei nafuu sawa shida ni accessibility hapo ndo kuna mziki
 
Mimi nilizinduka kitambo mkuu nina zaidi ya miezi mitatu sijaitumia line yao, hata ulaji wa mb uko kasi sana, saiv naunga 1gb kwa sh elfu moja voda natumia siku 4, naridhika kwa kweli.
 
Nimewapigia Leo baada ya dk 5,akapokea nimempa mashiti makavu makavu bi dada mmoja.Internet slowly,mda mwingine bando linakata haraka hata kama naperuzi vitu vya kawaida . wonderful enough kwenye huduma ya nmb mobile nalipia bidhaa kupitia huko ,aisee mtandao hovyo mda mwingi na ukiingia mara nyingi makato ni ya hatari.
 
Duh,hii ni kwa line zote za halotel au zile special,.?? Mimi mbona sipati🙄🙄 Ila hawa jamaa wanakuja kasi kwa utapeli,😏
 
Halotel kwa upande wa internet ni ovyo kabisa. Speed in ya Kobe kwa maeneo mengi.
 
Hizo 7GB kwangu ni siku 3 tu zinaisha. Una matumizi mazuri sana
 
Halotel ni.....
Hiv inakuaje matumiz y data zinatofautiana
Mfano mb za voda zinakaa san il sio halotel
Kwann zitofatiane
 
Halotel wezi kwenye bundle la internet
Ukiweka paaaap umeisha unabakia kujishangaa ni nini umetumia,yaan sasa nimewhama bora tigo
 
Mimi nilizinduka kitambo mkuu nina zaidi ya miezi mitatu sijaitumia line yao, hata ulaji wa mb uko kasi sana, saiv naunga 1gb kwa sh elfu moja voda natumia siku 4, naridhika kwa kweli.

Unanuniaje mkuu coz mwenyewe natumia Vodacom
 
Hao wangese nimewachoka leo nilikuwa nangoja wanao sajili laini nihame limtandao lao la kifisadi bando halikai uwashe data usiwashe
Kwamba ukizima simu usiku ukiwasha asubuhi unakuta bando limeisha
 
Nimejionea jana bando la 700mb limeisha hata kufungua video sijafungua
 
wako hao wengine ni hatari sana wanakwambia 500 unapata mb 200 na muda lukuki weka sasa uone kazi
 
Mimi nilizinduka kitambo mkuu nina zaidi ya miezi mitatu sijaitumia line yao, hata ulaji wa mb uko kasi sana, saiv naunga 1gb kwa sh elfu moja voda natumia siku 4, naridhika kwa kweli.

Unajiungaje mkuu?
 
wako hao wengine ni hatari sana wanakwambia 500 unapata mb 200 na muda lukuki weka sasa uone kazi
Akina Tigo nahis unawaongelea, naungaga halo kwa mwez ya elf40 ila kasi yao sometyms inasikitisha, kupata LTE kasi kabisa ni maeneo machache
 
Mwenye HALOTEL
*148*28#
Chagua ofa hlf angalia kati ya hizo aina za simu zilizoandikwa yako ipo
Kama ipo unapata ofa yako kuanzia mb 100 mpk gb 5 na dk nyingi za kupiga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…